Sunday, November 29, 2020

HUYU NDIYE ANAYEIWEZA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA SAADA SALIM,

KAMA ni upele, tunaweza kusema kuwa umepata mkunaji na iwapo itakuwa ni gari la bia, basi limeharibikia pembeni ya nyumba ya mlevi…hivyo ndivyo ilivyo Yanga kwa sasa.

Unakumbuka tatizo la Haruna Niyonzima lililokuwa likiwafanya baadhi ya mashabiki wa Yanga kumponda? Kama umesahau, ni kitendo cha kuwa na tabia ya kuchelewesha ‘move’ kwa kupenda kukaa na mpira muda mrefu, ikiwamo kurudisha mipira nyuma.

Watu wa Yanga walikuwa wakiamini kuwa, kitendo hicho kilikuwa kikiwanyima mabao, kwani kila pale timu ilipokuwa ikipanga mashambulizi, kiungo huyo alipopata mpira, alianza ‘kuupaka mafuta’ na pale alipoamua kutoa pasi, alikuwa ameshachelewa.

Ukiachana na tatizo hilo, makocha wengi wa Yanga walikuwa ni wazito kubaini tatizo la kiungo mkabaji kiasi cha kutoa mwanya kwa timu pinzani kuwazidi ujanja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Wana-Jangwani hao.

Lakini kupitia mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumamosi ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kila mpenzi wa soka atakubaliana na BINGWA kuwa, timu hiyo imempata mtu sahihi ambaye iwapo atapewa muda na kutokwazwa kwa namna moja ama nyingine, anaweza kuifikisha mbali timu hiyo, zaidi ikiwa ni kwenye michuano ya kimataifa.

Unajua ni vipi? Katika mchezo huo dhidi ya JKT Ruvu ambao Yanga walishinda mabao 3-0, Niyonzima alionekana kubadilika mno ambapo hakuwa akirudisha mipira nyuma wala ‘kucheza na jukwaa’, badala yake, kila alipopata mpira, alichojua ni aidha kupiga pasi hatari za mwisho au ‘kupunguza’ pale alipoona inafaa kufanya hivyo.

Ni kutokana na mabadiliko yake hayo kiuchezaji, alifanikiwa kutengeneza mipira ya mabao takribani saba, huku mitatu ikitumiwa vema na Simon Msuva na kuzaa mabao hayo.

Hakuna ubishi, mabadiliko hayo ya Niyonzima yametokana na ujio wa kocha mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, ambaye ni wazi alibaini kasoro za kiungo huyo kupitia mikanda ya video aliyoipitia mara alipotua nchini na kufanyia kazi udhaifu huo.

Ukiachana na hilo, Lwandamina pia alifahamu ubora wa Niyonzima, hasa katika suala zima la kumiliki mpira, utulivu, uamuzi sahihi, ujanja, ubunifu na mengine kama hayo, hivyo kuamini kuwa Mnyarwanda huyo ana uwezo wa kucheza namba 10 kwa mafanikio makubwa.

Lwandamina alimpandisha Niyonzima kucheza namba hiyo kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe, baada ya kumwingiza Said Juma Makapu kucheza namba sita baada ya Yanga kuzidiwa na JKT Ruvu katika safu ya kiungo iliyokuwa ikiongozwa na Hassan Dilunga.

Mabadiliko hayo yalionyesha wazi kuwa, Lwandamina alibaini udhaifu wa safu ya kiungo wa ulinzi iliyokuwa ikichezwa na Thaban Kamusoko, ambaye kiasili ni kiungo mshambuliaji, hivyo alimpandisha ‘dimba la juu’, nafasi aliyokuwa akicheza Niyonzima.

Mabadiliko hayo ambayo yalikuwa ni nadra kufanywa na makocha wa hivi karibuni wa Yanga, yaliimaliza kabisa JKT Ruvu, walioonekana kuwa tishio kwa vijana hao wa Jangwani ambao mwisho wa siku, walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa.

Kwa jinsi alivyojionyesha Jumamosi, Lwandamina anaweza kuwa mtu sahihi mno Yanga kutokana na uwezo wake wa kuusoma ubora na uchezaji wa vijana wake na wa timu pinzani, lakini pia nini kifanyike ili kuwafurahisha mashabiki wa klabu yao.

Mambo aliyoyafanyia kazi Lwandamina ndani ya muda mfupi, ndiyo ambayo yamekuwa yakiigharimu mno Yanga, hasa katika michuano ya kimataifa na kujikuta ikikubali kufungwa mabao ya dakika za lala salama.

Hakika Yanga sasa imepata mwenyewe anayeiwezea ambaye si mwingine, bali ni George Lwandamina.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -