Saturday, October 31, 2020

HIKI NDICHO KINACHOENDELEA VITA YA PAYET, WEST HAM

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

HIVI sasa Dimitri Payet ameimarishiwa ulinzi na uongozi wa klabu yake ya West Ham na hiyo ni baada ya mashabiki wake kumfanyia fujo siku kadhaa zilizopita.

Imeripotiwa kuwa uongozi wa West Ham umefikia uamuzi wa kusimamia usalama wa mchezaji wao huyo kwa saa 24, lengo likiwa ni kumnusuru na vurugu za wahuni wanaotajwa kuwa ni mashabiki wa West Ham.

Wiki iliyopita mashabiki ambao hawakufurahishwa na kitendo cha Payet kung’ang’ania kuondoka klabuni hapo, walivamia nyumbani kwa nyota huyo.

Payet mwenye umri wa miaka 29, amegoma kuichezea timu hiyo kwani anataka kuona ikimruhusu kujiunga na klabu yake ya zamani ya Marseille.

Payet haelewani na wachezaji wenzake na hata kocha Slaven Bilic ameshamwondoa kwenye kikosi chake kitakachokwenda jijini Dubai kwa maandalizi ya majira ya baridi.

Marseille wameshapeleka ofa tatu za kumhitaji mkali huyo lakini West Ham wamekuwa wakikataa kumwachia.

Klabu hiyo ya Ufaransa inamtaka Payet na tayari mabosi hao wako tayari kutumia pauni milioni 30 kumchukua.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -