Friday, December 4, 2020

Huyu Sven achana naye:Akusanya data zote za Tanzania Prisons, atamba mtaji wao upo kiganjani mwake

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA WINFRIDA MTOI

AMA kweli ‘Simba mwendapole, ndiye mla nyama’. Hilo limejidhihirisha kwa Kocha Mkuu wa Simba,Sven Vandenbroeckambaye pamoja na ukimya wake, kumbe data zote za Tanzania Prisons zipo mikononi mwake.

Simba inatarajiwa kucheza na Prisons keshokutwa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, Rukwa.

Kuelekea mchezo huo, kikosi cha wachezaji 22 cha Simba kimeondoka Dar es Salaam jana kuwafuata wenyeji wao hao, huku Sven akitamba amejipanga kuzoa pointi zote tatu.

Wachezaji waliokosekana katika safari hiyo, ni nahodha John Bocco na Gerson Fraga wanaouguza majeraha pamoja na Clatous Chama na Pascal Wawa waliopo nje ya nchi wakishughulikia hati zao za kusafiria makwao.

Simba imekwenda Sumbawanga ikiwa imetoka kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kushinda mabao 3-1.

Akizungumzia mchezo wao wa keshokutwa, Sven alisema anafahamu aina ya mchezo anaokwenda kukutana nao ambao utakuwa ni mgumu kutokana na soka wanalocheza Prisons.

Sven alisema anaufahamu vizuri uchezaji wa Prisons, ikiwamo kutumia nguvu zaidi, hivyo amekiandaa kikosi chake kwa mbinu nyingi na kuwaweka wachezaji tifi zaidi ili kukabiliana na ‘mtaji’ huo wa wapinzani wao.

“Prisons nawafahamu vizuri, wanacheza soka la nguvu, lakini matumaini ya sisi kufanya vizuri ni makubwa kutokana na ubora wa kikosi cha wachezaji 22 ninachoondoka nacho.

“Tutahakikisha tunafanikiwa malengo yetu ya kuondoka na alama tatu muhimu kwani tumejiimarisha katika kila idara kuwakabili wapinzani wetu,” alisema Sven.

Kocha huyo alisema muda waliotumia kufanya maandalizi ya mchezo huo, ni mrefu kuliko mechi nyingine zilizopita, hali inayowapa wachezaji wake kujiamini na hivyo kufanikisha malengo yao ya kuondoka uwanjani na pointi zote tatu.

Simba iliyopo nafasi ya pili na pointi 13 katika msimamo wa ligi hiyo, inataka kuendeleza ushindi ili kuifukuzia Azam inayoongoza na pointi 18.

Pamoja na mechi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons, Simba inakabiliwa na pambano la aina yake dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, litakalopigwa Novemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -