Friday, December 4, 2020

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA BRIGHITER MASAKI

UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi kwa jina la Ibra anayetoka katika kundi la Konde Gang.

Hii inatokana na juhudi zake ambazo amekuwa akizionesha katika kazi yake zilizosababisha kusajiliwa na mkali wa Bongo Fleva nchini, Rajab Abdul ‘Harmonize’ ambaye ni mmiliki wa kundi la Konde Gang.

Ibra ambaye jina lake halisi alilopewa na wazazi wake ni Ibrahim Abdallah, ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye nyota yake imeanza kung’ara baada ya kujiunga na lebo ya Konde Gang.

Ibra ambaye anatamba na ngoma kali kadhaa kama Nitachelewa, Wandoto, Nani, One Night Stand na Sawa, ameendelea kufanya vizuri katika muziki huo akibebwa na kipaji chake cha hali ya juu, lakini pia jitihada katika kazi yake hiyo.

Wiki iliyopita, BINGWA lilikutana na msanii huyo na kufanya naye mahojiano kuhusiana na safari yake ya muziki na maisha yake kwa ujumla.

ELIMU

Katika mahojiano hayo, Ibra anasema kuwa amepata elimu ya msingi wilayani Tandahimba, Mtwara na kuhitimu mwaka 2011 kabla ya kujikita muziki baada ya kutambua ana kipaji hicho.

JINSI ALIVYOBAINI KIPAJI CHAKE

Ibra anasema  alianza kutambua kuwa ana kipaji cha kuimba tangu yupo darasa la pili, ndipo safari yake ya kimuziki ilipoanza.

Anasema alianza kuimba akiwa shuleni katika matamasha mbalimbali na kuendelea na fani hiyo hata baada ya kumaliza shule.

“Baada ya kumaliza shule, ndipo nilipoanza harakati za muziki na tulikuwa tunashindana sana kimuziki ambapo nilikuwa nashinda na kuwa msanii bora wa kata na safari iliendelea,” anasema.

Anasema kulitokea tamasha la wilaya ambapo lilitoa nafasi kwa wanaojua kuimba kwenda kushindana na alijitokeza na kuibuka kidedea.

“Baada ya kuona nimefika levo ya msanii wa wilaya, niliamua kuhamishia muziki wake Dar es Salaam kwani mara nyingi msanii wa mkoani kufanikiwa ni vigumu sana,” anasema.

SAFARI YAKE KUTOKA MTWARA MPAKA DAR 

Baada ya kumaliza elimu ya msingi na kushindwa kusomeshwa na wazazi wake kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha aliamua kugeukia ufundi selemala.

Anasema alifanya kazi hiyo kwa muda wa miezi kadhaa kisha kuachana nayo na kuja mkoani Dar es Salaam na kufikia Yombo Bakwata.

“Baada ya kufika Dar es Salaam ambapo nilifikia kwa mjomba wangu nikapewa msingi wa shilingi 100,000 na kuanza na biashara ya kuuza CD, nikawa ninachukua mzigo Kariakoo kisha kupitisha katika maeneo mbalimbali,” anasema.

Anasema baada ya kufanya hiyo kazi ya CD, akageukia uuzaji wa makoti ya mtumba aliyokuwa akinunua Kariakoo na kuyatembeza katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

“Kupitia kuuza makoti ya mtumba, kukanifanya kuijua Dar es Salaam vizuri zaidi kwani nilikuwa ninapita maeneo mengi ,lakini pamoja na biashara hiyo, nilikuwa natenga muda wa kufanya mazoezi ili ikitokea nafanya muziki, basi nafanya kweli,” anasema.

Anasema kulikuwa na mjomba wake ambaye alikuwa amsapoti anaitwa Duke ambaye alikuwa anamuonyesha njia za kupita ili afanikiwe kwenye muziki.

“Huyo mjomba wangu Duke ambaye alikuwa anaishi Mtwara, alipata kazi ya kuwa dereva wa mama yake Harmonize, alimpigia na kumpa hiyo taarifa juu ya ofisi ya Harmonize,” anasema.

Anasema baada ya mjomba wake kumuelekeza zilipo ofisi za Harmonize, alihamua kufunga safari na kwenda ili kujaribu bahati yake na kuzidi kukuza muziki wake.

“Kweli, nilikuwa naenda mara kwa mara Sinza pale, lakini kuonana na Harmonize ilikuwa ngumu, lakini pia upande wa mtaji wa makoti ulikata na kuna muda nilikuwa naenda hapo ofisini kumuangalia Harmonize kwa miguu.

“Mjomba aliendelea kunipa sapoti ambapo alinitumia hela za kufanya muziki ambapo alimtumia produza Bonga na nikafanya kazi na ndipo ofisi ya Harmonize ikanisikia na kuomba kukutanishwa na mimi na ndipo nikakutana na Harmonize kwa mara ya kwanza,” anasema.

Anasema baada ya kukutana na Harmonize, alimweleza kuhusu ndoto zangu na msanii huyo alimpa moyo na kumtaka aongeze juhudi lakini pia alimpa nafasi ya kwenda ofisini kwake. 

KUHUSU KONDE GANG

Ibra anasema Konde Gang ni watu ambao wanapenda kazi kuliko kitu chochote na ndiyo siri yaao ya kufanikiwa zaidi.

ANAMZUNGUMZIAJE HARMONIZE?

Ibra anasema Harmonize pamoja kwamba ni bosi wake, lakini amekuwa kama rafiki na kaka kutokana na namna ambavyo amekuwa akimshauri kuhusu muziki wake.

Anasema Harmonize ni mtu ambaye anapenda sana kufanya kazi hata wakati mwingine anakuwa wa kwanza kufika studio na wa mwisho kuondoka.

CHANGAMOTO ANAZOKUTANA NAZO

Ibra anasema kazi yoyote ni lazima iwe na changamoto, lakini yeye kwake changamoto ni kama motisha ya kuendelea kupambana na kuhakikisha anafika mbali kisanaa, hivyo hajawahi kuzichukulia maanani.

“Kazi yoyote lazima iwe na changamoto, lakini mimi kwangu changamoto hazijawahi kunifanya kukata tamaa maana bila kuwa na moyo wa kujitoa, nisingefika hapa, nilipotoka ni mbali sana,” anasema.

USHAURI WAKE KWA VIJANA

Ibra amewataka vijana kutokukata tamaa katika kukipigania kile ambacho wanaamini kinaweza kuwanyanyua katika maisha yao.

“Vikwanzo au changamito vinaweza kuwa vingi, lakini kama kweli una nia na kitu fulani, usichoke kukipigania na utafanikiwa tu, hakuna aliyeandikiwa kukosa,” anasema.

Anasema yeye mpaka kufika alipo, ni juhudi zake na kutokukata tamaa, huku akiweka wazi kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa msanii mkubwa atakayeiwakilisha nchi kimataifa na kuinua vipaji vya vijana wengine.

Ibra alizaliwa mwaka 1998 katika hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salam akiwa ni mwenyeji wa Mtwara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -