Wednesday, October 28, 2020

IBISEVIC AELEZA ALIVYOKWEPA SHAMBULIZI LA KIGAIDI BERLIN

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

BERLIN, Ujerumani

JUMAPILI iliyopita jiji la Berlin lilikumbwa na mshituko baada ya kuibuka kwa shambulizi la kigaidi lililopoteza maisha ya watu 12 karibu na duka la mapambo ya Krismasi la Breitscheidplatz, jijini humo.

Na mmoja wa watu waliokuwapo katika eneo hilo alikuwa ni mshambuliaji wa klabu ya Hertha Berlin, Vedad Ibisevic, ambaye ameeleza namna alivyonusurika kwenye shambulizi hilo lililohusisha lori kubwa lililoua watu hao usiku wa Jumapili.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Bosnia alisema kuwa, tukio hilo lilishitua wengi ndani ya klabu yake na yeye, mama na mkewe walikuwapo ndani ya duka hilo kabla ya shambulizi kufanyika.

“Tulishitushwa sana na tukio hilo, kwani limetokea baada ya mimi, mke wangu na mama kuondoka eneo hilo,” alisema.

Katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia jana baina ya Hertha na Darmstadt katika dimba lao la nyumbani la Olimpiki, wachezaji na makocha walikaa kimya kwa dakika moja ili kuwaombea wahanga wa tukio hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -