Saturday, October 31, 2020

HUU NDIO UTAMU WA LIGI YA CHINA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

BEIJING, China

KATIKA miaka ya hivi karibuni China imejipatia umaarufu mkubwa kwenye ulimwengu wa soka baada ya ligi kuu nchini humo kuwavuta mastaa wengi kutoka Ulaya.

Cha kushangaza zaidi ni pale wachezaji wenye majina makubwa wanapoamua kuzitema klabu za Ulaya na kukimbilia China ambako hata hivyo ligi yao haina ushindani mkubwa.

Kwa lugha nyingine, sasa klabu za Ulaya zinapata upinzani mkubwa kutoka Ligi Kuu nchini China hasa linapokuja suala la usajili.

Fedha ndio kisu cha Wachina

Hakuna shaka kuwa fedha ndio kila kitu kwenye soka la kisasa na ni wazi klabu za China zimethibitisha hilo.

Kwa pamoja, Jackson Martinez, Ramires na  Alex Teixeira, walitua China na kiasi kilichotumika kinatajwa kuwa ni pauni milioni 90 (zaidi ya shilingi bilioni 250 za Kitanzania).

Kutokana na utumizi mkubwa wa fedha unaofanywa na Wachina, tayari kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema dunia inatakiwa kuogopa.

“Ndiyo, kwa sababu China wanaonekana kuwa na nguvu ya fedha inayoweza kuuhamishia mchezo wa soka kwao. Tunajua inatokana na nguvu ya kiuchumi waliyonayo,” alisema.

Hata hivyo, Wenger alitahadharisha kinachofanywa na China akiwatolea mfano Japan ambao walijaribu kufanya hivyo kabla ya kupotea.

Kumbe Rais wao ndiye aliyesababisha

Baada ya kufanya vizuri kwenye mapinduzi ya viwanda, Rais wa China, Xi Jinping, alitangaza kuwa sasa China inatakiwa kupiga hatua kwenye medani ya soka.

Wakati alipotembelea England, alifika hadi kwenye uwanja mpya wa mazoezi wa Manchester City na kujionea wenzao walivyopiga hatua.

Kuanzia hapo, amekuwa akihimiza maendeleo ya soka nchini kwake, ikiwamo ujenzi wa viwanja vya michezo na kuhimiza vijana kusakata kabumbu.

Kutokana na mkazo wa Xi, tayari wawekezaji wa China wamekuwa wakiingia kwa kasi kwenye biashara hiyo ya soka huku wanamichezo na ligi maarufu barani Ulaya zikianza kuwa na ushirikiano mzuri na China.

Jose Mourinho alikuwa jijini Shanghai kipindi fulani na sasa mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour, ameuza asilimia 13 ya hisa zake kwa wawekezaji kutoka China.

Kwa mujibu wa Xi, lengo lake ni kuhakikisha uchumi wa michezo nchini China unakuwa na utajiri wa dola bilioni 8 ifikapo mwaka 2025.

Mbali na mipango mingine, pia lazima China ije kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia katika siku za usoni.

Kuna sheria zinazowalinda wachezaji wazawa

Mipango ya kukuza soka la China haiishii kwenye uwekezaji wa nje ya uwanja, kuna mipango mizuri imewekwa kuhakikisha wachezaji wazawa wanapewa kipaumbele.

Mfano; kuna sheria zinazolenga kuwalinda wachezaji wazawa kwa kutamka wazi kuwa walinda mlango wote wa ligi kuu lazima wawe Wachina.

Katika mchezo mmoja, timu haitakuwa na haki ya kuchezesha zaidi ya wachezaji watatu wa kigeni.

Usidhani watafilisika!

 Imeelezwa kuwa licha ya matumizi makubwa ya fedha katika soko la usajili, klabu za Ligi Kuu China zimeendelea kuingiza mpunga mrefu.

Mwaka huu pekee mkataba wa miaka mitano wa haki za matangazo ya televisheni uliipatia ligi hiyo kitita cha dola bilioni 1.25.

Kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na kile kilichopatikana mwaka jana ambapo ligi hiyo iliingiza dola milioni 9.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -