Monday, January 18, 2021

HONGERA MANARA, MASHABIKI SI SEHEMU YA BENCHI LA UFUNDI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

WIKI mbili zilizopita, kulikuwa na taarifa zilizodai kibarua cha kocha wa Simba, Joseph Omog, kiko shakani. Ilivuma kuwa Mcameroon huyo angefungasha virago vyake katika siku za hivi karibuni.

Nyingine zilieleza kwamba, tayari uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi umempa mechi tano mkufunzi huyo wa zamani wa Azam na kama angeshindwa kupata matokeo mazuri, basi angetakiwa kukabidhi majukumu ya kuliongoza benchi la ufundi kwa kocha mwingine.

Hata hivyo, tetesi hizo zimezimwa na Mkuu wa Idara ya Habari klabuni hapo, Haji Manara, ambaye katika hilo ameonesha kiwango kikubwa cha weledi katika ufanyaji kazi wake. Hakika anastahili pongezi.

Manara, ambaye kimsingi ndiye mwenye dhamana ya kuzungumzia kila kinachoendelea katika klabu ya Simba, aliweka wazi kuwa viongozi hawajafikiria kuachana na huduma ya kocha huyo na ni mashabiki wa timu hiyo ndio wanaoibua presha hiyo.

Kiongozi huyo alisema mashabiki hawana weledi wa kuamua anayefaa kuwa mkuu wa benchi la ufundi. Hongera Manara.

Kwa hakika, zilikuwa ni habari za kushangaza kusikia mashabiki wa Simba wanataka Omog atimuliwe, ikizingatiwa kuwa ndiyo kwanza timu hiyo imecheza michezo mitatu tangu kuanza kwa msimu huu wa 2017-18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ni kweli kikosi chake cha sasa kimekuwa na tatizo kwenye safu ya ushambuliaji, lakini niliamini ni mapema mno kumhukumu Omog kwani bado ameendelea kuwa na matokeo ya kuridhisha.

Licha ya ubovu wa safu yake ya ushambuliaji yenye mastaa; Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo, Shiza Kichuya na John Bocco, tayari Simba imejikusanyia pointi saba kati ya tisa, pungufu ikiwa ni pointi mbili tu.

Lakini pia, Wekundu wa Msimbazi wana jumla ya mabao 10 yaliyopatikana katika mechi tatu, ukiacha mchezo waliokuwa ugenini dhidi ya Azam uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, ambapo timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana.

Kwa takwimu hizo, unaweza kugundua kuwa Manara yuko sahihi kukataa presha ya mashabiki wanaotaka Omog afukuzwe wakionekana wazi kutokuwa na hoja za msingi.

Lakini pia, ukiwa ni msimu wake wa pili kwenye benchi la ufundi, tayari kocha huyo amefanya kazi kubwa na inayotia moyo, ambapo amefanikiwa kuirejesha Simba kwenye michuano ya kimataifa.

Kabla ya Omog, itakumbukwa kuwa Simba ilishindwa kumaliza ligi ikiwa kwenye moja kati ya nafasi mbili za juu kwa misimu minne mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Iweje leo hii, ahukumiwe kwa mechi tatu, tena za mwanzoni mwa msimu, huku akiwa amedondosha pointi mbili pekee?

Binafsi ninaamini anachokifanya Manara ni kupingana na utamaduni uliozoeleka katika soka la Bongo, mashabiki kuwa na nguvu kubwa katika utendaji kazi wa kocha, ambayo imekuwa moja kati ya sababu nyingi za soka la Tanzania kushindwa kupiga hatua.

Hasa katika klabu kongwe za Simba na Yanga, mashabiki wamekuwa chanzo cha kufukuzwa kazi kwa makocha, jambo ambalo Manara ameonekana kuanza kulifanyia kazi na kulikomesha kwa upande wa Simba.

Kwa miaka mingi, viongozi wa timu hizo wamekuwa wakiwatoa kafara makocha, lengo likiwa ni kujisafisha kwa mashabiki wao, hasa pale wanapoweza kuonekana wameshindwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya uwanjani.

Kulijua hilo, hebu jiulize, kulikuwa na hoja ya msingi kumtimua Marcio Maximo pale Jangwani, kama si viongozi wa Yanga kufuata presha ya mashabiki wao? Ilikuwa hivyo pia kwa Micho. Viongozi walizidiwa nguvu na presha ya mashabiki waliotaka atimuliwe, lakini leo hii Mserbia huyo anatamba na Orlando Pirates ya Ligi Kuu Afrika Kusini, baada ya kuachana na kibarua kingine cha kuinoa timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’.

Ni kweli Micho ana kiwango kidogo, kiasi kwamba anatakiwa kuzinoa The Cranes na Pirates na si Yanga?

Viongozi walifanya kile walichokitaka mashabiki, ambao misingi ya weledi inatambua kuwa kazi yao ni kushangilia na kutoa maoni na si kuingilia masuala ya kiufundi ikiwamo kuchagua kocha anayepaswa kuliongoza benchi la ufundi.

Ni wazi Manara anapaswa kupongezwa kwa kile alichowaambia mashabiki wa Simba, kuwa suala la hatima ya Omog haliwezi kutoka kwao.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -