Wednesday, November 25, 2020

Hawa wataula kufungiwa Real Madrid kusajili

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

 TIMU za Real na Atletico Madrid  wiki iliyopita zilianza rasmi kutumikia adhabu yake ya kufungiwa kwa muda wa miaka miwili kutofanya usajili iliyopewa na Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA.

Vigogo hao wa soka Hispania wanatumikia adhabu hiyo baada ya UEFA kuvitia hatiani  kwa kukiuka kanuni za usajili za kimataifa kwa kusajili  wachezaji wenye umri mdogo.

Adhabu hiyo inaonekana kuwa ni taarifa mbaya kwa viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ya Los Blancos, kwani haitaweza kuingia sokoni katika kipindi hicho ili kuboresha kikosi chake.

Hata hivyo, pamoja na habari hizo kuwa mbaya kwa baadhi ya viongozi na mashabiki, lakini zinaweza zikawa si mbaya kwa wengine.

Ifutayo ni orodha ya  watu sita ambao huenda wakanufaika na klabu hiyo kufungiwa.

  1. Casemiro

Mbrazil huyo aling’ara msimu uliopita kabla ya kuja Zidane.

Staa huyo alionesha makali yake baada ya kocha Rafa Benitez kumpanga Casemiro  wakati wa Derby ya Madrid dhidi ya Atletico na kutokana na hivi karibuni kuonekana kurejea katika ubora wake anaweza kuwa tegemeo katika kikosi hicho cha  the Rojiblancos.

Katika mchezo huo, Casemiro alionekana kuwa mwiba kwa vinaja hao wa kocha Diego Simeone kutokana na kuwa alikuwa akiwasumbua mara kwa mara. Uimara wa Mbrazil huyo aliouonesha hivi karibuni unatajwa kuwa utamuongezea thamani na kwa sasa anaonekna kuwa katika mipango ya Zidane.
 

Kutokana na hilo, kwa sasa suala la kufungiwa Real Madrid linaonekana kutokuwa kichwani mwa Casemiro, kutokana na  kuwa hakuna majina makubwa ya wachezaji wapya ambao watakuja kutishia kibarua chake hadi Llorente atakapokuwa amerejea kutoka anakokipiga kwa mkopo majira ya joto yajayo.

  1. Zinedine Zidane

Mfaransa huyo kwa sasa anaonekana kutofungika kirahisi na pamoja  hata isingefungiwa, Real Madrid inaonekana ingeendelea kuwa imara kama alivyo  Zidane.

Misimamo ya  nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa unaonekana ndio utakaomfanya Rais wa Klabu hiyo, Florentino Perez,  asimwingilie katika mipango yake kutokana na kuwa atalazimika kuwatumia wachezaji alionao badala ya kusumbuliwa kichwa akasajili wengine.

  1. Marcos Llorente

Kiungo huyo mwenye umri mdogo kwa sasa anakipiga  kwa mkopo katika timu ya Alaves, baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid.

Kabla ya kupelekwa kucheza kwa mkopo, Llorente alikuwa akionekana kama majira haya ya joto angeweza kucheza kwenye kikosi cha kwanza baada ya  mwishoni mwa msimu uliopita kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho cha  Castilla na mwanzoni mwa msimu huu akang’ara wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya  PSG na  Inter.

Llorente ni mchezaji  mwenye kipaji cha kutosha ambacho kingeweza kumfanya abaki  Real Madrid na alistahili kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini kocha wake,  Zinedine Zidane akaamua kumpeleka katika timu hiyo yenye uzoefu mdogo katika michuano ya La Liga  ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Uamuzi huo unaonekana kuanza kuzaa matunda kutokana na kwamba Llorente ameshakuwa shujaa wa mechi zake mbili za kwanza na huku akitoa mchango mkubwa wakati wa mtanange ambao waliibuka na ushindi bila kutarajiwa dhidi ya Barcelona.

Inaelezwa kwamba endapo staa huyo mwenye umri wa miaka  21 msimu ujao atarejea kwenye kikosi hicho cha  Bernabeu, kuna kitu ambacho atanufaika nacho.

Hii ni kutokana na kwamba Zidane hataweza kutumia misimu mitatu mfululizo akimtegemea kiungo mkabaji mmoja  na pia Llorente  tayari atakuwa ameshakuwa na uzoefu wa kutosha katika michuano ya  La Liga  na pia atakuwa tayari kupangwa.

Kwa sasa kuna tetesi zinazodaia kuwa huenda akarejeshwa kikosini mapema Januari, mwakani.

  1. Marco Asensio

Asensio anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao watanuifaka na kifungo hicho cha miaka miwili ambayo wamepewa Real Madrid.

Hii ni kutokana naye pia hana wasiwasi wa kuja mchezaji mwingine mpya mwenye uwezo wa kupiga pasi na kufunga mabao kumzidi nyota huyo mwenye umri wa miaka 20.

Mbali na hilo, staa huyo anaonekana kuumudu vyema mfumo wa 4-3-3 ambao unamfanya aweze kufunga mabao matamu kama alivyofanya wakati wa  mechi dhidi ya  Sevilla katika michuano ya Kombe la Hispania na kisha akafanya hivyo wakati wa mtanange dhidi ya  Real Sociedad.

Kung’ara kwa Isco  na  James Rodriguez ndicho kilichosababisha ishuhudiwe Asensio msimu uliopita akipelekwa kukipiga kwa mkopo kwenye klabu ya  Espanyol, lakini kwa sasa anakuwa kwenye benchi pindi  Cristiano Ronaldo ama  Gareth Bale wasipopangwa.

Tangu alipoondoka Raul ni kwamba kikosi hicho cha Bernabeu kinadaiwa kuwa hakijawahi kupata mchezaji kama huyo, lakini kutokana na kipaji alichonacho Asensio huenda ndiye anayeweza kuwa mbadala wa nyota huyo.

Inaelezwa kwamba wachezaji kutoka Castilla wamekuwa wakikuzwa na kuondoka bila kupangwa katika kikosi cha kwanza kutokana na utaratibu uliowekwa na klabu, lakini  kutokana na uwezo wake Asensio amekuwa akipangwa katika nafasi zenye upinzani mkali ambapo amekuwa akishindania namba na wachezaji kama vile  Lucas Vasquez, James  na  Isco, lakini baada ya kufungiwa ili wasiongeze wachezaji wengine pengine inaweza kumuondolea mawazo kuhusu nafasi yake.

  1. Pepe

Ilikuwa ikitarajiwa kuwa nafasi ya  Pepe katika timu hiyo itakuwa inaelekea ukingoni, baada ya Raphael Varane kuanza kung’ara.

Lakini inavyoonekana jambo hilo kwa sasa halipo, kwani  Zidane atakapoamua kumweka benchi kwa muda mrefu inaweza kula wake.

Wengi walikuwa wakitarajia kuwa pengine kufungiwa kwa klabu hiyo kungekuwa na faida kubwa kwa Varane, lakini  ukweli ni kwamba katika sakata hilo anayeonekana atanufaika zaidi ni Pepe, kutokana na kwamba licha ya umri wake na mkataba wake ambao unakwenda hasi mwakani, vinatosha kumfanya kuwa mchezaji tegemeo katika kikosi hicho hadi  Real Madrid itakaposajili mchezaji mwingine.

Mbali na hilo, kwa sasa klabu hiyo haitakuwa na beki mwingine wa kati mzoefu zaidi ya kuwaita  makinda wake  Diego Llorente  na  Jesus Vallejo, ambao wanakipiga kwa mkopo nje ya klabu hiyo na hivyo kumfanya Varane ashindwe kutamba.

  1. Mariano

Mariano, huyo ni straika chaguo la tatu katika kikosi cha Real Madrid ambaye hajawahi kuwika tofauti na Borja Mayoral, ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo katika klabu ya Wolfsburg.

Hata hivyo, pamoja na kutowika, Mariano ameendelea kubaki katika klabu hiyo na anavyoonekana yupo tayari kubeba majukumu katika kipindi hiki ambacho klabu imefungiwa.

Hali hiyo imejitokeza kipindi cha wiki chache zilizopita ambapo ilikuwa ikisemekana Mariano angepelekwa kwenye klabu nyingine ya La Liga ili akakipige kwa mkopo, lakini  Zidane akamtaka ili aweze kusaidiana na Karim Benzema na  Alvaro Morata.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -