Wednesday, October 28, 2020

HILI LA UWANJA WA JAMHURI TFF MLIKUWA WAPI?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

WIKI hii Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza kuufungia Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, ili kupisha fursa kwa wamiliki wake kuufanyia marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea mpira.

Mbali na marekebisho hayo, pia wametaka kupata maelekezo ya kutosha kwa Jeshi la Polisi jinsi linavyosimamia usalama uwanjani, kwani mara nyingi wamekuwa ni sehemu ya mashabiki wanaoangalia mechi.

Shirikisho hilo limeona umuhimu wa kufanya marekebisho na ikishindikana basi mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizopangwa kuchezwa kwenye uwanja huo zitahamishiwa uwanja mwingine.

Tayari uwanja huo umeshatumika katika mchezo namba 151 baina ya wenyeji Mtibwa Sugar na Simba, mechi iliyochezwa hivi karibuni na kumalizika kwa sare ya kutofungana.

TFF imesema baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari walikuwa uwanjani hapo kufuatilia matukio.

Kuna watu najua hawatanielewa, ila hoja nyepesi tu unaweza ukajiuliza hawa viongozi wa TFF na Bodi ya Ligi  walikuwa wapi siku zote mpaka timu zinaingia uwanja ukiwa haufai kwa kuchezea ligi yao.

Hakuna asiyejua kuwa ligi kuu ilisimama kwa kipindi zaidi ya miezi kadhaa hivi TFF na Bodi ya Ligi hawakuona haja ya kukagua viwanja na kuvitathmini ubora wa miundombinu yake?

Muda ulikuwapo wa kutosha wa kuvipitia viwanja vyote na kuvikagua kabla ya mechi hazijaanza, lakini TFF hawakona haja ya kufanya hivyo sasa mechi zimeshaanza ndio wanatoka mafichoni na kufungia uwanja.

Nakumbuka TFF walichokumbuka wakati ligi imesimama ni timu itakayochelewa kufanya usajili wake kupigwa faini kwa kila mchezaji, lakini TFF sikuwasikia kokote wakisema kwamba kwa timu ambayo kiwanja chake cha nyumbani kitakachotumika kwa ajili ya mechi za ligi kama ni kibovu, basi kiwanja hicho kitafungiwa mpaka kitakapofanyiwa ukarabati.

Hakuna asiyefahamu kwamba viwanja vingi vya hapa nchini ni vibovu na havina hadhi ya kutumika kwa ligi kuu, ukiachana na viwanja vya Dar es Salaam pekee.

TFF ilitembea kukagua viwanja katika hatua ya awali, lakini inatakiwa kuvitembelea tena ili kujiridhisha kama kweli vimekidhi haja. Kwani kwa hakika naamini bado viwanja hivyo haviko katika hali nzuri ya kutumika.

Baadhi ya viwanja ambavyo vimetembelewa na ukarabati ulianza kufanyika ni Uwanja wa Mwadui FC ambao unamilikiwa na Mgodi wa Madini wa Mwadui pamoja na Uwanja wa CCM Kambarage.

Ukarabati wake ulikuwa mkubwa kwani hata hali ya vyoo tu ukiachana na uwanja wenyewe wa kuchezea ilikuwa katika hali tete.

Ukiacha viwanja hivyo pia nakumbuka Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mkwakwani Tanga, Majimaji Songea, Jamhuri Morogoro, Nagwanda Sijaona wa Mtwara na vinginevyo vyote vilielekezwa vifanyiwe ukarabati ila sidhani kama hilo lilifanyiwa kazi.

TFF kupitia Kamati ya Mashindano ilipaswa kuchukua hatua mapema  kuvifungia viwanja hivyo kutotumika kwa shughuli zozote za kimichezo mpaka hapo vitakapofanyiwa marekebisho na kama marekebisho hayo hayajakamilika basi hata mechi za ligi kuu zisichezwe kwenye viwanja hivyo.

Ubovu wa viwanja hivyo si kwamba vinaumiza wachezaji, bali hata usalama kwa mashabiki kushuhudia mechi hizo unakuwa mdogo. Hivyo, TFF isikomalie kutoza faini au kuzikamua klabu fidia za usajili, iwe makini pia katika suala zima la viwanja vinavyochezwa mechi za ligi kuu.

Soka haliwezi kusonga mbele kama wachezaji wanaendelea kucheza katika viwanja vibovu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -