Tuesday, October 27, 2020

HIMID MAO, MZABE KIBAO MUDATHIR YAHYA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA HALID MTUMBUKA

NI mchezaji wa kipekee sana, ni binadamu mwenye nidhamu kimwonekano hadi kimchezo. Mara nyingi hucheza huku jezi yake ikiwa imechomekewa kwa dakika zote tisini, yupo mmoja tu anayeweza kuishi hivi kwa dakika zote uwanjani.

Aliwahi kuulizwa juu ya kucheza bila jezi yake kuchomoka kwa dakika zote uwanjani, alichokijibu kilikuwa ni rahisi tu, alisema huwa hajui kama jezi yake bado ameichomekea, anachokiwaza akiwa dimbani ni mchezo husika.

Huyu ni Himid Mao. Kuchomekea jezi uwanjani humaniisha ishara ya nidhamu kwa mchezaji. Nidhamu ikiwa kwa mchezaji, mchezo mzima utapambwa na sifa za nidhamu. Jicho geni likialikwa kutazama mchezo wa soka, litaanza kuuchambua kwa vitu vidogovidogo kama hivyo.

Himid Moa ni mmoja kati ya viungo wakabaji wanaocheza mpira wa kisasa. Ni kiungo anayetimiza majukumu yake, hajawahi kuyakwepa majukumu yake uwanjani.

Nani alimuona kwenye mchezo dhidi ya Zimbabwe? Alitulia sana kwenye mchezo ule, ni ngumu kuiona kazi yake kwa kuwa huwa hakai sana na mpira mguuni. Ndiyo maana ninasema, anacheza kisasa. Kwake pasi za kuliinua jukwaa zisizo na maslahi kwa timu huwa hashughuliki nazo.

Kwake sifa si kitu kinachomshughulisha. Mpira wa sasa unahitaji aina hii ya viungo ambao watakuwa wakipiga pasi sahihi kuanzia kwenye eneo lao kwenda mbele. Mpira wa kisasa unahitaji wasambazaji wa mpira, lakini wenye miguu inayoona mpira ulipo na akili zinazofanya kazi kwa kasi ya umeme.

Si mara ya kwanza kwa Himid kujaribu kutibua mipango ya wapinzani na kucheza kwa maslahi ya timu. Pale Azam wanamfahamu vizuri kijana huyu.

Kuna wakati Jaffar Idd alipoulizwa juu ya mwenendo mbovu wa Azam msimu huu, alisema pamoja na mambo mengine, majeruhi yamekiandama kikosi chao, alimtaja Shomari Kapombe, Pascal Wawa ambaye hayupo na Himid Mao kama wachezaji muhimu waliokosekana kikosini.

Kwanini Himid? Kuna baadhi ya michezo alitumika kama mlinzi wa kati, sifa hii ya kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani na kuitumikia kwa ufasaha inamfanya mchezaji kuitwa kiraka. Ni ngumu sana kuachwa kikosini kwa kuwa huweza kukuahidi vitu vingi.

Ni ngumu kuyataja mafanikio ya Azam bila kumgusa Himid. Haonekani sana, lakini ana mchango sana.

Mwendelezo wa kiwango bora uwanjani ni kielelezo kingine kinachoupamba ubora wake, yupo wapi Mwinyi Haji? Mwendelezo wa kiwango bora uwanjani umemficha nyuma ya kivuli chake, haonekani.

Himid amekuwa akitokea mara kwa mara kwenye orodha ya wachezaji wa Taifa Stars kwa kuwa amekuwa na mwendelezo wa kiwango chake uwanjani. Hana vitu vingi vitakavyomfanya ashindwe kuwa na mwendelezo.

Kichwa chake hakijasukwa mtindo wowote wa nywele, hakijanyolewa mtindo wowote unaoufahamu duniani, mchezo wake mkubwa ni ‘Play Station’, hapo ni pale alipomaliza majukumu yake, huituliza akili yake kwa kucheza mchezo huo. Kwanini asiwe na mwendelezo wa kiwango bora?

Himid Mao, naimba jina lako wakati huu.

Nilikuwa njiani na jamaa zangu tukijadili maendeleo ya soka la Tanzania, mmoja wetu akasema hivi inawezekana vipi kesho tuna mechi ngumu mchezaji anashinda kwenye ‘korido’ na simu mkononi akiwa anakesha kwenye mitandao ya kijamii? Akaendelea kuhoji, mchezaji saa saba usiku unamkuta yupo ‘online’ kwenye mitandao ya kijamii muda wa kupumzika anaupata saa ngapi?

Swali hili majibu wanayo wenyewe wachezaji wa Tanzania. Hivi kweli haya ndiyo maisha sahihi ambayo wachezaji wetu wanatakiwa kuyaishi? Mchezaji unakesha facebook? Huwezi kuwa na mwendelezo wa kiwango bora kwa aina hii ya maisha.

Mwili wa mwanamichezo unatakiwa kunyenyekewa, unahitaji kuhudumiwa ili uendelee kuzalisha huduma ile ile kila siku. Yote haya ni nadra kuyaona endapo utapitia kwenye ngazi zote zinazostahili.

Najaribu kuwaza, huenda Himid anaweza kwa sababu aliishi kwenye ngazi tofauti tofauti, kuanzia akiwa mdogo hadi hivi sasa. Ninaamini sasa kwanini wasemaji walituachia msemo usemao chochote ukipatacho kwa haraka, utakipoteza kwa haraka pia.

Umaarufu wa Mo Music leo hii umebaki kwenye Basi Nenda tu. Kwanini? Kuwa namba moja haijawahi kuwa kibarua kigumu tangu kuumbwa kwa dunia.

Anaimba nyimbo zenye ladha ile ile kila siku. Huu huitwa mwendelezo.

Sifa nyingine ya mashairi yake yanayoimbwa vizuri na miguu yake ni kuachia mpira haraka, kiuhalisia kuna nadharia isemayo kwamba, ukigusa mpira mara moja, ya pili uachie mpira ili kutengeneza mazingira ya kuifanya timu imiliki mpira kwa muda mrefu ikiwa na uhakika wa kutengeneza nafasi na kufungua njia kwa timu yenu.

Huu ni uchezaji kitimu. Lakini Himid anacheza na watu wa aina gani? Utakapogundua kwamba anaocheza nao bado wanacheza mpira wa kiuanafunzi, ndipo utakapogundua kwamba kumlaumu Ramadhan Singano ni sawa na kumbebesha mzigo wenye uzito mkubwa mabegani mwake.

Kuna wakati Himid hucheza kama ‘box to box midfielder’, ndiyo maana ilikuwa rahisi mno kwenye mchezo dhidi ya Zimbabwe kuanza kama kiungo pekee wa ulinzi kwenye mfumo wa 4-1-4-1, hapa unaweza kumuona akishuka na kupandisha mashambulizi, lakini mpango huu ulifeli kwa sababu hakukuwa na muunganiko mzuri, utendaji kazi wa pamoja na mgawanyo wa majukumu kutokana na idara kwenye mchezo ule.

Pale Azam tumeshamshuhudia akicheza sana na Mudathir Yahya kama viungo wawili wa ulinzi, ambao mmoja akishambulia, mwingine hubaki chini. Mudathir si yule tena siku hizi, hata jicho la Mkwassa halijavutiwa na taswira yake kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Mudathir Yahya alikuwa ni moja kati ya viungo wenye uwezo mkubwa sana, lakini alishindwa kuwa na mwendelezo, alipanda haraka mno na kuporomoka kwa kasi ile ile aliyoitumia kupanda.

Himid, mzabe kibao kizito mgongoni mwake. Mzabe kibao ili ashtuke na kujiuliza usahihi wa yeye kuendelea kuporomoka ngazi za ubora wake. Baadaye mfundishe namna ya kuishi kama na namba moja milele. Mudathir zinduka uishi kama zamani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -