Wednesday, October 28, 2020

Huu ndio mwisho wa Ibrahimovic?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

“Jose anapenda kushinda, hata mimi mwenyewe na wote tunajua kile tunachokitaka. Kila tunapokwenda tunashinda na tutashinda.”

Kama kulikuwa na mtu ana mashaka juu ya mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu England, basi alikuwa kwenye safari ya pekee yake, ambapo ilikuwa wazi kwamba Jose Mourinho atafanikiwa Manchester United.

Mechi nne za mwanzoni mwa msimu akiwa United, Ibrahimovic alifunga mabao manne. Alianza kufunga bao kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kisha kufuatiwa na bao moja kwenye ligi na kuongeza mabao mawili akiwa kwenye Uwanja wa Old Trafford. Ilionekana kama amejiandaa kuishi kwenye dunia ya kipekee.

Lakini miezi miwili mbele, mambo yanaonekana kwenda mrama. Zlatan amefunga bao moja katika mechi zaidi ya tisa. Tangu afunge dhidi ya Zorya Luhansk kwenye Ligi ya Europa, hajafunga tena na kiwango chake kikionekana kuwa tofauti.

Katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City ulikuwa mmoja wa mchezo wake mbaya kuwahi kucheza kwa miaka kadhaa. Aliingia kwenye mechi hiyo ambayo kila aliposhuka kusaidia timu, alikuwa akipoteza mipira ovyo. Alishindwa kabisa kutoa pasi nzuri na kucheza vibaya kuliko wachezaji wote wa United katika kipindi cha kwanza.

Kuhama kwake mara kwa mara kulisaidia kipindi cha pili, baada ya kumzungusha beki, Nicolas Otamendi na kutoa pasi kwa Juan Mata aliyefunga bao la ushindi kwenye mchezo huo. Amekuwa akishindwa kumalizia mipira ya krosi za juu, katika mechi tatu mfululizo amepoteza nafasi za wazi za mipira ya aina hiyo.

Katika mechi dhidi ya Chelsea, alipiga kichwa kilichopaa juu baada ya krosi nzuri ya Antonio Valencia, ambapo mechi hiyo walichapwa mabao 4-0, kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool siku kadhaa zilizopita, pia alikosa bao la wazi akishindwa kuunganisha krosi ya Paul Pogba na kufanya mbinu za kocha wao, Jose Mourinho, zitiliwe shaka.

Inashangaza kuona mchezaji mwenye kiwango kama cha Ibrahimovic mwenye kujiamini akifanya makosa kama hayo, lakini kutokana na umri wake wa miaka 35, hiyo ndiyo inaweza ikawa sababu ya kushindwa kuwa kwenye kiwango chake.

Kasi yake imepungua miaka kadhaa iliyopita, halafu kwa wale waliocheza soka la Ligi Kuu England watakwambia kasi ya ligi hiyo inahitaji nguvu zaidi.

Kama kunahitajika nguvu, basi Zlatan anaweza, ila jambo linalotia shaka ni kiwango chake. Wengi wanahoji kama ana uwezo wa kubadilika na kuonyesha kiwango chake. Lakini kutokana na uwepo wa wachezaji kama Marcus Rashford na Anthony Martial, wanaweza kuisaidia timu hiyo mbele ya goli.

Huenda huu usiwe mwisho wa Zlatan, lakini ndio anaelekea mwisho wa soka lake. Anaweza kusaidia timu yake lakini itakuwa ngumu kwake kuonyesha uwezo wake kila wiki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -