Wednesday, October 28, 2020

Ipo hatari ya wachezaji kurudia utamaduni wa kuvuta sigara bila woga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MWANDISHI WETU NA MITANDAO

HISTORIA ya tumbaku na ya mpira wa miguu zimekuwa zikiambatana kwa muda mrefu, iwe ni wachezaji au makocha kuvuta sigara. Hawa huwa ni wavutaji wachanga na wale wanaweza kuwa wavutaji wazoefu.

Utamaduni unaweza kuwa umebadilika kwa kiasi fulani, lakini kiungo wa PSG, Marco Verratti, alikuwa akivuta sigara wiki iliyopita na ishu hiyo ilitikisa vyombo vya habari kwani tayari Muitaliano huyo alishagombana na kocha wake, Unai Emery, kisa kikiwa ni kufanyiwa mabadiliko wakati wa mechi.

Jambo hili huwa linazungumziwa kila kukicha kwamba uvutaji wa sigara si mzuri kwa wachezaji ambao wanategemewa kwa kiasi kikubwa kuonesha kiwango cha hali ya juu na maoni ya wadau yamebadili tabia hiyo katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita.

Kabla ya sheria ya kupinga uvutaji wa sigara hadharani au maeneo ya kazi, wachezaji mastaa kama Alfredo di Stefano walikuwa na uwezo wa kuvuta sigara hata kama timu ikiwa ziarani, halikuwa jambo la ajabu kwao.

Hakukuwa na eneo lililokuwa na onyo la kutovuta sigara, si kwenye mikutano na waandishi wa habari, benchi la ufundi wakati wa mechi, hata katika sehemu maalumu wanapokaa mabosi wa klabu kwa ajili ya kuangalia mechi. Makocha maarufu kama vile Luis Aragones, Johan Cruyff, Javier Clemente, Cesar Luis Menotti, Leo Beenhakker na Carlo Ancelotti waliwahi kuvuta sigara kwa nyakati tofauti.

Wachezaji pia walikuwa hawalaumiwi pindi wanapofanya kitendo hicho, Garrincha, Socrates, Frank Rijkaard na Robert Prosinecki waliwahi kuonekana ‘wakipiga pafu’.

“Mara nyingi huwa sivuti (sigara) mpaka nikipata hamu lakini watu husahau hilo pindi wanionapo nikikimbia uwanjani,” alisema mlinzi wa kati wa Barcelona, Jeremy Mathieu, ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaokiri kutumia sigara.

Wapo wachezaji wengine wa kisasa ambao waliwahi kukutwa wakivuta kama vile Fabio Coentrao, Kevin Prince Boateng na mlinda mlango wa zamani wa Arsenal, Wojciech Szczesny.

“Radja Nainggolan anavuta sana sigara ndio maana huwa namtafutia chumba chake mwenyewe kwenye hoteli,” alisema kocha wa zamani wa Ubelgiji, Marc Wilmots, ambaye alionekana kukubaliana na tabia ya mmoja wa mastaa wake.

Vitu vingi vimebadilika hivi sasa katika ulimwengu wa soka na kile kipindi cha wachezaji kuvuta sigara bila kuzuiwa kimepita, lakini kwa inavyoonekana ni kama tabia hiyo inajirudia tena na madhara yake ni kwamba Verratti na wengineo wataingia tena katika mkumbo huo hatari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -