Monday, November 30, 2020

HUU NDIO UKWELI HALI ILIVYO YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, pamoja na kuendelea kupeta kwenye michuano ya kimataifa, huku pia wakiwa na nafasi kubwa kutetea ubingwa wao huo, ukweli ni kwamba, kuna mambo mengi yanayoikabili timu hiyo ambayo iwapo hayatafanyiwa kazi, hali inaweza kuwa mbaya zaidi msimu ujao.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na BINGWA, Yanga inakabiliwa na mambo saba ambayo ndiyo hasa yanayohatarisha ubingwa wao, kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na kuanza kuwatia hofu mashabiki, wanachama na viongozi wao.

Ukata

Jambo la kwanza ni hali ya kifedha ambapo kwa sasa klabu hiyo inaonekana kutokuwa vema, tofauti na ilivyokuwa misimu ya hivi karibuni, hali inayoweza kuiathiri katika suala zima la mishahara ya wachezaji na makocha, lakini pia kuhimili mikikimikiki ya usajili na mengine kama hayo.

Tangu kiongozi wa klabu hiyo kukumbwa na misukosuko, Yanga imeonekana kuyumba mno kifedha na matokeo yake wachezaji kukosa morali wa kuitumikia timu kiasi cha kujikuta kutofanya vema kwenye baadhi ya mechi, hasa ile ya kimataifa ya nyumbani dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Iwapo hakutajitokeza watu wa kuokoa jahazi mapema, Yanga inaweza kujikuta ikiondokewa na nyota wake, hata wale wanaowategemea, lakini pia kushindwa kusajili wachezaji wenye kiwango mwishoni mwa msimu.

Maximo, Eto’o, Drogba

Tatizo lingine linaloikabili Yanga kwa sasa ni kuwa na kikosi chenye wachezaji walioitumikia timu hiyo kwa muda mrefu zaidi kiasi cha kupoteza nguvu za kuendelea kupambana pale inapobidi kufanya hivyo, ili kupata matokeo mazuri.

Wachezaji kama Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Haruna Niyonzima ambao ndio tegemeo zaidi Yanga, wamepoteza makali, kwani waliitumikia timu kwa muda mrefu zaidi, tena wakifanya hivyo kwa nguvu kubwa na uwezo wao wote tangu enzi za kocha Mholanzi Ernie Brandts, Mbelgiji Tom Saintfiet hadi Mbrazil Marcio Maximo.

Mbali ya kuitumikia Yanga, wachezaji hao hao pia ndio waliokuwa tegemeo katika vikosi vya timu zao za taifa zilizoshiriki michuano ya Afrika dhidi ya timu zenye wachezaji wanaotamba Ulaya kama Samuel Eto’o, Didier Drogba, Yaya Toure, Robinho, Kaka na nyota wengineo wengi, kiasi kwamba wamepoteza nguvu za kupambana kama walivyokuwa enzi zao.

Kwa upande wa nyota wao wa kimataifa kama Thaban Kamusoko, Justice Zulu na Donald Ngoma, nao wanaonekana wazi kutokuwa na nguvu za kuipigania timu kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi Yanga inatakiwa kujenga kikosi kipya chenye vijana wenye uchu na uwezo wa kupambana kupata mafanikio, lakini pia uzalendo wa hali ya juu kuipigania timu pale inapobidi.

 

Hamasa

Timu ya Yanga kwa sasa imeonekana kukosa hamasa na hilo linathibitishwa na mahudhurio ya mashabiki timu inapocheza, kwani ni wachache mno wanaofika, hali inayoonekana kuwavunja moyo wachezaji.

Lakini pia kitendo cha bosi wa Yanga kuwa matatani kwa sasa, kimeongeza hali ya kutojiamini ndani ya klabu hiyo kutokana na ukweli kwamba, ilikuwa ikimtegemea kwa mambo mengi.

Mapedeshee

Yanga imekuwa ni timu inayosifika kwa kuwa na matajiri wenye uwezo wa kuokoa jahazi pale mambo yalipoonekana kwenda kombo, lakini kwa sasa watu hao wanaonekana kusambaratika.

Miongoni mwao ni Hussein Ndama ‘Pedeshee Ndama’, Mussa Katabaro na wengineo ambao kwa sasa wamesambaratika.

Wakati Pedeshee Ndama akiwa mikononi mwa polisi kutokana na tuhuma mbalimbali, wengineo wamekaa kimya kiasi cha kushindwa kuokoa jahazi kutokana na hali ya ukata inayoikabili Yanga kwa sasa.

Kinachotakiwa kwa sasa ni vibopa wa Yanga kujikusanya upya na kuona ni vipi wanaweza kuweka mambo sawa Jangwani ili kurejesha furaha waliyokuwa nayo mashabiki na wanachama wao.

 

Kwa kuhitimisha, hiki kinaonekana kuwa kipindi muhimu mno kwa watu wenye mapenzi na Yanga kujitoa kadri ya uwezo wao, iwe ni kimali au kihali kuona ni vipi wanaisaidia klabu yao iweze kukabiliana na changamoto mbalimbali, zaidi ikiwa ni ya kifedha.

Iwapo kila mmoja atajiweka pembeni, watu wa Yanga wasijeshangaa kuiona timu yao ikizidi kuporomoka kadri siku zinavyozidi kwenda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -