Friday, October 30, 2020

HIKI NDICHO KILICHOWAMALIZA SPURS DHIDI YA LIVERPOOL

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MERSEYSIDE, Liverpool

KLABU ya Liverpool imerudisha matumaini yao ya kumaliza ligi katika nafasi nne za juu, shukrani kwa mabao mawili ya Sadio Mane yaliyoizamisha Tottenham Hotspurs mwishoni mwa wikiendi iliyopita.

Winga huyo alitumia vyema uzembe wa mabeki wa Spurs na kufunga mabao mawili ya haraka ndani ya dakika mbili na kukifanya kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Lakini, ilikuwa ni siku mbaya kwa kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino, ambao hawakuwa tishio kwenye lango la wapinzani wao hao, huku bundi wa kukosa matokeo kwenye dimba la Anfield akiendelea kuwaandama.

Tangu mchezo huo ulivyoanza, Liverpool ilifanikiwa kumiliki sana mpira huku Mane akiwa ndio mhimili mkuu na si ajabu kuiona Liverpool ikirudi kwenye mwenendo wa ushindi, baada ya ujio wake kutoka kwenye Fainali za Mataifa Afrika (Afcon 2017).

Sababu kubwa ya Liverpool kuuanza mwaka vibaya ilikuwa ni kukosekana kwa Mane ambaye ni mmoja wa washambuliaji hatari waliopo kwenye kikosi hicho.

Mabao yake mawili ya juzi yalimfanya afikishe jumla ya mabao 11 ya ligi kuu na hadi sasa hakuna mchezaji wa Liverpool aliyehusika kwenye mabao mengi ya klabu hiyo msimu huu zaidi yake.

Na iwapo ataendelea kuwa fiti uwanjani, Liverpool itamtegemea mno mshambuliaji huyu kwenye mpango wao wa kumaliza ndani ya ‘top four’ msimu huu.

Wakati Mane akirudi kwa kasi hiyo, Spurs walionekana kuandamwa na nuksi ya kutopata matokeo ndani ya dimba la Anfield. Ni nuksi iliyowaganda kwa muda mrefu.

Kila mtu alisubiri kuona wakifuta uteja wa kutoondoka na pointi za kutosha pale, lakini kichapo hicho cha bao 2-0 kiliwafanya wafikishe mechi 23 bila ushindi, ingawa waliwahi kushinda mechi moja tu kwa mabao 2-0 mwaka 2011.

Na katika mechi hizo 23, Liverpool iliitandika Spurs mara 15 na sare saba.

Achana na hilo la kutoshinda michezo mingi namna hiyo pale Anfield, hebu tujiulize swali hili; Spurs wana nguvu kweli ya kuitisha Chelsea au hata kuhimili presha ya mbio za ubingwa msimu huu?

Rekodi yao dhidi ya timu tano kubwa za juu hairidhishi, hasa wakiwa ugenini. Ni jambo la kufikirisha mno hilo, wana wachezaji wazuri lakini akili yao imekomaa kuwa mpinzani wa Chelsea?

Spurs imeshasafiri kwenda kwenye viwanja vya timu hizi, Man City, Arsenal, Chelsea, Man United na Liverpool. Kote huko haijapata ushindi.

Hebu wachukue vinara wa ligi, Chelsea, hawa walichukua pointi tatu kwa Man City na pointi moja ya muhimu mno kutoka kwa Liverpool. Je, Spurs inatushawishi vipi kama inaweza kuwania ubingwa?

Zaidi ya hilo, Spurs iliangushwa na mabeki wao wenyewe.

Jan Verthonghen na Danny Rose ambao ni mabeki imara wa Spurs kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, hawakuwapo na hilo liliwapa nafasi Liverpool kuisumbua mno Spurs, wakifunga mabao mawili dakika ya 16 na 18!

Ben Davies alichukua nafasi ya Rose upande wa kushoto lakini beki huyo alikutana na zahama ya Mane iliyompa presha kwenye dakika za awali za mchezo huo.

Eric Dier ambaye alianzishwa kwenye nafasi ya Vertonghen, hakuwa makini na bao la pili la Mane lilisababishwa na uzembe wake wa kutafuta sana mpira kuliko kulinda na Mane akawaadhibu tena.

Na kama asingekuwapo mlinda mlango Hugo Lloris, Spurs ingejikuta ikioga mvua ya mabao katika kipindi cha kwanza tu cha mchezo huo kutokana na nafasi kubwa walizowaachia Liverpool kucheza mipira ya hatari.

Liverpool ya Klopp ni ngumu kufungika pindi inapoachiwa mno nafasi za kucheza mpira na kama timu yako ikiwa na masikhara mengi kuliko umakini mchezoni, kufungwa ni lazima.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -