Wednesday, November 25, 2020

HONGERA SINGIDA UNITED, LIPULI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TIMU za Singida United na Lipuli ya Iringa tayari zimefanikiwa kutinga Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18

Timu hizo zinasubiri nyingine moja itakayoungana na timu hizo kucheza  Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

BINGWA tunazipongeza timu hizo kwa kufanikiwa kutinga Ligi Kuu Bara, tukiamini kwamba moto mliouwasha katika Ligi Daraja la Kwanza mtapanda nao ligi kuu ili kuhimili mikikimikiki ya ligi hiyo yenye timu 16.

Timu hizo mbili zote zimewahi kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kuteremka na hatimaye baada ya kupambana kwa miaka mingi zimefanikiwa kurejea tena.

Kimsingi Ligi Kuu Tanzania Bara si  lelema mama, hivyo kama wadau wa soka tunapenda kuzikumbusha Lipuli na Singida United umuhimu wa kufanya maandalizi ya kina ili kuepuka kuwa wasindikizaji wa timu nyingine na kisha mkarudi mlikotoka.

Upo mfano wa timu ya African Sports ambayo ilishuka daraja na kupotea kwa muda mrefu na ilifanikiwa kurudi Ligi Kuu msimu wa 2015-16, lakini kwa sababu ilikuwa haijajiandaa sawa sawa kwa changamoto mpya ilijikuta ikishuka tena daraja baada ya msimu mmoja tu.

Kwa mfano huu wa timu ya African Sports, BINGWA tunaamini hili litakuwa somo kwa timu za Lipuli na Singida ambazo zimefanikiwa kurejea Ligi Kuu baada ya kuhaha bila mafanikio kwa miaka mingi.

Tunaamini ili kuepukana na janga lililoikuta African Sports, Lipuli na Singida United zitasajili wachezaji wanaoendana na changamoto za Ligi Kuu.

Zaidi ya hapo tunatarajia wakazi wa mikoa inayotoka timu hizo mtaendelea kuziunga mkono ili ziweze kuwapa burudani ambayo mliikosa kwa miaka mingi.

Tunatarajia kuwa mashabiki wa mikoa hiyo wataungana kuhakikisha timu hizo zinapata maandalizi mazuri ili ziweze kushiriki kikamilifu katika Ligi Kuu msimu ujao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -