Thursday, October 22, 2020

Hawa sio wa mchezo mchezo England

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

London, England

MECHI saba za Ligi Kuu England zimeshaanza kutoa picha ya timu zinazoweza kunyakua ubingwa msimu huu.

Lakini jambo muhimu kwa timu zinazopewa nafasi ya kunyakua ubingwa itakapofika Mei mwakani ni safu zao za ushambuliaji.

Kuna timu kubwa ambazo zilinunua wachezaji na nyingine zilifanya mabadiliko ya ndani na zile ambazo zilibakia kama zilivyo. Je, zitawezaje kunyakua ubingwa?

CHELSEA

Washambuliaji: Eden Hazard/Diego Costa/Willian

Benchi: Michy Batshuayi

Kocha Antonio Conte alihusishwa na mpango wa kusajili wachezaji mbalimbali majira ya kiangazi, mmojawapo akiwa ni Romelu Lukaku. Lakini mwisho wa siku walifanikiwa kumnasa Michy Batshuayi pekee kwa pauni milioni 33 kutoka Marseille. Alifunga kwenye mechi yake ya pili na kuongeza mawili katika mechi ya EFL Cup ‘Kombe la Ligi’,  lakini hadi sasa mabao yamekauka kwa Batshuayi. Ila hilo si tatizo, kwa kuwa kiwango cha mshambuliaji Diego Costa, ambaye anaweza kuwanyamazisha wapinzani wakati wowote kiko juu.

Baada ya msimu uliopita kuwa mbaya kwake na kufunga mabao 12, Costa ameshapachika mabao sita msimu huu, ambayo yanamfanya kuwa kinara wa mabao. Ameungana na wenzake, Eden Hazard na Willian, ambao wametupia mabao mawili kwenye mechi moja. Willian anaonekana kurejea kwenye kiwango chake cha msimu uliopita na Hazard ameanza kuonyesha soka lake, ambalo lilimpa tuzo ya PFA msimu wa 2014/15.

Mabao:

Diego Costa 6

Eden Hazard 2

Willian 2

Michy Batshuayi1

MAN CITY

Washambuliaji: Raheem Sterling/Sergio Aguero/Nolito

Benchi: Kelechi Iheanacho

Wakati Sergio Aguero alipopata majeraha, Manchester City, wamekuwa wakionekana kuwa dhaifu, hiyo ni kutokana na ubora wa nyota huyo wa Argentina. Lakini wakati akiwa nje akitumia adhabu ya kosa la kumpiga kiwiko nyota wa West Ham, Winston Reid, Kelechi Iheanacho aliziba pengo lake vizuri akifanikiwa kufunga bao kwenye mechi dhidi ya mahasimu wao, Manchester United.

Raheem Sterling, ambaye alidhaniwa kwamba angetimuliwa na kocha Pep Guardiola, amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza msimu huu. Amepachika mabao manne na kupika mawili na kumfanya aonekane kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alistahili kununuliwa kwa pauni milioni 44 kutoka Liverpool mwaka jana.

Upande mwingine ni nyota aliyesajiliwa majira ya kiangazi, Nolito, ambaye amepachika mabao kadhaa tangu ametua Etihad.

Wakati washambuliaji wa City wanauwasha moto, kinachowafanya wang’are ni uwepo wa Kevin De Bruyne nyuma yao. Nyota huyo tayari amepika mabao manne msimu huu.

Mabao:

Sergio Aguero 5

Raheem Sterling 4

Nolito 2

Kelechi Iheanacho 2

TOTTENHAM

Washambuliaji: Erik Lamela/Harry Kane/Son Heung-min

Benchi: Vincent Janssen

Tottenham wanafanya vizuri sana kwa sasa, wakionyesha hilo katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Man City na kuwafanya kuwa timu pekee ambayo haijafungwa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu England, huku wakionekana kuwa na safu ya ushambuliaji hatari.

Wakati mshambuliaji wao tegemeo, Harry Kane amepata majeraha, nyota Vincent Janssen, aliyesajiliwa majira ya kiangazi, alitarajiwa kuonyesha kiwango cha juu, lakini Mholanzi huyo alishindwa kufanya hivyo na mpaka sasa hajafunga hata bao moja.

Bahati nzuri kwa Tottenham ni kwamba mchezaji Son Heung-min amekuwa kwenye kiwango cha pekee, akifunga mabao ya ushindi dhidi ya Middlesbrough kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow. Ataendelea kufanya hivyo hata Kane atakaporejea?

Spurs wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, lakini wamefunga mabao machache kuliko kikosi kingine isipokuwa Chelsea, ambao wanalingana kwa mabao 12.

Mabao:

Son Heung-min 4

Harry Kane 2

Erik Lamela 1

Vincent Janssen 0

ARSENAL

Washambuliaji: Theo Walcott/Alexis Sanchez/Alex Iwobi

Benchi: Olivier Giroud, Lucas Perez

Mashabiki wa Arsenal wanaweza wakakwambia Olivier Giroud hana lolote na watakuwa wanahisi kwamba Arsene Wenger ameingia kwenye akili zake na kuamua kumnunua Lucas Perez majira ya kiangazi, ili kutoa msaada. Ukweli ni kwamba, kila mmoja analo jibu, ambalo ni kiwango cha Alex Iwobi na majeruhi Giroud ndiyo yamemhamisha Alexis Sanchez kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Ndiyo maana Sanchez amecheza kama mshambuliaji wa kati, huku Giroud akiendelea kuuguza majeraha ya kidole gumba na Perez bado hajapata nafasi. Hiyo imemfanya nyota wa Chile kuonyesha makali yake. Huku Walcott akiendelea kung’ara katika kila mechi na kuwa tishio. Lakini moja ya kivutio katika safu hiyo ya ushambuliaji ya Arsenal ni Iwobi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 ameonekana kama ameanza kupangwa kwenye kikosi cha kwanza cha Gunners kwa miaka minne iliyopita, jambo ambalo limemfanya Sanchez kuhamishwa kwenye nafasi ya mshambuliaji na kumwacha Iwobi akicheza winga wa kushoto.

Kama Mesut Ozil ataanza kupika mabao kama alivyofanya msimu uliopita, ambapo kwa sasa hajatoa ‘assist’ hata moja, lakini ataanza kupika mabao basi safu hiyo inaweza kuipa Gunners taji msimu huu.

Mabao:

Alexis Sanchez 4

Theo Walcott 3

Olivier Giroud 0

Alex Iwobi 0

Lucas Perez 0

LIVERPOOL

Washambuliaji: Sadio Mane/Roberto Firmino/Philippe Coutinho

Benchi: Daniel Sturridge

Kabla ya msimu huu kuanza kulikuwa na maswali mengi juu ya Liverpool. Maswali hayo ni Daniel Sturridge atakuwa fiti? Roberto Firmino ataweza kufunga mabao ya kutosha kuonyesha kwamba alistahili kununuliwa kwa dau la pauni milioni 29? Pauni milioni 34 halikuwa dau kubwa kwa Sadio Mane?

Kazi nzuri ya Jurgen Klopp na kikosi chake cha Liverpool imejibu maswali yote. Wote Firmino na Mane tayari wana mabao matatu kila mmoja, huku Philippe Coutinho akionyesha kiwango. Wameweza kubadilika na kushirikiana kila mmoja na kuonekana kuwa tishio.

Kutokana na uwezo wa Mane, Firmino na Coutinho, imemfanya Sturridge akae benchi.

Mabao:

Philippe Coutinho 3

Sadio Mane 3

Roberto Firmino 3

Daniel Sturridge 0

MAN UNITED

Washambuliaji: Marcus Rashford/Zlatan Ibrahimovic/ Jesse Lingard

Benchi: Anthony Martial

Hapa kuna mchanganyiko wa vijana na wachezaji wenye uzoefu. Baada ya kuwasili kwa kocha Jose Mourinho, alimuweka benchi Marcus Rashford, lakini ameshindwa kuendelea kumwacha benchi nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 kutokana na uwezo wake na kuamua kumwanzisha kikosi cha kwanza.

Tofauti ni kwamba, Zlatan Ibrahimovic, ndiye mchezaji pekee ambaye Mourinho hawezi kumweka benchi, lakini bahati nzuri mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 hajampa kocha huyo nafasi ya kufanya hivyo kutokana na kufanya vizuri, akifanikiwa kufunga mabao manne kwenye msimu huu Ligi Kuu England.

Upande mwingine ameibuka Jesse Lingard na kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Man United, lakini anapaswa kufunga mabao ili aendelee kupata nafasi yake. Lakini hadi sasa ameonyesha kiwango cha juu. Mourinho anaweza kumtumia Wayne Rooney au Juan Mata kwenye nafasi hiyo, pia yupo Anthony Martial, ambaye naye anaweza kucheza nafasi hiyo. Mourinho ana wachezaji wengi kuweza kuwatumia kwenye safu ya ushambuliaji.

Mabao:

Zlatan Ibrahimovic 4

Marcus Rashford 3

Anthony Martial 1

Jesse Lingard 0

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -