Tuesday, October 27, 2020

Huyu ndiye hatari zaidi Simba SC

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS,

KIKOSI cha Simba kimeendelea kuwaacha njiapanda wale wote waliokuwa wakikibeza kuwa huenda kikaishia ‘kunawa’ katika harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kama ilivyokuwa misimu takribani minne iliyopita.

Baada ya ligi kufikia raundi ya tano, huku Shiza Kichuya akionekana kuwa tishio zaidi ndani ya kikosi cha Simba, wapo walioamini kuwa kasi ya mchezaji huyo ni nguvu za soda na kwamba hataweza kuikwamua timu yake hiyo kutoka katika ukame wa mataji unaowakabili Wekundu wa Msimbazi hao.

Ubashiri huo ulielekea kuwa kweli pale Kichuya alipotoka kapa ndani ya mechi tatu na hivyo kuamini huenda mchezaji huyo akawa amepoteza mwelekeo na hivyo huo kuwa mwanzo wa Simba kuyumba.

Kichuya alishindwa kucheka na nyavu katika mechi dhidi ya Mbao, Kagera Sugar na Toto Africans, kabla ya kuzifumania nyavu za Mwadui mwishoni mwa wiki iliyopita katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata ugenini.

Kitendo cha Kichuya kutofunga huku akishindwa kumaliza dakika zote 90, kilianza kuwafanya wapinzani wa Simba na hata baadhi ya wapenzi wa timu hiyo, kuamini winga huyo amepoteza makali, ikiwa ni baada ya kuanza kwa kishindo na kujikuta akiongoza katika orodha ya wafungaji mabao.

Japo kuna walioibuka kwa kuwa mashujaa wa timu hiyo katika mechi hizo tatu, akiwamo Muzamiru Yassin, lakini bado kudorora kwa Kichuya aliyekuwa akipewa nafasi kubwa kuwa shujaa wa Simba, kulionekana kuwashtua wengi.

Lakini wakati mashabiki wa soka nchini wakionekana kuelekeza macho na akili yao kwa Kichuya na hata pengine Laudit Mavugo, Muzamiru, Ibrahim Ajib na wengine wenye jukumu la kutikisa nyavu za timu pinzani, BINGWA limebaini kuwa kuna mchezaji ambaye inaonekana wazi ndiye ‘roho’ ya Simba.

Mchezaji huyo ni kijana aliyetua Msimbazi msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ambaye uchezaji wake unaweza kulinganishwa na ule wa kiungo wa zamani wa Simba, Hussein Masha, zaidi ikiwa ni utulivu wake anapokuwa na mpira, kujiamini na zaidi alivyo fundi wa kujua ni wakati gani anatakiwa kupiga au kutoa pasi.

Huyo si mwingine bali ni Mohammed Ibrahim ambaye watu wa Simba wamempachika jina la Mo Ibrahim.

Ibrahim ameonyesha kuwa na kipaji cha hali ya juu cha soka, miguu, mwili na akili yake, vikionekana kama kuwa na undugu na mpira, kutokana na jinsi anavyouchezea kadiri anavyotaka.

Gazeti hili limekuwa likimfuatilia katika mechi takribani tano alizocheza na kubaini vitu adimu alivyonavyo, zaidi ikiwa ni utulivu, sifa waliyoikosa baadhi ya wachezaji hodari wa hapa nchini na hata wale wa kigeni wanaolipwa mamilioni ya fedha.

Moja ya mfano wa sifa ya utulivu aliyonayo kiungo huyo mshambuliaji, ni bao alilofunga Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo aliinasa kwa uhodari wa hali ya juu pasi ndefu ya juu na kujitengea pasi kwa kifua, kabla ya kukokota kidogo na kumchambua kipa Shaaban Kado na kufunga.

Ibrahim alifanya vitu adimu kadhaa katika mchezo huo kama ilivyo kawaida yake, ikiwamo krosi ‘iliyokwenda shule’ iliyozaa bao la pili lililofungwa na Kichuya katika ushindi wa mabao 3-0.

Kwa jinsi inavyoonekana, iwapo Ibrahim ataendelea kuaminiwa na kupewa nafasi zaidi, hakuna shaka kuwa Simba itakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Bara kwani ana uwezo wa kuwapikia akina Kichuya mabao kila atakapotaka, lakini pia kufunga.

Uzuri wake, si mchoyo wa pasi kama ilivyo kwa baadhi ya washambuliaji wa Simba, lakini pia akiwa ni fundi wa kujua auweke wapi mpira ambapo mwenzake anaweza kuukuta na kuzitikisa nyavu za timu pinzani.

Tayari baadhi ya mashabiki wa Simba wameanza kutambua mchango wa mchezaji huyo ambapo wamekuwa wakimshangilia kila baada ya mchezo, wakionekana kuthamini mchango wake.

Kwa tathmini iliyofanywa na BINGWA katika mechi za hivi karibuni, imeonyesha kuwa kwa sasa Mo Ibrahim ndiye kipenzi zaidi cha mashabiki wa Simba kuliko hata ilivyo kwa nyota kadhaa wa timu hiyo.

Juu ya mchezaji huyo, kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema: “Ni mchezaji mzuri sana na tunaamini atakuwa na msaada mkubwa kwa timu yetu, hilo halina shaka. Tutajitahidi kumjenga ili awe bora zaidi kama ambavyo tumekuwa tukifanya, ikumbukwe uwezo alionao sasa si ule aliokuja nao hapa (Msimbazi).”

Kikosi cha Simba kwa sasa kinaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 32 kutokana na mechi 12, kikifuatiwa na Yanga yenye pointi 27 baada ya kushuka dimbani mara 12 pia, huku Stand United iliyoweka kibindoni pointi 22, ikiwa nafasi ya tatu, lakini ikiwa na mchezo mmoja zaidi ya wakongwe hao wa soka nchini.

Majimaji ndiyo inayoshika mkia kwa kuwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Toto Africans (pointi 11), JKT Ruvu (pointi 12) na Ndanda yenye pointi 13 sawa na Mwadui ambao wao wameshuka dimbani mara 12, huku Mbao ikiwa na pointi 13 ilizozipata ndani ya mechi 13.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -