Monday, January 18, 2021

HUJUMA NZITO YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara jijini Arusha baada ya kudai kubaini hujuma wanayofanyiwa Dar es Salaam.

Wanajangwani hao ambao kwa sasa wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 12, wamekuwa wakihaha kupata ushindi wa mabao mengi.

Katika michezo hiyo, Yanga haijapoteza hata moja, ila bado haijawaridhisha mashabiki wao kutokana na ushindi kiduchu wanaopata.

Habari za kutoka ndani ya Yanga ambazo BINGWA imezipata, jana uongozi uliitisha kikao cha dharura na kujadili mkakati mpya wa mechi zao zilizobaki baada ya kubaini hujuma kutoka kwa wapinzani wao.

Inadaiwa kuwa Yanga imekuwa ikishinda kwa tabu kunatokana
na njama chafu zinazofanywa na wapinzani wao, zinazosababisha wachezaji kuchoka kabla ya dakika 90 kumalizika.

Chanzo kutoka ndani ya Yanga,

kimesema kuwa kuna mtu asiyejulikana ambaye amekuwa akijipenyeza ndani ya kambi yao iliyopo Kigamboni na hata kwenye vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani na kuwafanyia mchezo mchafu.

“Yanga tumebaini si hali ya kawaida inayotufanya tushindwe kupata mabao tunayohitaji katika michezo yetu na utafiti tuliofanya, tumegundua kuna hujuma zinafanywa na wapinzani wetu.

“Tunadhani kuna mtu yupo ndani yetu anatumiwa, tena inawezekana tupo naye kila siku na anajipenyeza hadi kambini Kigamboni. Sasa

ili kujiepusha na hili, tunafikiria kuhamishia mechi zetu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha au sehemu nyingine tutakayoona inafaa,” alisema.

Hivi karibuni bada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema wanafikiria kupeleka mchezo mmoja katika mkoa mmojawapo wa Kaskazini.

Alisema uongozi unafikiria mkoa sahihi wa Kanda ya Kaskazini ili kuwapelekea burudani mashabiki wao na inawezekana ukawa wa dhidi ya Ruvu Shooting.

“Tunashukuru kuendelea kukusanya alama tatu katika michezo yetu na kukaa kileleni, kutokana na kuwathamini mashabiki wetu wa kila eneo, tunafikiria mechi yetu na Ruvu Shooting kupeleka mkoani.

“Mikoa tunayofikiria ni ya Kaskazini, tutaangalia ni mkoa
upi utapendekezwa na viongozi, baadaye tutautangaza ili mashabiki wetu wajiandae kuipokea timu yao,” alisema Nugaz.

Yanga inatarajia kucheza mechi tano Ligi Kuu Bara mwezi huu,
mbili wakiwa wenyeji dhidi ya Ruvu Shooting Jumapili hii na nyingine na Dodoma Jiji, Desemba 19.

Mechi tatu zitakazokuwa ugenini ni dhidi ya Mwadui ya Shinyanga Desemba 12 (Shinyanga), Ihefu FC Desemba 26 (Sokoine) na kumalizia na Tanzania Prisons Desemba 31 (Mandela, Sumbawanja).

Msimu huu, kanuni za Bodi ya
Ligi zimetoa nafasi kwa kila timu kuchagua mkoa wowote wa kwenda kucheza mechi mbili.

Hadi sasa, KMC ndiyo imetumia nafasi moja baada ya mchezo wake na Yanga kwenda kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -