Wednesday, November 25, 2020

IFAHAMU VITA YA GUARDIOLA NA MOURINHO NJE YA UWANJA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

KWA kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na Pep Guardiola wa Man City, wamekuwa na vita kubwa ndani ya uwanja tangu walipokuwa wakizinoa klabu za Inter Milan, Barca na Real Madrid.

Lakini msimu huu wakiwa kwenye Ligi Kuu England, makocha hao wameibukia kwenye vita nyingine ya kifedha ambapo Mourinho ametajwa kuwa kocha anayekamata kipato kikubwa, takribani mara mbili ya kile anachokusanya Guardiola kwenye msimu wake huu wa kwanza.

Katika orodha iliyotolewa mapema wiki hii na jarida la France Football, ni kwamba Mreno huyo ataweka kibindoni pauni milioni 24.2, fedha itakayomfanya awe kocha anayelipwa zaidi duniani.

Kiasi hicho cha fedha kinamfanya Mourinho ambwage mbali Guardiola ambaye atakusanya jumla ya pauni milioni 12.5, ambapo mshahara na marupurupu anayoyapata Man City pamoja na ‘madili’ ya biashara yote yakijumuishwa ndani yake.

Kwa mwaka Mourinho ambaye anakamata mshahara wa pauni 15 pale United, lakini nje ya ofisi yake United ana mikataba mingi aliyoandikishiana na makampuni kwa ajili ya matangazo yakiwamo kuonekana kwenye tangazo maarufu la Heineken, saa za Hublot, kampuni ya magari ya Jaguar, kituo cha michezo cha BT Sport, Adidas, hoteli za Atlantis na EA Sports.

Mikataba hiyo imemsaidia Mourinho kumpiku Guardiola kwenye orodha ya makocha wanaokamata mkwanja mrefu, kutokana na Mhispania huyo kutojihusisha sana na mambo mengine nje ya uwanja kama Mourinho.

Umaarufu alionao Mourinho ndio unaomletea fursa ya matangazo ya kibiashara.

MAKOCHA WANAOKAMATA FEDHA NONO

  1. Jose Mourinho (Man United)-Pauni mil. 24.2
  2. Marcello Lippi (China)- Pauni mil. 20.3
  3. Laurent Blanc (hana klabu)- Pauni mil. 17.3
  4. Carlo Ancelotti (Bayern Munich)- Pauni mil. 13.7
  5. Pep Guardiola (Man City) – Pauni mil. 12.5
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -