Sunday, November 29, 2020

Hiki ndicho kinachowafelisha Wahispaniola wa Azam

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

HAKUNA asiyejua kuwa Azam haiko vizuri sana msimu huu na ushahidi wa hili ni mwendo wa kusuasua iliyoanzanao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Katika michezo tisa ambayo Azam imecheza hadi sasa, miamba hiyo ya Chamazi imevuna pointi 12 kutokana na kushinda mechi tatu, kutoka sare tatu na kufungwa tatu, kitu kinachozidi kuwaondoa kwenye mbio za ubingwa kutokana na kasi waliyoanza nayo Simba msimu huu.

Wakati watu wakizidi kujiuliza tatizo nini Azam, BINGWA linakuletea sababu zinazomfelisha kocha Mhispaniola, Zuben Hernandez na benchi lake la ufundi pale Chamazi.

Uzoefu wa soka la Tanzania

Inawezekana Hernandez ni bonge la kocha, lakini tatizo kubwa ambalo linamkabili ni kukosa uzoefu wa soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla, hivyo anajikuta kwenye wakati mgumu kupambana na makocha waliozoea soka hili na aina ya viwanja vya Tanzania.

Na kama kuna kosa kubwa ambalo Azam walilifanya ni kuondoa watu wote wenye uzoefu wa soka la Tanzania kwenye benchi lao la ufundi, lakini kama wangeweza kumuwekea msaidizi mwenye uzoefu wa soka la nchi angeweza kumshauri kwenye baadhi ya mambo, ila bahati mbaya kwenye benchi lake amejaza Wahispaniola wenzake wasiolijua soka la Afrika.

Kuondoka kwa Kipre & Farid

Kati ya wachezaji waliokuwa muhimu kwenye kikosi cha Azam msimu uliopita ni Kipre Tchetche na Farid Mussa, ambao wote hawapo kwenye kikosi cha matajiri hao wa  Chamazi msimu huu.

Kipre katimkia Uarabuni, wakati Farid jina lake halikujumuishwa kikosini kutokana na kutakiwa kwenda Hispania, hivyo kukosekana kwao kwenye timu kumeiathiri safu ya ushambuliaji ya Azam msimu huu na kujikuta wakifeli kufanya makubwa.

Pengo la Wawa

Beki Muivory Coast, Pascal Serge Wawa, alikuwa kiongozi muhimu kwenye ukuta wa Azam msimu uliopita, lakini msimu huu amekosekana muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi na huku pia sakata lake la mkataba mpya likionekana kumvuruga zaidi.

Kukosekana kwake kumesababisha beki ya Azam kuwa dhaifu, licha ya ujio wa Mghana, Daniel Amour na ndiyo maana katika mechi tisa msimu huu Azam imeruhusu mabao nane, kitu ambacho kimewaweka kwenye wakati mgumu kushinda mechi zao.

Wachezaji wa kimataifa

Hili nalo ni tatizo kubwa sana Azam, kwa sababu imeingia msimu huu ikiwa na wachezaji wanne wapya wa kimataifa, ambao kiukweli uwezo wao ni wa kawaida sana na wameshindwa kuthibitisha uhalali wao wa kuchezea timu kubwa kama Azam.

Ukiacha Amour, aliyesajiliwa kutoka Medeama SC ya Ghana, wachezaji wengine wapya wa kimataifa wa Azam kama Wazimbabwe Bruce Kangwa na Francisco Zekumbawira pamoja na Muivory Coast Ya Thomas Gonazo wameshindwa kuthibitisha thamani zao na kuibeba Azam kwenye kipindi hiki muhimu.

Ishu ya posho

Kuna tetesi kuwa ndani ya Azam kuna mgomo baridi kwa wachezaji ambao wanadaiwa kukerwa na kitendo cha kocha mpya wa timu hiyo kufuta baadhi ya posho ambazo walikuwa wakipokea miaka ya nyuma, kitu ambacho kimeathiri vipato vyao.

Awali wachezaji wa Azam walikuwa wakilipwa posho mbalimbali baada ya mechi, ziwe za ugenini au za nyumbani, lakini baada ya ujio wa kocha mpya alifuta posho hizo akidai kuwa wachezaji hawatakiwi kulipwa posho kwa kazi ambayo wanalipwa mshahara.

Inadaiwa kuwa, kutokana na hali hiyo, posho za mechi za ugenini na nyumbani zimefutwa, kitu ambacho kimewakera wachezaji wa timu hiyo na kushusha morali yao uwanjani, matokeo yake kusababisha timu kuwa na mwenendo mbovu.

Kushuka kwa viwango vya wakongwe

Viwango vya wachezaji wakongwe ndani ya Azam kama akina John Bocco, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ na wengine si kama vilivyokuwa misimu miwili mitatu iliyopita, safari hii vinaonekana kutetereka, kitu ambacho kinaathiri kiwango cha klabu uwanjani kwa ujumla.

Mfumo mpya

Azam ya Stewart Hall ilikuwa ikitumia mfumo wa 3-5-2 ambao uliifanya kuwa bora sana uwanjani, lakini baada ya ujio wa Wahispaniola, Azam imerudi kutumia mfumo wa mabeki wanne nyuma, kitu ambacho kinawaathiri wachezaji ambao walizoea mfumo huo wa Hall, ambao ulimfanya mchezaji kama Shomary Kapombe kuwa tegemeo kwenye timu kutokana na mabao yake, huku timu ikiwa na ukuta wa chuma nyuma.

Hitimisho

Kama kuna wakati busara inahitajika Azam ni wakati huu, kwa sababu licha ya kuanza ligi, tayari wameshatumia gharama kubwa kuwaleta Wahispaniola hao Chamazi, hivyo uongozi wa timu hiyo unatakiwa kusimama nyuma ya kocha wao na kumpa nafasi zaidi, huenda akaja kubadilisha mwenendo wa timu.

Kumfukuza Zuben na benchi lake la ufundi kwa sasa kutawaingiza Azam kwenye mtego wa timua timua ambao hauna afya kwa maendeleo ya klabu hii ambayo inatazamwa kama ya mfano kwenye soka la Tanzania, kwa hiyo itakuwa busara kama wakiendelea kuwaamini makocha hao kwa sababu wana kitu ambacho kiliwashawishi wawape kazi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -