Thursday, December 3, 2020

IBRAHIMOVIC AITAHADHARISHA CHELSEA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

STRAIKA Zlatan Ibrahimovic ameitumia salamu Chelsea akisema ubingwa wa juzi walioupata katika michuano ya Kombe la EFL, ni ishara kuwa bado wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na huku akiwataka wenzake kuendelea na vita hiyo.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Wembley, straika huyo mwenye umri wa miaka 35, alizifumania nyavu mara mbili na kuwawezesha vijana hao wa Jose Mourinho kuondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton.

Taji hilo ni la pili kwa Man United baada ya Agosti mwaka jana kutwaa Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City ikiwa ni mechi yake ya kwanza   Ibrahimovic aliweza kupachika bao.

Kwa sasa Man United inashiriki kwenye michuano ya Ligi ya Europa hatua ya 16, robo fainali ya Kombe la FA na inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kutokana na hali hiyo, Ibrahimovic amepania mataji mengine zaidi kabla ya kufika mwishoni mwa msimu huu.

“Tutazidi kufanya hivi,” staa huyo alikiambia kituo cha televisheni cha MUTV.

“Kuanzia mwanzoni mwa msimu kuna makombe matano na sasa tumeshatwaa mawili, hivyo bado kuna matatu,” aliongeza staa huyo.

Alisema kwa hivyo baada ya kutwaa hilo la juzi kwa sasa wanayafukuzia matatu yaliyobaki likiwamo la ligi kuu kwa kile alichodai kwamba mbio bado ziko wazi.

Kwa sasa Chelsea ndio wanaoongoza kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kujikusanyia pointi 63 idadi ambayo ni zaidi ya pointi 15 dhidi ya Man Utd.

Hata hivyo, pamoja na mashetani hao wekundu kuzidiwa kwa idadi hiyo, raia huyo wa Swiden anadai si tatizo kubwa kwao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -