Friday, November 27, 2020

HONGERENI SIMBA KWA KUBADILISHA KATIBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MWISHONI mwa wiki iliyopita wanachama wa Simba kwa wingi wao walipitisha kipengele cha uendeshaji wa klabu kwa muundo wa hisa, katika mkutano mkuu wa dharura wa mabadiliko ya katiba uliofanyika ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay.

Wanachama hao wamefikia hatua hiyo baada ya mwenzao ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’, kutangaza nia ya kuweka hisa ya asilimia 51 (51%) lengo likiwa ni timu hiyo kuendeshwa kisasa zaidi.

Kwa ujumla hiyo ni hatua kubwa sana kwani kwanza mkutano wenyewe ulifanyika katika hali ya amani na utulivu na pili ni wanachama wenyewe walioamua kwa kauli moja kupitisha mabadiliko hayo.

Mkutano huo ambao uliongozwa na Rais wa klabu, Evance Aveva, ulihudhuriwa na wanachama 642 hiyo ikimaanisha kuwa kulikuwa na mwamko mkubwa.

Huwa linapotokea jambo jema lazima lisifiwe na sisi kama BINGWA tunatoa pongezi kwa wanachama wa Simba kwa kufikia makubaliano hayo kwa nia moja na ni matumaini yetu kuwa mchakato mzima utamalizika kwa amani kubwa.

Labda jambo la kukumbushana hapa ni kwamba, uwekezaji katika klabu si kitu cha kushangaza kwani hata baadhi ya timu kubwa barani Ulaya zipo kwenye mifumo hii, hivyo Simba hawajafanya muujiza na badala yake kilichobakia waungwe mkono.

Simba kama ilivyo kwa Yanga wana umri mkubwa lakini hakuna la maana wanaloweza kujivunia, linapokuja suala la kucheza mechi za kimataifa na pia hakuna maendeleo yoyote kama ilivyo kwa wenzao Azam FC.

Azam FC licha ya kwamba bado hawajafikisha umri wa miaka 20, lakini wanamiliki uwanja wao na huwezi kusikia wachezaji wao wakilia mara kwa mara kwamba hawajapewa mishahara yao, lakini kwa Simba na Yanga hayo yamekuwa mambo ya kawaida sana.

Kama timu hizi zinaingia katika mfumo huu wa hisa ni wazi wafanyabiashara mbalimbali watajitokeza kumwaga fedha, ni suala la kujenga viwanja na kulipa mishahara kwa wachezaji bila shida tena.

BINGWA tunaamini kuwa hatua waliyoipiga Simba ni kubwa sana na ambacho tunaweza kuishauri, ni kwamba uongozi, wanachama pamoja na mashabiki waendelee kushikamana kwani mpango huu ukikamilika kikamilifu watayafurahia matunda yake.

Kama kauli mbiu yao inavyosema ‘Simba Nguvu Moja’, tunaamini kuwa maneno hayo hayaishii mdomoni peke yake bali yatatekelezwa kwa vitendo.

BINGWA kama gazeti linalopenda maendeleo ya michezo linaamini kuwa huu ni mwanzo tu na timu nyingine zitafuatia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -