Tuesday, October 20, 2020

Hii ni moja ya kanuni ya kukupa mpenzi wa kukupa furaha

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

WAPO waliokutana katika daladala na baada ya siku chache wakafunga ndoa na leo wanaishi katika maisha ya amani na furaha. Wengine walionana ufukweni na ndani ya wiki kadhaa wakaingia katika ndoa inayowafanya wafurahi na kuwa na amani karibu muda wote. Hayo yanawezekana kutokea.

Unaweza kukutana katika siku chache na mwenzako na kisha baada ya muda kidogo mkaingia katika uhusiano. Inawezekana. Ila ni moja kati ya kumi!

Wengi waliokutana katika namna hiyo na kuharakisha kuingia katika uhusiano ni wenye kujuta na kulaumu maamuzi yao. Mapenzi ni suala pana sana. Si suala linalohitaji papara au uamuzi wa jazba. Kuna misingi na kanuni fulani unabidi kufuata ili uweze kufikia katika uhusiano wa amani, raha na thamani.

Ndiyo, mapenzi ni hisia zinazokuja zenyewe bila kulazimishwa wala kushurutishwa na mtu. Ni hisia zisizochagua mahala pakuonekana wala kujionesha. Si sahihi kusema eti mpenzi wa kweli nitampata chuoni au kazini, hapana.

Wengi walikutana huko wakaambulia maumivu na madhila. Na wengi walikutana huko wakajikuta wanaingia katika ukurasa wa furaha na amani ya maisha yao. Hakuna eneo wala nchi ya kupata mpenzi wa kweli. Si shuleni, hospitali wala baa. Kila sehemu ina nafasi yake ya kukupa furaha katika maisha yako na karaha katika maisha yako kupitia mapenzi. Suala ni umakini na kufuata misingi bora ya uanzishaji wa uhusiano.

Kuna watu nawajua walikutana sehemu za starehe, sehemu ambazo kwa wengi huamini kuwa si salama kwa kukutania na watu wa maana. Ila baada ya muda fulani wakaingia katika uhusiano na leo ni miaka kadhaa kuna amani na furaha katika ndoa zao.

Kuna mwanamuziki anaitwa Benjamini wa Kundi la Mambo Jambo, alikutana na mpenzi wake katika maandalizi ya video ya wimbo wake. Alisema kuwa alikuwa akitafuta wanawake kwa ajili ya kucheza ndani ya ile video. Alitafuta wasichana wengi ila mmoja wapo alikuwa huyu ambaye leo anamwita mke.

Japo msichana yule hakuwa tayari kwa ajili ya video ile ila baada ya hapo waliwasiliana na matokeo yake imezaliwa ndoa ya furaha na amani kwa mujibu wa maelezo yake. Suala ninalotaka ulielewe hapa ni kuwa hisia hazina mahala wala muda wa kuonekana. Suala ni umakini na kushusha hali ya haraka katika uanzishaji wa uhusiano wako.

Ndiyo, umekutana na mtu unayeamini unampenda katika daladala ila je, unafuata hatua gani katika kuingia naye ndani ya uhusiano? Wengi watachukua namba ya simu leo saa sita mchana, kesho kutwa saa kumi jioni atatongoza. Hapa ndipo wengi tunapoumia na kila siku kulia katika uhusiano.

Anzisha naye urafiki wa karibu usiohusisha mambo ya mapenzi. Tena kuwa mjanja wa kutoonesha kwa pupa hisia zako juu yake ili upate muda wa kumsoma kwa umakini na kumjua jinsi alivyo.

Usiwe na papara, unaweza kuwa naye katika hali hii hata kwa zaidi ya miezi mitatu au minne. Suala si mapenzi ya kweli? Sasa haraka ya nini? Vijana wengi huwa na pupa ya ngono na matokeo yake wanawahi kutaka kuanzisha uhusiano haraka na kujikuta wakiingia katika majuto na maumivu yasiyokuwa na mfano.

Kuwa makini na kauli na matendo yako katika hali hii. Jitahidi kuwa na ule urafiki utakaokufanya umjue yeye vizuri, marafiki pamoja na nasaba yake. Hili litakusaidia kumjua vizuri zaidi na kujua yeye hasa ni mtu wa aina gani.

Tunapozungumza kuwa inabidi ujuane na mtu unayetaka kuanzisha naye uhusiano, haina maana ujue jina lake tu na upate namba yake ya simu. Hapana!

Inabidi umjue hasa yeye nani, ana mipango gani na mtu wa aina gani. Ujue tabia yake halisi na hili linawezekana tu kama utamfanya awe rafiki yako huku ile dhamira yako ya kutaka kuanzisha naye uhusiano ukiificha katika hali fulani, ili asiweze kuijua na matokeo yake akawa anaonesha tabia za kuigiza.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -