Saturday, November 28, 2020

HONGERA YANGA, SIMBA KWA SOKA SAFI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LIGI Kuu Tanzania Bara iliendelea wikiendi iliyopita kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo miamba ya soka nchini, Simba na Yanga, ilioneshana kazi katika vita hiyo ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Kama ilivyo desturi ya mchezo huo wa watani wa jadi, umati mkubwa wa mashabiki ulifurika kushuhudia timu zao hizo zikipambana kwa ajili ya taji msimu huu.

Simba ambao ndio vinara wa ligi kuu, waliingia kwenye mchezo huo wakiwa ndio vinara wa ligi na pointi 51, huku Yanga wakiwafuatia na pointi 49, kila mmoja alikuwa na nia ya kuhakikisha anazikusanya pointi tatu muhimu.

BINGWA tulitarajia kuona soka safi lisilo na ukakasi kutoka kwenye timu zote mbili kutokana na maandalizi mazito kabla ya mchezo, hasa suala la kuweka kambi nje ya Jiji la Dar es Salaam, jiji ambalo limekuwa ni makazi yao ya muda mrefu.

Katika kutambua hilo, BINGWA tuliridhishwa na hatua ya timu hizo kuheshimu uzito wa mchezo wenyewe hasa kwa kuwa ingetoa nafasi kwa timu zote mbili kuupata utulivu wa kutafuta mbinu za kupata ushindi na kufanyia kazi mapungufu yao kabla ya mchezo.

Matarajio yetu BINGWA ya kuona soka la kiufundi baina ya klabu hizi kongwe nchini yalitimia, baada ya timu zote kuchuana dakika zote 90 na mshindi kupatikana kihalali bila mikwaruzano yoyote.

BINGWA tunazipa pongezi timu hizo kwa kuja na mrejesho mzuri wa maandalizi yao kabla ya mchezo, upinzani wao ulionekana zaidi uwanjani na hakika umaarufu wa mtanange huo ulizidi kuongezeka ndani na nje ya nchi kwa kiwango bora kilichooneshwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Tunatarajia kuona mchezo mwingine mzuri baina ya timu hizo pindi zitakapokutana tena na tuna matumaini ya kuiona mechi bora zaidi ya wapinzani wa jadi ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -