Friday, November 27, 2020

HOFU KWISHA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

ZAITUNI KIBWANA NA SAADA SALIM

JAPO watu wa Simba wamekuwa wakitamba kuwa hakuna kitakachowazuia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, lakini pamoja na tambo zao hizo, walikuwa na hofu mioyoni mwao.

Unajua ni hofu gani? Si nyingine bali ni vipi washambuliaji wao wataendeleza makali yao katika ufungaji mabao waliyonayo kwa sasa.

Hofu hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, hakuna mchezaji mwenye uwezo wa kulazimisha, hasa mwenye ubavu wa kupambana na mabeki ‘wabishi’ wa timu zinazosaka majina kama Mbao FC na nyinginezo.

Katika hilo, mara kadhaa watu wa Simba walikuwa wakimkumbuka mshambuliaji wao, Frederick Blagnon, raia wa Ivory Coast ambaye walimuuza nchini Oman.

Kitendo cha kuondoka kwa Blagnon, kilimfanya Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, kubakiwa na washambuliaji ‘wepesi’ kama Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo, Pastory Athanas, Juma Luizio ambaye hata hivyo bado hajaonyesha cheche zake pamoja na mawinga Shiza Kichuya, Jamal Mnyate, Hija Ugando na kiungo mshambuliaji, Mohammed Ibrahim ‘Mo’.

Hapo ndipo watu wa Simba walipoanza kumkumbuka Blagnon wakiamini kuwa straika huyo ndiye ambaye angeweza kupigana vikumbo dhidi ya mabeki wa timu watakazopambana nazo katika mechi zao za mwisho na hivyo kutoa mwanya kwa akina Ajib kufanya yao kirahisi.

Na baada ya kilio cha muda mrefu, hatimaye Blagnon amerejea nchini na tayari amewasili jijini Arusha kuungana na wenzake.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema mshambuliaji huyo tayari ametua Arusha kuunganisha na wenzake kuelekea mchezo wao wa Jumapili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Madini FC.
“Blagnon amerudi na hapa tunavyoongea ameunganisha moja kwa moja kwenda Arusha,” alisema.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema: “Ujio wa Blagnon utaisaidia timu yetu kwani tunaamini kutokana na uwezo wake kwa ushirikiano na wachezaji waliopo, tutafanikisha azma yetu ya kutwaa ubingwa na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.”

Alisema wanafahamu kuwa wanakabiliwa na mechi ngumu za Kanda ya Ziwa kwa hiyo umoja wao hasa kwa upande wa wachezaji, utawasaidia katika mipango yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Simba imekuwa katika ukame wa mataji kwa misimu minne sasa lakini kwa hali ilivyo ndani hadi nje ya kikosi hicho, inaonekana Omog hatakuwa na kisingizio cha kushindwa kumhamisha ‘mwali’ kutoka Mtaa wa Jangwani yalipo maskani ya watani wao wa jadi, Yanga na kumpeleka kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -