Friday, December 4, 2020

HIKI NDICHO KINACHOMFANYA IBRAHIMOVIC AZIDI KUNG’ARA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

UWEZO alionao straika wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, bado unawashangaza wengi, licha ya kuwa na umri mkubwa.

Uwezo wa nyota huyo umekuwa ukiongezeka zaidi kadri umri wa nyota huyo unavyozidi kwenda na bao alilofunga  siku ya `Boxing Day` dhidi ya  Sunderland lilikuwa la 12 kwa mshambuliaji huyo katika Ligi ya England na bao la 17 katika mashindano yote ambayo klabu yake imeshiriki, na hivyo kuiwezesha United kukusanya pointi 10 kutokana na mabao yake aliyoyafunga msimu huu.

Kucheza mechi 17 za Ligi akiwa katika kikosi cha kwanza msimu huu  kutokana na umri wake, ni jambo lililomfanya kocha wake, Jose Mourinho, aseme kuwa mchezaji huyo, `amekamilika`.

 

 *Siri yake ni hii  hapa

Uwezo huo anaoendelea kuonyesha Ibrahimovic ni kutokana na mazoezi ya kiwango cha juu anayoyafanya, yakijumuisha mazoezi ya karate, kutotumia pombe na kusikiliza muziki wa reggae.

Uwezo wa kimwili na mazoezi ndiyo sababu iliyomfanya kocha wake, Mourinho, kumpa siku zaidi mshambuliaji huyo wakati wa mechi za kimataifa.

Kutokana na hali hiyo, uwezekano wa kuongezewa mwaka mmoja katika mkataba wake kuendelea kubaki Old Trafford msimu ujao ni mkubwa.

Viongozi katika klabu ya mazoezi ya Carrington walipigwa na butwaa baada ya Ibrahimovic kuvunja rekodi za wachezaji wengine ndani ya United kwa uwezo wake wa kufanya mazoezi mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Imegundulika kuwa, nyota huyo wa Sweden anafanya mazoezi ya ziada na mwalimu wake binafsi wa viungo, Dario Fort, ambaye alihama naye kutoka Paris Saint-Germain, baada ya kufahamiana naye akiwa anaichezea klabu ya AC Milan.

Katika mkataba wake na Manchester United kama  ilivyokuwa PSG , Ibrahimovic  amekuwa akisisitiza kuwa anahitaji daktari au mwalimu wa viungo na sasa ameruhusiwa kuendelea kuwa naye na analipwa na Man United, lakini si miongoni mwa wasaidizi wa  Mourinho na wala hakai katika benchi la klabu hiyo.

Katika idara ya viungo wanaotambulika na Mourhino, ni Daktari Steve McNally na mwalimu wa viungo Neil Hough wanaoshughulika na wachezaji majeruhi ndani na nje ya uwanja, lakini ni Fort ambaye anamsimamia Ibrahimovic pekee.

Mwalimu huyu wa viungo ndiye aliyemsaidia Ibrahimovic wakati akijiandaa kukabiliana na soka ya England baada ya kusajiliwa na `mashetani wekundu`. Mtaalamu huyo anasimamia mazoezi yake ya ziada na husisitiza straika huyo kusikiliza muziki wa reggae ili kutuliza akili yake wakati wa mazoezi.

Mazoezi yake yamemsaidia kuwa katika soka kwa muda wa miaka 20, akiwa amecheza mechi 750 na amekuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji kinda wa Manchester United.

“Hakika kwa kila namna ameonyesha weledi”. “Hata katika jambo ambalo ni gumu kwa sasa kwa kila mtu, ameweza kumudu kutunza siri ya familia yake na inayoishi kwa furaha,” Mourinho alisema wiki iliyopita.

“Ameweza kujitunza katika maisha yake nje ya soka. Ni mfano wa kuigwa katika kila jambo, na ukiwa naye na Michael Carrick aliye na umri wa miaka 35, wachezaji kinda hawatapa mfano mzuri wa kuigwa kutoka kwa wachezaji hao,” alisema Mourinho.

Ibrahimovic si mchezaji wa kutoka usiku kwenda kustarehe kama walivyo mastaa wengine na anasema amekunywa pombe mara chache sana.

Katika mazungumzo yake, Ibrahimovic anasema aliwahi kuzidisha kinywaji mara moja na kupoteza fahamu akiwa maliwatoni baada ya kutwaa taji la Scudetto kwa mara ya kwanza akiwa na Juventus, na amemtupia lawama mshambuliaji mwenzake wakati huo, David Trezeguet, kuwa ndiye aliyemfanya kudizisha kilaji.

Akizidi kuainisha sifa zake, Mourinho anasema: “Nilijua kuwa kutokana na mapenzi yake katika soka, uwezo wake, angefaa kuwepo hapo alipo. Nilimwambia England si sehemu nzuri ya kustarehe, kama mtu tajiri na mwenye kipaji akitaka kustarehe hatakiwi kuja England. Njoo England iwapo unataka kucheza katika Ligi ngumu kuliko zote duniani, ili uonyeshe uwezo wako.

‘Kwa mantiki hiyo, kuja kwake kulitokana na maelezo hayo, na si kufunga mabao pekee. Bali ni kuonyesha uwezo wake kiuongozi na  kuhamasisha, na hakika nina furaha.”

Hivi karibuni Michael Owen alisema kuwa, Ibrahimovic  ni mchezaji aliyesajiliwa kwa muda tu na atashindwa kukabiliana na mikiki ya Ligi hiyo na sasa mshambuliaji huyo anathibitisha kuwa kauli ya nyota huyo wa zamani wa Liverpool, Real Madrid, Newcastle, Manchester United na timu ya taifa haikuwa sahihi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -