Wednesday, November 25, 2020

HUU NI MUDA SAHIHI WA SAMATTA, BAILEY HAYUPO TENA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA AYOUB HINJO


DIRISHA dogo la usajili la kimataifa limefungwa rasmi Januari 31, saa sita usiku. Pamoja na dirisha hilo kufungwa, timu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imefanikiwa kuingiza pauni milioni 42 kutokana na mauzo ya wachezaji wake.

Leon Bailey, Wilfred Ndidi, Christian Kabasele na Neeskes Kebano ni baadhi ya wachezaji waliouzwa na klabu hii ya Genk ambayo anachezea Mbwana Samatta kwenye dirisha dogo la Januari.

Bailey amekwenda zake Bayern Leverkusen ya nchini Ujerumani. Ndidi amejiunga na bingwa mtetezi wa EPL, Leicester City. Kabasele ameingia mkataba wa kuitumikia Watford inayoshiriki Ligi Kuu England na Kebano ametimkia Fulham inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini England.

Nyota ya Bailey ilianza kung’aa mapema sababu ni mchezaji mwenye kipaji cha asili ambaye miguu yake imejaaliwa uwezo wa hali ya juu kuuchezea mpira na kusababisha hatari kwa wapinzani.

Uwezo wa Ndidi umemfanya kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Leicester City. Jamaa ni kiungo mkabaji, kazi yake anaifanya vyema katika ulinzi na hata kusaidia mashambulizi, amekuja kuziba pengo la Ngolo Kate aliyekiacha kikosi hicho na kujiunga na Chelsea.

Kabasele na Kebano ni wachezaji wa nafasi tofauti lakini ubora na uwezo waliouonyesha ndio umewatoa Genk na kuwapeleka walipo sasa.

Genk hawa hawa ndio waliofanya biashara na Aston Villa kwa Christian Benteke. Yule Kevin De Bruyne unayemuona ndani ya jezi ya Manchester City, alikuwa palepale Genk kabla ya Chelsea timu na nyingine hazijamuona na hatimaye kuja Man City.

Ni wazi inaonekana Genk ni timu ya biashara ambayo hutegemea soko la wachezaji kuwa sehemu kuu ya kuinua uchumi wa timu hiyo. Asilimia kubwa ya wachezaji wanaonunuliwa na Genk wanatokea ligi ndogo zisizojulikana duniani.

Hao wote niliowataja, hapo awali walikuwa ni wachezaji tegemeo wa Genk lakini sasa wameuzwa na wapo kwenye ligi za juu duniani.

Kuondoka kwa akina Bailey kunatoa nafasi pana kwa Samatta kuonyesha uwezo wake. Sababu uwepo wa Bailey ulikuwa unaleta mgawanyo wa magoli, yaani hakukuwa na mtu maalumu katika kufunga.

Ni rahisi kwa Samatta kuonekana  na kuanza kuuvaa ufalme wa Genk kama alivyofanya pale TP Mazembe na wakati ule alipokuwa Simba SC na baada ya Mazembe kumuuza Tresor Mputu ambapo Samatta akachomoza.

Unadhani Samatta akiwa kwenye ubora wake atabaki palepale Genk? Unajidanganya, kwani Genk ni wafanyabiashara hawataweza kuendelea kumng’ang’ania kwa hilo, kwa sababu wanapenda kufanya biashara wapate faida lakini pia waendelee kupata sifa kwamba ni moja ya klabu inayouza wachezaji.

Kwa ubora na uwezo ule wa Samatta wakati  yupo Mbagala Market, uliwafanya vigogo wa Simba SC kukesha wakisaka saini yake, huku wakiwa na ahadi ya kumpatia gari kijana wa miaka 18.

Tofauti kubwa ya Samatta na Nikos Karelis ipo kwenye aina ya mpira wanaoucheza. Karelis ni mshambuliaji anayesubiri kufanyiwa kazi kisha yeye anamaliza kwa kufunga, lakini Samatta si mshambuliaji tegemezi sana kwa sababu ana uwezo wa kujitafutia mwenyewe au kutengeneza nafasi kwa wengine. Sifa hizo alizonazo Samatta zinatosha kumpa ulaji popote pale sababu dunia ya mpira wa sasa haiwahitaji sana washambuliaji wasiokuwa tegemezi.

Njaa ya mafanikio aliyonayo Samatta ni kali mno. Uwepo na umuhimu wake sasa unaweza kuwa mkubwa sababu anatakiwa kuongoza jahazi sambamba na Karelis, huku timu yake ikiwa bado inashiriki Europa na ligi kuu. Ana nafasi ya kuwa mfalme, pia ana uwezo wa kuwafanya mashabiki wa Genk waimbe jina lake kila timu hiyo inapocheza.

Jinsi alivyoingia na kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo iliyo Ubelgiji, anaonyesha anahitaji kuwa zaidi ya hapo alipo. Takwimu zake za sasa zinambeba japo ni muda mfupi tu tangu ajiunge na klabu hiyo.

Kama Benteke alitoka na kwenda Aston Villa, sasa kwanini nafasi ya Samatta iwe finyu wakati washambuliaji wa aina yake ndio wanaohitajika zaidi kwa sasa?

Timu nyingi za daraja la kati kama Sunderland, Everton, Watford, Real Sociedad, Malaga na nyingine nyingi hununua wachezaji wazuri na wenye uwezo kutoka timu ambazo ziko ligi zisizojulikana sana.

Mara nyingi hata hizo timu za daraja la kati nao hununua wachezaji kusikojulikana ili wafanye biashara kwa timu zilizo juu yao kiuwezo kama ilivyotokea biashara nzuri ya Benteke kwenda Liverpool. Kwa kipaji alichonacho Samatta, inaonekana hatakaa sana pale Ubelgiji. Muda bado upo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -