Tuesday, November 24, 2020

HISTORIA ITAKAYOOKOA KIBARUA CHA ARSENE WENGER

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

BAADA ya timu yake ya Arsenal kupokea kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha Arsene Wenger, amezidi kuandamwa na presha kutoka kwa mashabiki wake.

Kumekuwa na maswali kama ataepushiwa aibu na historia yake ya kumaliza ligi vizuri ambayo inatabiriwa kutokea tena msimu huu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, alizungumza na vyombo vya habari huku sauti yake ikiwa si ile changamfu kama alivyozoeleka, Wenger alisisitiza kichapo cha Bayern bado hakijamshawishi kwamba huu ndio wakati sahihi wa yeye kuachana na washika bunduki hao wa London.

Alisema kwa sasa hana uamuzi hadi itakapofika Machi au Aprili mwaka huu, akifafanua zaidi kwa kusema bado ana matumaini ya hali kukaa sawa.

Wakati akiwa na imani juu ya uwezekano wa kikosi chake kuiangusha Bayern na kusonga mbele, Wenger pia bado ana matumaini ya Chelsea kuteleza kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England huku akilitolea macho kombe la tatu la FA ndani ya miaka minne ya hivi karibuni.

Ukimsikiliza Wenger na kuiangalia ‘fomu’ waliyonayo kwa sasa unaweza kupatwa na mashaka, lakini pia huenda Wenger akawa na sababu zake za kuwa na matumaini yote hayo.

Historia hiyo ya Arsenal kumaliza vizuri mwishoni mwa msimu, huwa inatokea hasa wanapoondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Machi kila mwaka, labda msimu huu mashabiki wanaweza kujirudi na kumpa ushirikiano Wenger kutokana na kiwango kukaa sawa.

Inakumbukwa mwaka 2014, Wenger alikuwa na miezi michache mno kabla ya mkataba wake kufikia tamati lakini alimaliza msimu vizuri na hilo lilijirudia tena na kufikisha idadi ya misimu minne ya Wenger kuwa na mwisho mzuri.

Ilikuwaje baada ya Arsenal kuondolewa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya?

2012-13:

Baada ya Arsenal kuondolewa na Bayern licha ya kuwa walikaribia kuiangusha miamba hiyo ya Ujerumani, sasa walibaki na kazi moja tu ya kufanya nayo ni kupigania kumaliza ligi katika nafasi nne za juu huku tayari wakiwa na machungu ya kuondolewa kwenye Kombe la FA.

Hadi kufikia katikati ya Aprili, Arsenal ilikuwa ikihaha kutoka kwenye nafasi ya tano na walipoamka kutoka usingizini, walishinda mechi nane na kutoa sare mbili katika mechi zao 10 za mwisho, ambapo waliinyuka Tottenham na kutinga nne bora kwa kishindo.

2013-14:

Kwa mara nyingine Wenger alikumbwa na presha ya hali ya juu msimu huo. Mkataba wake ulikuwa mwishoni na maisha yakazidi kuwa magumu baada ya kuondolewa tena na Bayern kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, siku chache tangu alipopokea kichapo kingine Stamford Bridge dhidi ya Chelsea.

Lakini Arsenal waliinuka walipoangukia na kutembeza vichapo vitano mwezi Aprili. Wakamaliza kwenye nafasi nne za juu na kama hiyo haitoshi wakafanikiwa kuondoa ukame wa miaka tisa bila taji kwa kunyakua Kombe la FA. Kombe hilo lilitosha kumfanya Wenger apewe mkataba mpya wa miaka mitatu.

2014-15:

Baada ya kuwahuzunisha mashabiki wao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kuondolewa kwao na AS Monaco, Arsenal walirudi na nguvu mpya iliyowafanya washinde mechi nne za ligi pamoja na ushindi mgumu dhidi ya Reading kwenye nusu fainali ya FA.

Katika harakati zao za kusaka nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu uliofuatia, Arsenal ilipoteza mechi moja tu dhidi ya Swansea, ikafuzu kucheza Ulaya na kubeba taji la pili mfululizo la FA.

2015-16:

Baada ya vijana hawa wa Wenger kutandikwa mabao 3-1 na Barcelona katika mchezo wa marudiano kule Camp Nou, walihakikisha hawamalizi vibaya kwenye ligi kwani walizibanjua timu tano na kutoa sare nne.

Ingawa walipoteza pointi muhimu kwa West Ham, Crystal Palace na Sunderland, bado walifanikiwa kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili.

Je, msimu huu Wenger ataokolewa na matokeo mazuri ya mechi za mwisho?

Kuna uwezekano mkubwa wa kuona mashabiki wakitaka apewe mkataba mpya hata kama akishinda taji jingine la FA. Lakini kama historia hii itambeba, ni mapema sana kusema ataondoka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -