Saturday, October 31, 2020

INGEKUWA VIPI? Kama Monaco wasingeuza nyota wao wasingeshikika Ulaya

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MONACO, Ufaransa

MWAKA 2013 klabu ya Monaco ilikuwa ikishiriki katika Ligi Daraja la Kwanza nchini Ufaransa, lakini miaka mitano mbele imekuwa moja ya timu bora Ulaya kwa kufanikiwa kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushinda Kombe la Ligi Kuu Ufaransa.

Uwekezaji uliofanywa katika kikosi chao ulikuwa mkubwa sana tena wakisajili nyota wenye viwango vya juu ambao walihusishwa kuelekea klabu kubwa Ulaya.

Lakini kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji kuliwafanya kushindwa kubaki na nyota wao, huku wakijikuta katika wakati wa kuanza mpya.

Kwa kiasi kikubwa uuzwaji wa wachezaji wa viwango vya juu umeibomoa klabu hiyo chini ya Leonardo Jardim ambaye aliitengeneza timu hiyo kuwazunguka nyota hao.

Kama wangefanikiwa kubakisha nyota wao ingekuwa timu moja ya tishio barani Ulaya na labda ingeandika historia kwa kushinda mataji makubwa Ulaya.

MLINDA MLANGO

Stephan Ruffier si jina kubwa katika soka lakini alikuwa mmoja wa makipa waliofanya kazi kubwa ndani ya kikosi cha Monaco kwa kuidakia timu hiyo michezo zaidi ya 130 akiwa nahodha.

Lakini aliondoka mwaka 2011 na kujiunga na St. Etienne ambako katika misimu yake saba ameonyesha kiwango cha juu.

SAFU YA ULINZI

Kwa wakati ule safu ya mabeki wa kati iliundwa na Aymen Abdennour, akisaidiana na Terence Kongolo, ambao walifanya kazi katika jezi ya Monaco.

Mwaka 2014, Abdennour alitimkia Marseille kwa dau la pauni milioni 20 ambako amekuwa beki tegemeo wa klabu hiyo iliyofungwa na Atletico Madrid katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mwaka 2017, Kongolo alifuata kwa kujiunga bure na klabu ya Huddersfield Town ya nchini England.

Monaco ilikuwa na mabeki wa pembeni wenye kasi wakati wa kushambulia na kukaba pindi timu hiyo iliposhambuliwa, huku mabeki hao wakichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mabao kutokana na kupiga krosi nyingi.

Upande wa kushoto walikuwa na Layvin Kurzawa ambaye hivi sasa anakipiga katika klabu ya PSG, wakati huo kushoto alikuwepo Benjamin Mendy aliyejiunga na Manchester City msimu uliopita.

SAFU YA KIUNGO

Katika maeneo ambayo Monaco walionekana kuwa tishio basi eneo la kiungo liliundwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Fabinho alikuwa akitumika kama kiungo wa ulinzi ndani ya timu hiyo, licha ya umahiri wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Hivi sasa kiungo huyo wa Brazil ni mchezaji wa Liverpool ambaye anasubiriwa kucheza mchezo wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho cha Jurgen Klopp.

Lakini katika safu ya kiungo cha ushambuliaji walisimama James Rodriguez na Bernado Silva kwa pamoja.

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, Rodriguez alisajiliwa na Real Madrid kabla ya kujiunga na klabu ya Bayern Munich hivi sasa.

Silva alijiunga na Manchester City msimu uliopita huku akiwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Pep Guardiola kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine.

SAFU YA USHAMBULIAJI

Licha ya kupita wachezaji wengi katika safu ya ushambuliaji, bado inaaminika uwepo wa Kylian Mbappe, Anthony Martial na Thomas Lemar ungekuwa na msaada mkubwa zaidi.

Mwaka 2014, Manchester United walivunja rekodi kwa kumsaji Martial akiwa mchezaji ghali zaidi kijana katika historia ya wakati huo.

Kabla ya usajili wa dirisha hili kufungwa, Lemar alijiunga na Atletico Madrid kwa dau la pauni milioni 54 ambako ameanza kuonyesha makali yake ndani ya kikosi hicho.

Upande wa Mbappe tangu msimu uliopita alipotolewa kwa mkopo katika klabu ya PSG, amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa Ufaransa huku akiwa tayari kujiunga na timu hiyo kwa ujumla.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -