Wednesday, November 25, 2020

HILI LA VIBALI TFF INACHANGIA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TAARIFA za baadhi ya klabu hapa nchini kuvunja sheria kwa kuajiri wafanyakazi bila ya kufuata taratibu ni moja kati ya vitu vilivyoacha mshangao si tu ndani ya tasnia ya michezo, bali kwa taifa kwa ujumla.

Klabu za Yanga, Simba na Azam zimeripotiwa kuingia matatani kufuatia kuwatumia wachezaji na makocha ambao hawana vibali vya kuishi wala vile vya kufanya kazi hapa nchini.

Tatizo la wachezaji au makocha wa kigeni kuingia nchini na kufanya kazi bila ya vibali, imekuwa ni suala la kawaida sasa kiasi cha kufanya sasa kugeuka ni jambo la kawaida kwa wahusika.

Kitendo hicho kimeutia doa mchezo wa miguu kwa kudhihirisha wazi kuwa viongozi wake wengi ni wasiofahamu majukumu yao na pia ni wenye kupindisha sheria kuanzia za nchi hadi zile zinazoongoza mchezo husika.

Kimsingi suala hilo limeacha maswali mengi kwa wadau wa michezo hususani soka kutokana na ukweli kwamba wahusika wameshindwa vipi kuwafuatilia wageni ambao wanaingia nchini kupitia mipaka, njia zinazodhibitiwa huku wakiwa na taarifa juu ya wapi wanakwenda, wamekuja kufanya nini na watakaa nchini kwa muda gani pamoja na kuwa na anuani ya watakapofikia.

BINGWA linashauri kuwepo na msako mkali kuhusiana na wageni waliopo nchini ambapo kupitia udhaifu huu wa wachezaji wa kigeni kuna kila dalili ya sekta nyingine za michezo wakawepo wageni wanaofanana na hawa.

Hali hiyo inazitia aibu taasisi kama TFF na Uhamiaji kwa kuonekana zimezembea katika kutekeleza majukumu yao ya kazi mpaka zikumbushwe katika njia isiyopendeza.

Kwa mtazamo wa haraka chanzo kinaonekana ni klabu pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambao wote kwa pamoja wana uwezo wa kulidhibiti licha ya ukweli kubaki wazi kwamba imechangiwa kwa kiasi kikubwa na uzembe wa Uhamiaji, taasisi yenye dhamana ya kusimamia majukumu hayo.

TFF kama ambavyo inaheshimu sheria za nchi katika kutekeleza majukumu yake, nayo inapaswa kuhakikisha inatoa msaada kwa Serikali katika kuzifanya taasisi zake ziweze kutekeleza kwa urahisi majukumu yake.

Hakuna shaka kabisa ikiwa Uhamiaji na Wizara ya Kazi wakiamua kutumia sheria zilizopo waathirika wakubwa watakuwa ni klabu ambao kama wachezaji hao walishafanya kazi wakiamuriwa kuondoka nchini ni wazi klabu zitaingia hasara kubwa kwakuwa zimeshaingia gharama za usajili pamoja na nyingine kibao kama vile kuwalipa pango la nyumba.

BINGWA linaishauri sasa TFF kuweka utaratibu maalumu utakaozifanya klabu kabla ya kukabidhiwa leseni ni lazima wakamilishe vibali vya kazi na vya kuishi nchini kabla ya kukabidhiwa leseni za uhamisho wa kimataifa zinazowafanya wachezaji wa kigeni kucheza soka.

Tuna amini kupitia tatizo hilo inaweza kuwa funzo kwa TFF, taasisi inayopaswa kuendesha shughuli zake bila kuvunja sheria mama za nchi ikaja na utaratibu mwingine utakaoliacha soka la Tanzania likiwa safi bila ya kashfa yoyote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -