Sunday, November 29, 2020

Ilkay Gundogan; Usajili wa bei chee, majeruhi, lakini atambeba Guardiola

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

KAMA ulikuwa hujui, kiasi walichotumia Manchester City kumnunua staa Ilkay Gundogan hakifii kile alichopata wakala aliyemuuza Paul Pogba kwenda Manchester United.


Gundogan ambaye alitokea Borussia Dortmund, aliigharimu Man City pauni milioni 21 pekee.

Wakala aliyesimamia mpango wa Pogba kuhamia Old Trafford akitokea Juventus, Muitalia Mino Raiola, alilamba pauni milioni 24 kukamilisha mchakato huo.

 

Wakati Man City walipowaduwaza Barcelona kwa kuwachapa mabao 3-1, Gundogan alipasia nyavu mara mbili na Kevin De Bruyne alifanya hivyo mara moja.

 

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Etihad, Gundogan alikuwa silaha ya ushindi kwa Man City.

 

Kama ulibahatika kuutazama mtanange ule wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabibngwa Ulaya, utakubali kuwa staa huyo aliivuruga safu ya kiungo ya Barca Kwa kiasi kikubwa.

 

Ikumbukwe kuwa siku nne kabla ya kuwavaa Barca, Man City waliisambaratisha West Bom kwa mabao 4-2 na Gundogan alicheka na nyavu mara mbili.

 

Baada ya mchezo huo, Guardiola alizungumza na wandishi wa habari na kuwaambia: “Nilimwambia, ‘asante’,” alisema Guardiola.

 

“Tunamuhitaji. Bila yeye hatuwezi kufikia malengo yetu, itakuwa ngumu.”

Wachambuzi wa soka wamedai kuwa Gundogan ndiye mrithi wa Yaya Toure kwenye kikosi hicho.

 

Wakati wa majir ya kiangazi, wengi walitabiri kuwa Man City wameingia chaka hasa kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimwandama Gundogan.

Majeruhi yalisababisha nyota huyo akose Fainali za Mataifa ya Ulaya za mwaka huu ‘Euro 2016’.

 

Tangu alipopona majeruhi ya goti, Gundogan ameshafunga mabao matano katika michezo tisa aliyocheza.

 

Kwa upande wake, Pogba ambaye ada yake ya uhamisho ya pauni milioni 89 ilivunja rekodi ya usajili duniani, ameshindwan kuthibitisha thamani yakle pale Old Trafford.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Gundogan ameshacheza mechi sita za Ligi Kuu England ambapo amepasia nyavu mara tatu.

 

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, nyota huyo amepata nafasi ya kuingia uwanjani mara nne na kufunga mabao mawili.

 

Guardiola alimnunua Gundogan baada ya kuvutiwa na kazi zke alipokuwa na Dortmund iliyokuwa ikinolewa na Mjerumani Jurgen Klopp.

 

Kabla ya kukubali kutua Etihad, Gundogan alikuwa akifukuziwa na mabingwa wa Bundersliga, Bayern Munich.

Alipotua Ligi Kuu England, Gundogan alikaririwa na waanduishi wa habari akisema: “Sababu kubwa ya uhamisho wangu ni fursa ya kuungana na Pep Guardiola na Manchester City,” alisema.”

“Guardiola aliniombva nije Manchester na falasafa yake ilinishawishi.”

Hata hivyo, imeoneskana kuwa kiwango cha Gundogan kimekuwa kikipanda tangu alipotua Dortmund mwaka 2011.

 

Kiungo ghuyop alitua Dortmund akitokea Nurnberg huku ada ya uhamisho wake ikitajwa kuwa ni pauni milioni 3.

 

Akiwa chini ya Klopp, Gundogan alinyakua taji lake la kwanza pale Dortmund.

Kwa kipindi hicho, Klopp alimtaja Gundogan kama mchezaji mwenye akili nyingi na anayependa kujifunza.

 

Alikuwa moto wa kuotea mbali pale alipokiwezesha kikosi chake hicho cha Dortmund kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Alikuwa sehemu imatra ya safu ya kiungo wakati Dortmund ilipowachapa Real Madrid katika mchezo wa hatua ya nusu fainal ya michuano hiyo.

 

Pia, alifunga bao kwa mkwaju wa penalti katuika mchezo wa fainali ambapo Dortmund walianguimkia pua mbele ya Bayern.

 

Kutokana na balaa lake l;a majeruhi, wengi wanatilia shaka uwezekano wake wa kuwa uwanjani mara kwa mara.

 

Mara nyingi, staa huyo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mgongo.

Kama Gundogan ataendelea kuwa fiti, huenda kocha Guardiokla akaendelea kucheka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -