Friday, November 27, 2020

INDOMITABLE LIONS WALIVYOUNGURUMA TENA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LIBREVILLE, Gabon

MICHUANO ya Mataifa ya Afrika imemalizika Jumapili ya wiki iliyopita nchini Gabon na Cameroon ‘Indomitable Lions’ kunyakua taji lao la tano la michuano hiyo, ikiwa ni ushindi wao mkubwa.

Nyota wa Kombe la Dunia, Roger Milla, alitoa mchango mkubwa kwenye ubingwa wa mwaka 1984 na 1988, huku mataji mawili mfululizo 2000 na 2002 yakichagiwa na mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Inter Milan, Samuel Eto’o, ambaye alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne.

Lakini kikosi cha mwaka 2017 kilikuwa na mastaa wengi na hawakumtegemea mchezaji mmoja.

Kabla ya michuano hiyo, wachezaji wa Cameroon wenye majina makubwa kama Joel Matip anayekipiga Ligi Kuu England kwenye kikosi cha Liverpool, lakini kama ilivyokuwa kwa wengine kadhaa, beki huyo alikataa heshima hiyo ya kukipiga kwenye kikosi hicho kilichoingia fainali mwaka huu dhidi ya Misri na kubeba taji.

Matip na wenzake waliokataa kuichezea ‘Indomitable Lions’ sababu zao zilitokana na kutokuelewana kwao na shirikisho la soka la nchi yao na hivyo kugoma kuacha klabu zao barani Ulaya.

Hivyo kukosekana kwao ndiko kulizaa timu ambayo imekwenda Gabon, timu ambayo hata kulipotokea utata wa kutolipwa bonasi zao haikuharibu hamasa ya kizazi hicho cha Indomitable Lions.

Ubishani pekee uliotokea ni pale wachezaji hao walipopewa bonasi kwa kutinga nusu fainali, ambapo bonasi hiyo ilikuwa ndogo mara nne ukilinganisha na ile waliyopewa walipofuzu robo fainali, hiyo ilisababisha kocha wa kikosi hicho, Hugo Broos, kuwaunga mkono wachezaji wake.

“Hata bila ya fedha, bado tunacheza vizuri na hili ni muhimu sana, inaonyesha wachezaji hawako hapa kwa ajili ya fedha ila kwa ajili ya taifa lao,” alisema Broos akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari.

Kocha huyo alifanya kazi kubwa kwenye kibarua chake cha kwanza cha kufundisha timu ya taifa.

Si kuzungumza mambo sahihi kwa wakati sahihi pekee, pia kuwatengeneza wachezaji na kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyokuwa kwa mmoja wa wachezaji wake ambaye anachezea soka nchini Angola, lakini alicheza vizuri kimbinu na kimaamuzi.

Angalia jinsi alivyomwacha beki wa kulia Ernest Mabouka, ambaye alishindwa kucheza vizuri kwenye mechi ya kwanza, hata jinsi alivyobadilisha washambuliaji wake katika hatua ya makundi kwa jinsi alivyofikiria itafaa.

Kiini cha mafanikio ya kikosi hicho cha Cameroon kilikuwa ni safu yao ya ulinzi.

Akiwa na umri wa miaka 21, mlinda mlango Fabrice Ondoa, aliiokoa timu hiyo dakika za majeruhi dhidi ya wenyeji Gabon kwenye mechi ya mwisho ya makundi kwa kuokoa shuti lililokuwa linajaa nyavuni, pia alidaka penalti ya mwisho ya Senegal iliyopigwa na Sadio Mane kwenye mikwaju ya penalti.

Ukiachana na Ondoa ambaye hana nafasi hata kwenye kikosi B cha Seville nchini Hispania, pia mabeki wa kati, Adolphe Teikeu na Michael Ngadeu walicheza vizuri sana.

Walicheza kwa nidhamu sana, walikumbwa na kashikashi lakini utulivu wao na uwezo wao wa kucheza mipira ya angani na kuusoma mchezo, ingawa mara yao ya kwanza kucheza pamoja ilikuwa ni Septemba mwaka jana.

Waliilinda timu yao dhidi ya Senegal, kisha kazi ilikuwa kweye nusu fainali walipokutana na Ghana wakifanikiwa kushinda mabao 2-0.

Kwenye fainali, timu ambayo hamasa yake ilikuwa wazi kuonekana, walionyesha kupambana wakitoka nyuma kwa bao la kiungo wa Arsenal, Mohamed El Nenny, alilowafungia Misri dakika ya 23.

Misri hawajawahi kupoteza mechi kwenye michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika tangu mwaka 2004 wakicheza jumla ya mechi 25, lakini baada ya Nicolas Nkoulou kusawazisha, Vincent Aboubakar, alifanya maajabu zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, baada ya kuubetua mpira juu ya beki Ali Gabr na kufunga bao la ushindi.

Aliingizwa na kocha Broos kipindi cha pili, mabadiliko hayo yalizaa matunda, ikiwa ni mshambuliaji wa kwanza wa Cameroon kufunga michuano hiyo ya Gabon.

Lakini yote katika yote ni lazima umzungumzie nahodha Benjamin Moukandjo, nyota wa mchezo kwenye mechi hiyo ya fainali, pamoja na Christian Bassogog, mwenye umri wa miaka 21, aliyetangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo na aliyekuwa na mvuto kumtazama.

Miaka miwili iliyopita, winga huyo alikuwa akiichezea timu ya daraja la tatu nchini Marekani kabla ya kuhamia Denmark, ambako Broos alipewa ushauri kutoka kwa marafiki zake kuhusiana na mchezaji huyo na winga huyo wa kushoto kupata nafasi ya kwanza kuichezea timu ya taifa. Hiyo ilikuwa ni wiki 12 zilizopita.

Wamefanikiwa kuvuka changamoto mbalimbali na kunyakua taji lao la kwanza la Mataifa ya Afrika tangu mwaka 2002, mwonekano wa sura za furaha za Wacameroon baada ya filimbi ya mwisho zilitokana na mafanikio yao.

Wachezaji wengi walishindwa kuamini kama wamemaliza kazi waliyotumwa, baada ya fainali moja na mafanikio ya kunyakua taji ambalo walistahili.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -