Thursday, December 3, 2020

HAWA NDIO WATAKUWA KIVUTIO EL CLASICO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MADRID, Hispania

MIAMBA miwili ya soka duniani, Barcelona na Real Madrid, leo inakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania, La Liga, maarufu kama El Clasico, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Mbali na kuikutanisha miamba hiyo, mechi hiyo pia inawakutanisha wachezaji wawili duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, ambao kila mmoja atakuwa akitaka kuonesha ufalme wake.

Mwisho miamba hao kukutana ilikuwa ni kwenye uwanja huo wa Camp Nou, ambapo Real Madrid waliinyuka  Barca  mabao 2-1, yaliyowekwa kimiani na staa wao, Cristiano Ronaldo.

Hata hivyo, pamoja na kuwa vikosi hivyo vimesheheni nyota kadhaa, lakini kuna wengine ambao wanatarajiwa kuwa kivutio katika mtanange huo ambao ni kama ifuatavyo:

1.Marcelo – Real Madrid

Licha ya timu hiyo kuwa na nyota kadhaa kama Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, lakini  Marcelo anaonekana atakuwa kivutio kikubwa kutokana na  uwezo wake wa  kutengeneza pasi, kupanga safu ya ulinzi na huku akisaidia mashambulizi.

Katika orodha ya  wachezaji wa  Real Madrid,  Marcelo msimu huu anashika nafasi ya nne kwa kutengeneza mabao  katika michuano ya  La Liga, akiwa na asilimia 1.3,  akizidiwa  kidogo  na  Bale, mwenye asilimia 1.4.

Mbali na hilo, staa huyo anashika nafasi ya nne kwa kutoa pasi muhimu, akifanya hivyo kwa asilimia 1.3 kwa kila mechi, akiwa nyuma dhidi ya Bale, Dani Carvajal na Toni Kroos.

Marc-Andre Ter Stegen – Barcelona

Licha ya kuwa tegemeo kwa Barcelona kutokana na uwezo wake wa kuokoa mpira, staa huyo amekuwa akifanya makosa ya kizembe ambayo yamekuwa yakiigharimu timu.

Hata hivyo, katika mechi ya leo, staa huyo haitarajiwi kama atafanya hivyo, hususan baada ya kuboronga dhidi ya Celta, ambapo aliigharimu Barcelona.

Kwa sasa kasi yake ya kupangua michomo inaonekana kuimarika, kwani amefanya hivyo kuliko mlinda mlango yeyote  wa La Liga, sawa na asilimia 20 kwa kila mechi.

Luka Modric – Real Madrid

Licha ya kuwa amekuwa akicheza kama kiungo mkabaji, lakini staa huyo mara nyingi amekuwa akifanya kazi ya kukaba.

Staa huyo huwa anafanya hivyo wakati Real Madrid inapokuwa imeelemewa na mashambulizi ambapo hulazimika kuyapunguza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -