Wednesday, November 25, 2020

YALIYOTIKISA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI ILIYOPITA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

LIVERPOOL walitikisa Ligi Kuu England wiki iliyopita baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya wababe wa Kaskazini mwa London.

Matokeo hayo yaliwafanya Arsenal kuchomoka katika nafasi nne za juu, hivyo kuweka shakani uhakika wao wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, aliamua kucheza kamari kwa kupanga kikosi chake cha kwanza bila nyota Alexis Sanche, ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi.

Lakini, kutokana na michezo iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, huenda kuna matukio mengi yalikupita.

Aguero ni hatari aisee

Straika huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa kwenye wakati mgumu wa kupata namba tangu kutua kwa Gabriel Jesus.

Hata hivyo, mpaka sasa Aguero ameshapasua nyavu mara 23 na amekuwa nguzo imara ya safu ya ushambuliaji ya Man City tangu kuumia kwa Jesus.

Wanyama ang’ara

Wakati Tottenham walipoibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Everton, Victor Wanyama, raia wa Kenya alikuwa silaha ya ushindi kwa upande wa Spurs.

Tottenham walitumia kiasi cha Pauni milioni 9 pekee kumchukua kutoka Southampton ambako pia alikuwa mchezaji muhimu kikosini.

Akishirikiana na Morgan Schneiderlin, ambaye aliwahi kucheza naye Southampton, Wanyama alikuwa moto wa kuotea mbali kwa viungo wa Everton.

Pogba alipotea wikiendi hii

Mancherster United walitoa Pauni milioni 89 kumnunua Paul Pogba. Wachambuzi wa soka wamedai kuwa, bado Mfaransa huyo hajaonyesha kilele cha ubora aliokuwa nao Juventus.

Jumamosi ya wiki iliyopita, Man United walitoka sare ya bao 1-1 na Bournemouth.  Pogba hakuonekana kuwa msaada kwenye mchezo huo. Alipokuwa na mpira, maamuzi yake yalikuwa mabovu na hakuwa akijitoa.

Ukame wa mabao uliendelea Middlesbrough

Wikiendi iliyopita, Middlesbrough waliendeleza mkosi wao wa kutopasia nyavu baada ya kulambwa mabao 2-0. Mpaka sasa ndiyo klabu inayoongoza kwa kuwa na mabao machache Ligi Kuu England, ikiwa imepasia nyavu mara 19.

Ingawa wana safu nzuri ya ulinzi, lakini idadi ya mabao na pointi ina faida kubwa, hasa kwa kipindi hiki ambacho inakabiliwa na balaa la kushuka daraja.

Rekodi zilizopo ni kwamba, katika misimu minne iliyopita, klabu ambazo zilikuwa na mabao machache kufikia hatua hii zilishuka daraja, hivyo huenda historia ikawashusha daraja Middlesbrough.

Sakho alikuwa dunia  nyingine

Nyota wa zamani wa Liverpool ambaye alionekana si lolote Anfield, ameanza kuwa muhimu kwenye kikosi cha Crystal Palace.

Walinzi wa kati wa muda mrefu kwenye kikosi hicho, Scott Dann na Damien Delaney, wameonekana kupoteza nafasi mbele ya Sakho anayecheza vizuri akiwa na James Tomkins.

Walipoifunga West Brom wikiendi iliyopita, ulikuwa ni mchezo wao wa pili kutoruhusu bao, baada ya ule walioshinda bao 1-0 dhidi ya Middlesbrough.

Llorente aliibeba Swansea

Fernando Llorente alifunga bao lake la 10 katika michezo 11 aliyocheza msimu huu.

Amekuwa mchezaji tofauti tangu makocha Bob Bradley na Francesco Guidolin walipotimuliwa.

Badala ya mabao mawili aliyofunga, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania angepachika ‘hat trick’ lakini shuti lake katika kipindi cha kwanza liligonga mwamba.

Kocha mpya Leicester aliendeleza moto

Mkufunzi aliyechukua nafasi ya Claudio Ranieri kwa muda katika kikosi cha Leicester, Craig Shakespeare, alishinda mechi yake ya –pili mfululizo.

Alianza kwa kuichapa Liverpool mabao 3-1 na mwishoni mwa wiki iliyopita aliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley.

Kama ataendelea kuwashangaza mabosi wa Leicester kwa matokeo mazuri, huenda Shakespeare akakabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -