Sunday, November 1, 2020

HAWA KWA KUCHEKA NA NYAVU ‘BOXING DAY’ USIPIME

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

SIKU ya pili ya Krismasi, maarufu kama ‘Boxing Day’, ni siku ambayo huwa ni ya ya watu kutoa zawadi maalumu ama kwa rafiki yako au ndugu.

 Utamaduni huo umekuwapo tangu miaka mingi iliyopita na utaendelea kuwapo hadi mwisho wa dunia.

 Licha ya kuwa utamaduni wa kupeana zawadi, pia unaonekana kuwa kwenye michezo, hususan soka, ambapo wachezaji huwa wakijitahidi kuzifungia timu zao mabao kama zawadi.

 Katika makala haya, BINGWA itajaribu kuangalia ni wachezaji gani ambao wamewahi kuzipa timu zao zawadi ya mabao katika siku hiyo.

  1. Robbie Fowler (tisa)

Alipachika katika mechi 10, tatu akiwa na Liverpool, manne akiwa na Leeds, ikiwamo ‘hat-trick’ walipoondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bolton miaka 15 iliyopita na mawili akiwa na timu ya Manchester City.

Mbali na hayo, staa huyo aliweza kucheka na nyavu mfululizo katika siku hiyo ya Boxing Day kati ya mwaka 2001 na 2004.

  1. Robbie Keane (nane)

Aliyapachika katika michezo tisa, moja akiwa na Coventry, matano akiwa na Tottenham na huku mawili wakati akiitumikia Liverpool.

  1. Alan Shearer (nane)

Aliyapachuka katika michezo 11 ambapo manne alikuwa akiichezea  Blackburn na manne akiwa na Newcastle.

Katika michezo hiyo bao la kwanza la Shearer la kufunga katika siku hiyo ya Boxing Day ilikuwa ni katika mchezo ambao Blackburn iliondoka na ushindi wa mabao 3-1, kabla ya kutenguka goti ambalo lilimfanya azikose mechi nyingine zilizokuwa zimebaki msimu huo.Robbie Keane

  1. Thierry Henry (saba)

Aliyapachika katika mechi saba na yote akiwa na Arsenal

Katika idadi hiyo kuna ‘hat-trick’ moja aliyoifunga dhidi ya Leicester City wakati walipoondoka na ushindi wa mabao 6-1 mwaka 2000.

  1. Jermain Defoe (sita)

Yote aliyafunga katika mechi 10 na moja alikuwa akiichezea West Ham, matano akiwa na Tottenham.

Idadi ya mabao mengi aliyoyafunga straika huyo Desemba 26 alikuwa na  Tottenham walipoondoka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa mwaka 2012 na pengine Jumatatu huenda akaongeza idadi nyingine wakati Sunderland watakapokuwa wakivaa Manchester United katika michuano ya Ligi Kuu England.

  1. Frank Lampard (matano)

Yote aliyafunga katika michezo 17 ambapo mawili alikuwa na timu ya West Ham na matatu akiwa na Chelsea.

Katika historia hiyo Lampard anaonekana kuwa na nyota ya kufunga katika siku hiyo ambapo katika kipindi cha kuanzia 1999  hadi 2001 aliweza kufunga mabao mfululizo ambapo mara mbili alikuwa na  West Ham. Bao alilolifunga mwaka  2001 alikuwa kwenye Uwanja wa  Highbury  dhidi ya  Arsenal na mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kuchapwa  2-1.

  1. Steven Gerrard (matano)

Aliyafunga katika michezo 14 na yote akiwa na Liverpool.

Si jambo la kushangaza kumshuhudia  Stevie G akiingia kwenye orodha hii ya wachezaji wenye  bahati ya kufunga mabao katika siku hiyo.

Katika historia hiyo, kiungo huyo alifunga mabao manne katika miaka mitano kati ya mwaka 2004 na 2009 na kisha akafanya hivyo mwaka 2012  dhidi ya Stoke, ambapo Liverpool ilicheza Desemba 27 mwaka huo.

  1. Andy Cole (matano)

Yote aliyafunga katika michezo tisa ambapo matatu alikuwa na timu ya Manchester United, moja akiwa na  Blackburn na Manchester City.

9.Dimitar Berbatov (matano)

Aliyafunga katika michezo sita ambapo manne alikuwa akiichezea  Manchester United na moja akiwa na Fulham.

Katika idadi hiyo imo ‘hat-trick’ moja aliyofunga wakati wa mchezo wa  Manchester United  dhidi ya  Wigan, ambao waliondoka na ushindi wa mabao 5-0 miaka mitano iliyopita.

Nyota wengine ambao waliwahi kucheka na nyavu katika siku hiyo ni Gareth Barry (5) akiwa na timu za  Aston Villa  na Manchester City, Ryan Giggs (4)akiwa na Man  United, Wayne Rooney (4) naye akiwa na  Man  United, Duncan Ferguson (4) akiwa na timu za  Everton, Newcastle, Michael Owen (4) akiwa na Liverpool na Trevor Sinclair​ (4) wakati akiichezea West Ham.

Wengine ni Louis Saha (4) wakati akizichezea timu za Fulham na Man  United, Niall Quinn (4) akiwa na Manchester City, Sunderland, Jason Euell (4) akiwa na timu za Wimbledon na  Charlton, Steffen Iversen (4) akiwa na Tottenham, Carlton Cole (4) akiwa na West Ham na  Juninho (4) aliyofunga akiwa na  Middlesbrough.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -