Sunday, January 17, 2021

HII VITA YA ‘TOP FOUR’ ATAKAYEZUBAA SHAURI YAKE

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

HUENDA ikawa ni mapema sana kusema kwamba nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England imepata ‘mkazi wa kudumu’.

Bado ligi haijafikia mwisho. Hadi kufikia mwezi huu wa Februari, ligi itachezeka hadi Mei mwaka huu mpaka bingwa mpya wa ligi hiyo atakapotangazwa na Chelsea ndiye kinara akiongoza kwa tofauti ya pointi tisa, kutokana na ushindi wake wa michezo 19 kati ya 24.

Ni ngumu kuitengeneza picha kwamba wataangushwa kutoka kwenye kilele cha msimamo.

Kama taswira ya Chelsea kuanguka kutoka kileleni ikiwa haiwezekani kuundwa, je, kuna nini kilichobakia?

Vita ya timu tano zinazowania nafasi tatu kati ya nne za juu kwenye msimamo huo, nafasi ambazo zitawapa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Miamba hiyo mitano imepishana pointi chache mno, ambapo ukipiga hesabu ya pengo la pointi baina ya Spurs aliye nafasi ya pili na Man United aliye nafasi ya sita ni pointi tano tu.

Katikati yao kuna Man City ambao bado wanazoeshwa aina ya soka la Pep Guardiola, kuna Arsenal walioteleza hivi karibuni na Liverpool ambao wameporomoka mno licha ya kuanza msimu huu kwa kiwango cha hali ya juu.

Mtandao wa Daily Mail umechambua kwa upana jinsi kila timu itakavyoweza kutinga ‘top four’ na hasara zitakazopatikana kwa kuikosa nafasi hiyo muhimu.

 

SPURS

Spurs hawajafungwa michezo tisa ya Ligi Kuu England (ukiwamo ushindi dhidi ya Chelsea) na wikiendi hii watachuana na Liverpool kwenye dimba la Anfield.

Kwa kuzingatia viwango vya timu hizo, mechi hii huenda ikawaharibia vijana wa Mauricio Pochettino, kwani watakuwa nje ya dimba lao la nyumbani.

Lakini, jaribio gumu zaidi ni pale atakapotakiwa kuweka uwiano mzuri wa kikosi chake kwenye mechi za Ligi ya Europa, FA (kama ataendelea kuwapo). Na alishaonesha uwezo huo hapo kabla.

Kama Spurs itashindwa kuingia kwenye nafasi nne za juu, haitahesabika kama ni hasara kwani ana vijana wadogo na hakutumia fedha nyingi kusajili.

Lakini uwezo wa kutinga ‘top four’ wanao, labda majeruhi yawaharibie.

Utabiri: Wataingia

 

MAN CITY

Pep Guardiola alikaribishwa EPL na presha ya hali ya juu, lakini katika siku za hivi karibuni zimeonekana dalili za utulivu ndani ya kikosi chake.

Hakuna atakayemwelewa kocha huyo kama City itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, kwani walitabiriwa hata kuwa ndio vinara wa ligi kuu kwa jinsi walivyosajili wachezaji wa gharama za juu.

Lakini bado wanayo nafasi kubwa ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao kwa jinsi kikosi chao kilivyoanza kutulia na kucheza soka la kueleweka.

Utabiri: Wataingia

 

ARSENAL

Heshima anayoipata kocha Arsene Wenger ndani ya klabu ya Arsenal kwa miaka 10 ya hivi karibuni, ni kumaliza msimu bila kukosa nafasi kwenye ‘top four’.

Uwezo wa kumaliza msimu huu ndani ya nafasi nne za juu wanao lakini Januari hii imegeuka kuwa nuksi kwao. Mashabiki wameanza tena kupiga kelele za kumwona Wenger akiondoka huku hatima ya mastaa wa timu hiyo, Alexis Sanchez na Mesut Ozil ikiwa haijulikani.

Ile furaha ndani ya klabu imeondoka haraka sana.

Je, maumivu ya kukosa nafasi ndani ya ‘top four’ yatakuwa makubwa kivipi? Na nini kitawatokea Sanchez na Ozil kama Arsenal isipocheza ligi ya mabingwa msimu ujao?

Utabiri: Hawataingia

 

LIVERPOOL

Vijana hawa wa kocha Jurgen Klopp wameuanza mwaka 2017 kwa kiwango cha chini mno.

Januari 4 mwaka huu, walikuwa nyuma ya Chelsea kwa tofauti ya pointi tano. Lakini kwa sasa wameachwa na vinara hao kwa tofauti ya pointi 13, wakiporomoka kutoka nafasi ya pili hadi ya tano na kuna dalili za wao kutonyakua ubingwa wa ligi kwa mara nyingine.

Unadhani watafurahi kuikosa nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao? Hapana, kwa sababu wao ndio wapinzani pekee waliokuwa wakitishia nafasi ya Chelsea kileleni kwa muda mrefu.

Liverpool hawatakuwa na furaha kama wataikosa nafasi hiyo kwani hakuna mchezaji mkubwa atakayekubali kutua kwenye timu isiyocheza ligi ya mabingwa msimu ujao.

Lakini, kwa kuzingatia kiwango cha hali ya juu walichokionesha kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi, huku wakiwa hawana mechi yoyote ya kuwania makombe mengine tofauti na ligi, Liverpool watabakiwa na vita moja tu nayo ni kusaka tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Utabiri: Wataingia

 

MAN UNITED

United ikiwa chini ya kocha Jose Mourinho, ilianza vizuri msimu huu lakini ilijikuta inaporomoka, kabla ya kurudi kwenye kiwango chao tena wakiwa hawajapoteza michezo 14 ya Ligi Kuu England.

Hata hivyo, licha ya kutopoteza michezo yote hiyo, United bado haijaweza kurudi kwenye nafasi nne za juu na kama watashindwa kutinga kwenye ligi hiyo ‘watachota’ hasara ya pauni milioni 85 kutoka kwa wadhamini.

Presha itamvaa Mourinho msimu ujao, kwani kila mtu atataka kuiona United ikifanya makubwa ili kulipa hasara ya kusajili kwa ‘sifa’ msimu huu.

Kwa sasa tusubiri kuona kama mechi zilizosalia zitawapandisha juu.

Utabiri: Hawatoingia

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -