Wednesday, October 28, 2020

Hawa ndio watabeba taji Ligi Kuu England

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Manchester, England

BAADA ya Manchester United kuonyesha soka bovu wakiwa ugenini dhidi ya Liverpool, imetoa picha ugumu wa vita ya kuwania taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Timu mbili ambazo zina matarajio ya kuwania taji hilo la Ligi Kuu England zilikutana katika mechi ambayo timu zote zikipambana kuepuka kupoteza mchezo huo katika msimu huu mpya wenye mechi nane mpaka sasa. Inaweza ikawa si mara ya mwisho mechi kubwa kumalizika kwa mtindo huo, ingawa kwao huenda wakawa wamefurahishwa nayo.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, ameizungumzia klabu hiyo akisema kwamba sasa Jose Mourinho atajua kwamba kikosi chake hakina nafasi ya kunyakua taji la Ligi Kuu England ikifika Mei mwakani.

Hivyo ni klabu gani itaipora Leicester City taji hilo la England? Mtandao wa Sportsmail umeangalia timu zenye uwezekano wa kuwa mabingwa baada ya mechi 30 zijazo.

 

MANCHESTER CITY

Kikosi ambacho kipo vizuri kwenye Ligi Kuu England kwa sasa ni cha kocha Pep Guardiola, Manchester City, ambao wanaongoza ligi kwa tofauti ya bao moja dhidi ya Arsenal.

 

City kutokana na kuwa na wachezaji wazuri wenye vipaji chini ya kocha Manuel Pellegrini miaka kadhaa iliyopita, ukijumlisha na wale walioongezwa majira ya kiangazi, kocha mpya, Guardiola atakuwa na uhakika wa kunyakua taji na kuongeza hazina yake ya mataji pamoja na yale aliyoyachukua Hispania na Ujerumani.

Kuwa fiti kwa Sergio Aguero ni moja ya kigezo muhimu kwao, lakini kutokana na adhabu aliyokuwa amepewa mwanzo wa msimu ilionyesha kwamba City wanaweza kufanya vizuri bila ya mshambuliaji huyo wa Argentina.

Kwingineko, kuna kiwango, ubora na wachezaji wa kutosha kwa kila nafasi uwanjani.

Kutokana na udhaifu waliouonyesha dhidi ya Tottenham na kuambulia kichapo cha mabao 2-0, lakini City bado wana uwezo wa kuongoza msimu huu.

Wanapewa alama: 8/10 

 

ARSENAL

Arsene Wenger anaweza akafanikiwa kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kufanya hivyo miaka 12 iliyopita? Madhaifu ya kila mara yanaweza kujitokeza na kuzima ndoto zao, lakini kuna dhana kwamba hii ni Arsenal bora sana kuwahi kutokea katika muongo mmoja.

Ushindi wa kishindo dhidi ya kikosi kikali cha Chelsea, ukiambatana na pointi tatu muhimu kutoka nyumbani mwa Burnley, kisha ushindi mwingine nyumbani dhidi ya Swansea City, umewafanya Gunners kuwa na wiki kadhaa za furaha.

Kipindi cha baridi na majeruhi ndio kitakuwa kipimo, lakini wakiwa na Shkodran Mustafi na Laurent Koscielny, timu hii inaonekana kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi kuendana na safu yao ya ushambuliaji yenye vipaji lukuki.

Arsenal wamepoteza mechi moja ndani ya miezi saba. Wakionekana kuwa kwenye kiwango kizuri cha kuitoa City kwenye usukani wa ligi.

Wanapewa alama: 7/10

 

TOTTENHAM

Kikosi hicho cha Mauricio Pochettino kilikuwa kinakosa ile nguvu ambayo walikuwanayo msimu uliopita na kuwa moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kunyakua taji hilo la Ligi Kuu England, lakini sasa wana mwaka mmoja wakiwa na uzoefu huo.

Ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa katika ligi tatu za soka la England, huku wakionyesha kwamba wana uwezo baada ya kuichapa City kwenye Uwanja wa White Hart Lane.

Uwepo wa Victor Wanyama unaongeza thamani kwenye kikosi hicho pamoja na kununuliwa kwa thamani ya pauni milioni 12, huku Son Heung-min akiwang’arisha Spurs kwa mabao yake. Je, Spurs wanaweza kuendelea na kasi yao pamoja na kuwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya?

Wanapewa alama: 7/10

 

 

LIVERPOOL

Jurgen Klopp huenda akawa ndiye kocha mwenye timu inayovutia Ligi Kuu England, ingawa hakuna aliyeweza kung’ara mbele ya United mwanzoni mwa wiki.

Kocha huyo wa Ujerumani amekuwa na mwaka mmoja wa kujenga kikosi chake na ubora wao kwenye kukaba kwa kulazimisha umeweza kuleta majanga kwa Arsenal na Chelsea katika msimu huu.

Kuna mambo kadhaa, kama kipigo dhidi ya Burnley yanaonyesha ugumu walionao na kuwapa nafasi ndogo kwenye mbio za ubingwa huo.

Ukizingatia mechi ya juzi dhidi ya Man United, ndio ulikuwa ni mchezo wao wa kwanza kucheza bila ya nyavu zao kutingishwa na kuonyesha kwamba wana tatizo katika safu ya ulinzi. Hivyo wanaweza kufunga mabao mengi na kufungwa mengi.

Wanapewa alama: 6.5/10

 

MANCHESTER UNITED

Jumatatu usiku ilikuwa ni siku ambayo Mourinho angeonyesha kwamba hana uwezo wa kuipa klabu yake ya Man United taji la Ligi Kuu England msimu huu, lakini hakuna shaka kwamba klabu hiyo ya Old Trafford bado ni tishio kwa timu zilizo kileleni.

Majira ya kiangazi Man United wametumia zaidi ya pauni milioni 150 bila shaka itaifanya timu hiyo kuwa hatari zaidi ya City, ukizingatia bado hatujaona cheche za kiungo Henrikh Mkhitaryan.

Ingawa kuna matatizo. Paul Pogba anatakiwa kuonyesha kiwango chake na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, anatakiwa kuendelea kupachika mabao, hapo ni bila ya kuangalia matatizo ya nahodha wa England na klabu yao, Wayne Rooney.

Beki huyo wa zamani wa Man United, Neville huenda akawa anasema hakuna uwezekano wa klabu hiyo kunyakua mataji. Mourinho, anaweza akaonyesha hilo, akiwaziba midomo wanaomtilia shaka, hata kama mwanzoni mwa wiki hii (Jumatatu) hakuonyesha dalili za kuweza kufanya hivyo.

Wanapewa alama: 6/10

 

CHELSEA

Kocha Antonio Conte, amekuwa akiambulia matokeo mabaya kutokana na kutumia mfumo wake mpya wa 3-4-3, akiwa na wachezaji ambao walinyakua taji la Ligi Kuu England 2014/2016. Wakiwa hawana ratiba za Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kuna maswali mengi yasiyo na majibu juu ya kikosi hicho cha Chelsea. Kushindwa kwao kufanya vizuri msimu uliopita inakuwa ngumu kuweza kuwategemea kufanya lolote na maswali yanabakia kwa wachezaji tegemeo wa kikosi hicho.

Mfumo huo mpya katika safu yao ya ulinzi inaweza ikawa imefanikiwa kwa vikosi vinavyojikongoka Hull City na Leicester City, lakini kipimo chao kitakuwa ni safari yao ya Manchester kwenye Uwanja wa Old Trafford, Jumapili hii.

Wana kocha ambaye anajua mbinu za kuweza kunyakua mataji, akifanikiwa kubeba taji akiwa England itaonyesha uwezo wa kocha huyo wa Italia, Conte.

Wanapewa alama: 5.5/10

 

EVERTON

Moja ya timu ambayo inaweza kushangaza kuingia kwenye orodha ya timu saba zinazopewa nafasi ya kunyakua taji la Ligi Kuu England baada ya mechi saba kwenye msimu huu mpya ni kikosi cha Ronald Koeman, Everton ambao wamefanikiwa kujiweka nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo.

Wamekuwa timu ya kwanza kuweza kubeba pointi moja katika uwanja wa Etihad mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini wameshindwa kupata ushindi katika michezo yao minne ya michuano mbalimbali.

Toffees wakiwa chini ya kocha wao mpya, Koeman wameshindwa kuongeza nguvu kwenye baadhi ya maeneo na kuifanya timu hiyo ionekane kukosa kasi nzuri.

Ikiwa na mshambuliaji wao, Romelu Lukaku, ataendelea kuwa fiti bila kushuka kiwango akipachika mabao itakuwa nafasi nzuri kwao kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya na watakuwa na nafasi ndogo ya kuchukua ubingwa.

Wanapewa alama: 4.5/10

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -