Saturday, October 31, 2020

Wenger aliwanasa kwa bei poa wakapiga mzigo wa maana

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KOCHA Arsene Wenger anasherehekea miaka 20 tangu alipokabidhiwa kibarua cha kuinoa Arsenal.

Lakini, Wenger amekuwa na kawaida ya kutumia fedha kiduchu katika harakati za usajili, jambo ambalo limekuwa likisababisha ashindwe kuelewana na baadhi ya mashabiki wake.

Licha ya ‘ubahili’ wake huo kwenye soko la usajili, Mfaransa huyo ana historia nzuri ya kununua wachezaji kwa fedha kiduchu na hatimaye wakawa na msaada mkubwa klabuni hapo.

Thierry Henry

Hakuna shabiki wa soka ambaye hakukubali kipaji cha striaka huyo raia wa Ufaransa, hasa linapokuja suala la kuwatungua magolikipa.

Alitua Gunners mwaka 1999 kwa ada ndogo ya pauni milioni 11 akitokea Juventus.

Wenger alimbadilisha namba kutoka winga hadi mshambuliaji wa kati.

Ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuifungia Arsenal mabao mengi, ikiwa ni baada ya kupasia nyavu mara 175.

Emmanuel Petit

Mchezaji mwingine ambaye alibadilishwa namba na Wenger ni Petit.

Alihamia Arsenal akiwa beki, lakini Wenger alimtaka kucheza nafasi ya kiungo.

Wenger alimnasa Mfaransa mwenzake huyo kutoka Monaco kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 2.5 na hiyo ilikuwa ni mwaka 1997.

Mpaka anajiunga na Barcelona mwaka 2000, staa huyo alikuwa amecheza michezo 118 na aliuzwa kwa pauni milioni 7.

Patrick Viera

Ni mmoja kati ya wachezaji wa mwanzo kusajiliwa na Wenger.

Alimnasa kwa pauni milioni 3.5, lakini aliipa timu hiyo makombe sita.

Alikuwa sehemu muhimu ya safu ya kiungo ya Arsenal kwa kipindi chote alichokuwa klabuni hapo.

Freddie Ljungberg

Alitokea katika klabu isiyojulikana ya Halmstads iliyopo Sweden. Uhamisho wake uliigharinmu Arsenal pauni milioni tatu pekee na hiyo ilikuwa mwaka 1998.

Katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Arsenal, alipachika bao dhidi ya Manchester United.

Katika misimu mitano aliyodumu London, alipachika jumla ya mabao 72.

Robin van Persie

Ingawa aliikacha Arsenal na kujiunga na mahasimu wao, Man United, hilo halimfanyi Van Persie kufutwa kwenye historia ya klabu hiyo.

Alipohamia Arsenal, straika huyo wa kimataifa wa Uholanzi alianza kusumbuliwa na majeraha.

Katika michezo 238 aliyoichezea Arsenal kabla ya kutimkia Old Trafford, staa huyo alipachika mabao 132.

Ikumbukwe kuwa Wenger alimnunua mkali huyo kwa ada ndogo tu ya pauni milioni 2.5 akitokea Feyenoord.

Robert Pires

Alijiunga na Arsenal akitokea Marseille kwa pauni milioni sita.

Hiyo ilikuwa ni wakati anaondoka alikuwa ameshapasia nyavu mara 84 katika mechi 284.

Cesc Fabregas

Ni kitita cha pauni 500,000 kilichoitoka Arsenal kumpata Fabregas kutoka Barcelona.

Aliingia kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 16 kabla ya baadaye kuukwaa unahodha.

Kabla ya kurejea Barca kwa ada ya pauni milioni 30, Fabregas aliifungia Arsenal mabao 57 katika michezo 303.

Kolo Toure

Mwafrika huyo alitua kwenye mikono ya mzee Wenger kwa pauni 150,000, lakini aliibuka kuwa shujaa kwenye kikosi cha Gunners.

Akitokea ASEC Mimosas, aliweza kupenya na kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Gunners ambapo alicheza sambamba na Sol Campbell katika safu ya ulinzi.

Kabla ya kujiunga na Manchester City mwaka 2009, beki huyo aliichezea Arsenal michezo 326.

Lauren

Akitokea Mallorca kwa ada ya pauni milioni 7.2, beki huyo wa pembeni aliiongoza Arsenal kushinda mara mbili taji la Ligi Kuu England na matatu ya Kombe la Ligi.

Sol Campbell

Akiwa kinara wa safu ya ulinzi, Mwingereza huyo aliiwakilisha Arsenal katika michezo 211.

Alipachika mabao 12, likiwemo lile alilofunga mwaka 2006 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona.

Nicholas Anelka

Alisajili na Wenger akitokea Paris Saint-Germain na ada yake ya uhamisho ilikuwa ni pauni 500,000.

Baadaye, Wenger alimuuza kwenda Real Madrid kwa pauni milioni 22.3.

Marc Overmars

Licha ya majeraha ya mara kwa mara, Wenger aliamua kucheza kamari kwa kumsajili Overmars.

Alimnyakua kutoka Ajax mwaka 1997 kwa dau la pauni milioni 5.

Mpaka anatimka Arsenal, Mholanzi huyo alikuwa amepachika mabao 41 katika michezo 142.

Wenger alimpiga bei kwenda Barca na hapo kocha huyo alivuna pauni milioni 30.

Jens Lehman

Mlinda mlango huyo aliicheza Arsenal kwa vipindi viwili tofauti.

Kwa mara ya kwanza, alitua Arsenal kwa ada ya pauni milioni 1.5 akitokea Borussia Dortmund.

Kutokana na umahiri wake langoni, alinyakua tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka Ligi Kuu England katika msimu wa 2003-04

Gilberto Silva

Wenger alitumia pauni milioni 4.5 kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.

Baadaye, alikuwa nguzo imara kwenye sehemu ya kingo ya timu hiyo na hata alipotimka kwenda Olimpiacos, ilichukua muda mrefu pengo lake kuzibika.

Laurent Koscielny

Ni pauni milioni 10 pekee iliyotumika kumng’oa Mfaransa huyo pale Lorient.

Amekuwa msaada mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya kikosi cha mzee Wenger katika siku za hivi karibuni.

Aaron Ramsey

Akitokea Cardiff City, Ramsey alijiunga na Arsenal kwa ada ya pauni milioni 5.

Alianza kuingia kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 17.

Ana rekodi ya kuwa mchezaji wa tano kufunga bao Ligi Kuu England akiwa na umri mdogo.

Katika msimu wa 2013-14, alitupia mabao 16 katika michezo 30.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -