Monday, August 10, 2020

Ilanfya, Simba wamalizana

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya KMC, umethibitisha mchezaji wao, Charles Ilanfya, atajiunga na Simba muda wowote baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho unaofanywa na pande zote mbili.

KMC imeweka wazi kuwa ilimuachia mchezaji huyo afanye mazungumzo na Simba kabla ya kukamilisha dili hilo, kinachosubiriwa ni timu hizo mbili kukubaliana baadhi ya vipengele vya mkataba ili mchezaji huyo awe mali ya Simba.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio hapa nchini, Katibu Msaidizi wa KMC, Walter Harrison, alithibitisha kuwepo kwa mazungumzo ya mwisho baina yao na Simba, akiamini siku chache zijazo mambo yatakuwa yamekamilika.

Alisema Ilanfya bado ana mkataba na KMC, Simba ilituma maombi ya kutaka kumsajili na yalikubaliwa na kumruhusu mchezaji huyo kujadiliana maslahi binafsi na timu hiyo.

“Ni kweli Ilanfya anakaribia kujiunga na Simba, uhamisho wake utakamilika hivi karibuni, tupo kwenye mazungumzo na wenzetu na jana nilikuwa nawasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba (Senzo Mbatha) kuhusu usajili huo.

“Tupo katika hatua ya kukubaliana vipengele vya usajili, moja ya vipengele ni kwamba KMC imeweka sharti la kupata mgao wa fedha endapo mchezaji huyo atauzwa kwingineko, tunasubiri wenzetu wakikubaliana na matakwa hayo basi dili litakamilika muda wowote kutoka sasa,” alisema Harrison. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -