Thursday, December 3, 2020

Ipi ni kombinesheni bora safu ya kiungo Arsenal?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

NANI na nani wanastahili kucheza safu ya kiungo kwenye kikosi cha Arsenal? Mchambuzi wa Sky Sports, Peter Smith anafafanua.

Safu ya kiungo ni moja ya eneo ambalo lilikuwa tatizo kwa klabu ya Arsenal, lakini kocha Arsene Wenger ana wachezaji wengi wa kuchagua kucheza kwenye safu hiyo. Santi Cazorla, Granit Xhaka, Francis Coquelin na Mohamed Elneny wote wanagombea nafasi hizo mbili. Swali ni kwamba, kombinesheni ipi ni bora?

Mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Middlesbrough, Coquelin na Elneny walichukua nafasi ya majeruhi Cazorla na Xhaka aliyekuwa na adhabu, ambapo walicheza katika mfumo anaoupenda Wenger wa 4-2-3-1.

Lakini walishindwa kusaidia Gunners kuibuka na ushindi, huku Petr Cech akifanya kazi ya ziada kuokoa mabao ya wazi mawili dhidi ya wageni hao.

Je, Wenger atafanyaje atakapokuwa na viungo wote wanne wakiwa wazima? Mtandao wa Sky Sports umejaribu kuangalia kombenesheni gani atakayotumia.

 

Elneny na Coquelin

Jumamosi ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Wenger kumpanga Elneny pamoja na Coquelin tangu alipofanya hivyo kwenye mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu England, ambayo walipoteza kwa kichapo cha mabao 4-3 dhidi ya Liverpool.

Katika mechi hiyo ya kwanza, Elneny alipumzishwa dakika ya 67 baada ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji wa Liverpool. Hakufanikiwa kupora hata mpira mmoja na kusaidia timu yake kumiliki mpira mara tatu pekee.

Kwa mara nyingine tena dhidi ya Middlesbrough alitolewa dakika ya 74 na nafasi yake kuchukuliwa na Alex Oxlade-Chamberlain, Wenger alipotaka kuongeza kasi ya mashambulizi kwenye kikosi chake.

 

MECHI WALIZOCHEZA

Arsenal 4-3 Liverpool

Arsenal 0-0 Middlesbrough

 

Cazorla na Coquelin

Hii ndio kombinesheni maarufu katika safu ya kiungo ya Arsenal ambayo imeshinda mechi nne kati ya tano. Ukiwemo ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea, ambapo Coquelin alitolewa nje baada ya kupata majeraha kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza 2-0, pia Gunners walishinda dhidi ya Southampton, wakati Cazorla akipiga penalti dakika za majeruhi.

Wenger aliwaamini Cazorla na Coquelin dhidi ya Paris St-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo walitoka sare ya bao 1-1. Mechi nyingine ambayo kombinesheni hiyo imeibuka na ushindi ni dhidi ya Hull na Ludogorets, ambapo Cazorla alitoa pasi ya bao kabla ya kutolewa baada ya kupata majeraha.

 

MECHI WALIZOCHEZA

Arsenal 2-1 Southampton

PSG 1-1 Arsenal

Hull 1-4 Arsenal

Arsenal 3-0 Chelsea

Arsenal 6-0 Ludogorets

 

 

Xhaka na Cazorla

Kombinesheni nyingine maarufu ni Xhaka na Cazorla. Nyota hao wa Uswisi na Hispania wameshinda mechi nne kati ya nne walizoanza pamoja, ikiwemo ushindi wa ugenini dhidi ya Watford na Burnley kwenye Ligi Kuu England.

Wawili hao walianza pamoja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Basel na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Katika mchezo mwingine dhidi ya Swansea, ambao walishinda mabao 3-2, Xhaka alitolewa dakika ya 70.

Xhaka aliingia dakika ya 32 akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Chelsea, ambapo Arsenal walishinda mabao 3-0, ambapo alicheza dakika zote za mechi zilizobakia pamoja na Cazorla.

 

Mechi walizocheza

Watford 1-3 Arsenal

Arsenal 2-0 Basel

Burnley 0-1 Arsenal

Arsenal 3-2 Swansea

 

 

 

Elneny na Xhaka

Elneny na Xhaka wamecheza pamoja mara moja msimu huu. Xhaka alifunga bao la kuongoza katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nottingham Forest kwenye mechi ya Kombe la Ligi (EFL Cup).

 

MECHI WALIZOCHEZA

Nottingham 0-4 Arsenal

 

 

Coquelin na Xhaka

Coquelin na Xhaka walicheza pamoja katika mchezo wa sare ya 0-0 dhidi ya Leicester mwanzoni mwa Agosti, ambapo Cazorla alicheza namba 10.

Waliweza kujilinda vizuri kabla ya Xhaka kutolewa dakika ya 73 na kuingia Jack Wilshere. Coquelin alipora mipira mara tano na kuingilia pasi tano, wakati Xhaka akiweza kumiliki mipira mara tisa ikiwa ni zaidi ya wenzake wote.

 

MECHI WALIZOCHEZA

Arsenal 0-0 Leicester

 

Elneny na Cazorla

Wenger bado hajawahi kuwachezesha Elneny na Cazorla kwenye mechi yoyote msimu huu.

 

Kombinesheni nyingine

Moja ya kombinesheni nyingine ambayo Wenger amewahi kuipanga ni ile ya zaidi ya viungo wake wawili wa kati kwa pamoja. Alifanya hivyo katika mechi dhidi ya Leicester, ambapo Cazorla alicheza namba 10, huku Elneny akicheza namba nane na Coquelin akiwa mkabaji.

Wenger pia amewahi kumchezesha Alex Oxlade-Chamberlain kwenye safu ya kiungo, ambapo mchezaji huyo wa England aliingia dakika za majeruhi akichukua nafasi ya Elneny dhidi ya Middlesbrough wakati Arsenal wakisaka ushindi dakika za majeruhi, lakini pia kuna kombinesheni nyingine itaongezeka atakaporejea kiungo Aaron Ramsey anayesumbuliwa na majeraha kwa sasa.

Hitimisho

Kutokana na ushindi, mabao na pasi za mabao ambazo Arsenal wameweza kuzipata wakiwa na Cazorla, bila shaka jina la nyota huyo wa Hispania hasa akiwa fiti ndio litakuwa namba moja kwenye karatasi ya kikosi cha Wenger. Kocha huyo alimsifia mchezaji huyo akizungumzia kukosekana kwake kwenye mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akiulizwa kama Arsenal walikuwa na pengo kwa kukosa Cazorla dhidi ya Middlesbrough, Wenger, alisema: “Ndio, siku zote asipokuwemo anakuwa na pengo. Kutoka nafasi ya kiungo hadi kwenye robo ya mwisho ya uwanja, kutokana na pasi zake kuwa za haraka na uhaikika.”

Kazi ni nani atacheza na Cazorla, mkali wa pasi Elneny, anayekaba kwa nguvu Xhaka ambaye ameonyesha pia uwezo wake wa kufunga akiwa mbali na mtaalamu wa kuvuruga mambo, Coquelin.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -