Friday, October 23, 2020

HII SASA FUJO! WACHINA WAMTAKA NA RONALDO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MADRID, Hispania
HII sasa fujo pale unapozungumzia harakati za usajili ambazo zinafanywa na klabu za Ligi Kuu ya China maarufu kama Chines Super League.

Msemo huo unakuja baada ya wakala wa straika Cristiano Ronaldo, Jorge Mendez, kusema mteja wake ameahidiwa ofa ya Euro milioni 100 kwa mwaka ili aweze kucheza katika ligi kuu ya soka nchini humo.

Hivi karibuni mshambuliaji wa zamani wa Argentina, Carlos Tevez, alikamilisha usajili wake katika klabu ya Shanghai Shenua na kuwa mchezaji anayelipwa vizuri kuliko wachezaji wote wa soka duniani na iwapo usajili wa Ronaldo utakamilika atalipwa mara mbili zaidi ya Tevez.

Aidha, si malipo yake yatazidi yale ya Tevez, lakini atamshinda mara tatu zaidi mchezaji aliyeweka rekodi ya usajili duniani, Paul Pogba, aliyesajiliwa kwa ada ya pauni milioni 100 na klabu ya Manchester United katika majira ya joto.
Wakala wa Ronaldo, Mendes, amesema pamoja na ofa hiyo bado mteja wake ataendelea kuheshimu mkataba wake na `Los Blancos`.

“Kutoka China wametoa ofa ya Euro milioni 300 kwa Real Madrid na zaidi ya Euro milioni 100 kwa mwaka kwa Ronaldo.” Lakini fedha si kila kitu, klabu hiyo ya Hispania ndio maisha yake,” Mendes aliuambia mtandao wa Sky Sports Italia.

Umaarufu wa wakala Mendes utaongezeka iwapo atafanikisha mpango huo, baada ya hivi karibuni wakala mwingine maarufu Mino Raiola kutawala soko la usajili msimu wa kiangazi.

Wateja watatu wa Raiola Pogba, Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic walijiunga na mashetani wekundu baada ya Jose Mourinho kukalia kiti cha moto Old Trafford.

Hivi karibuni uwekezaji katika soka nchini China umewashangaza wadau na wapenzi wa soka duniani kwa jinsi wanavyotumia fedha kufanikisha azma yao ya kutangaza ligi yao `Chinese Super League`.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -