Wednesday, October 28, 2020

JAMIL HAMID KHAN, BINGWA MBIO ZA MAGARI NCHINI ANAYEKIMBIZANA NA KASI YA RAIS MAGUFULI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SHARIFA MMASI

BADO Watanzania wengi wana imani na uwapo wa jina la Jamil Khan (38), kwenye orodha ya madereva mahiri wanaotegemewa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa hapo baadaye.

Kutegemewa huko kunatokana na kuwahi kuibuka kidedea katika mashindano mbalimbali ya taifa ya mchezo huo, yakiwamo yale yaliyowahi kumalizika Agosti 16 mwaka juzi, mjini Bagamoyo yaliyowashirikisha jumla ya madereva 20 kutoka mikoa tofauti hapa nchini.

Mbali na hayo, mwaka jana Khan aliibuka kidedea katika mashindano ya ndani yaliyofanyika tena mjini Bagamoyo na kufanikiwa kuongoza awamu tisa zilizokuwa zikipiganiwa na madereva mbalimbali walioshiriki.

BINGWA lilifanya mahojiano na Khan kutaka kujua mengi zaidi kuhusu maisha yake ya kimichezo pamoja na changamoto mbalimbali zinazoendelea kuutafuna mchezo huo, kumfanya kukosa mashabiki  wengi kama ilivyo soka.

Khan, anasema siri kubwa inayomuweka kileleni katika kila mashindano  ni umakini awapo katika chombo cha moto na kuwa muangalifu barabarani kama njia mojawapo ya kulinda na kutunza miundo mbinu ya nchi.

“Niwapo katika chombo cha moto huwa nakuwa makini sana, uangalifu huo unazidi mara mbili pale ninapokuwa katika mashindano yoyote yale kwa kutuliza akili yangu na kufanya kile kinachonihusu katika mudao huo.

“Wakati nikituliza akili ya kuendesha gari kwa kucheza na muda ili niibuke bingwa, huwa naendesha kwa umakini kulinda uharibufu wa miundo mbinu ambayo naamini ni msaada mkubwa kwetu sisi madereva hasa katika mchezo wetu huu wa mbio za magari,” anasema Khan.

Khan anasema, mbinu zote anazotumia kupata ubingwa katika mashindano alipewa na baba yake mzazi akiwa na umri wa miaka 18, kipindi ambacho anaandaliwa kuwa dereva bora wa mchezo wa magari, ambapo mzazi huyo alikuwa ni mdau wa mchezo wa magari kipindi cha nyuma, huko nchini India.

“Mafanikio yangu katika mchezo huu yanatokana na baba yangu mzazi ambaye ndiye alinijenga katika misingi imara ya kuwa dereva bora wa mchezo wa magari hadi hivi sasa.

“Namshukuru sana kwakweli kwani bila yeye sidhani kama leo ningejulikana hapa nchini kwangu hivyo sinabudi kufuata kile alichonielekeza ili niendeleze ushindani baina ya nchi yangu ya Tanzania na nyenginezo,” anasema Khan.

Akizungumzia changamoto, Khan anasema mchezo huo unakila aina ya changamoto ikiwemo ushindani wanchi mbalimbali pindi wanapokutana katika mashindano makubwa kwani kila dereva anakuja na mbinu za kutaka kuwa bingwa wa magari duniani.

Ukiachana na changamoto hiyo, anasema mbio za magari zinahitaji wadhamini wengi ndio maana Tanzania kuna madereva wenye viwango lakini wanashindwa kufikia malengo kutokana na kukosa watu wa kuwafadhili ili watimize ndoto zao.

Khan anasema, kwa sasa ndoto zake kubwa katika mchezo huo, ni kuja kuwa dereva bora wa mbio za magari duniani, pamoja na kuwa mwalimu wa madereva ili mchezo huo uzidi kukua zaidi ya hapo.

“Wakati naanza kufundishwa huu mchezo sikuwa na mawazo ya kuja kuwa dereva bora nchini lakini kadiri siku zilivyosonga mbele mafanikio yalijitokeza na kufikia hapa nilipo.

“Kuwa bingwa wa taifa bado hakuja timiza ndoto zangu kwani hata mimi niliandaliwa na mzazi wangu mpaka kufikia hapa, hivyo sina budi kuhakikisha napongeza jitihada ili niwe bingwa wadunia,” anasema Khan.

Akitoa ushauri kwa vijana wenye nia ya kujikita katika mchezo huo, Khan anawataka wajiunge katika klabu mbalimbali za hapa nchini na sio kujaribu kuendesha magari bila kupata mafunzo kuepusha kupoteza uhai wao na hata uharibufu wa miundo mbinu.

“Siwaungi mkono kabisa vijana wanaopenda kujaribu huu mchezo bila ya kujifunza kupitia klabu zetu za hapa nyumbani na waalimu wenye viwango, hii inaonyesha wazi kwamba madhara yake ni makubwa na nirahisi kusababisha uharibifu wa miundombinu ambayo tunaitegemea kuja kuiletea sifa nchi yetu,” amesema Khan.

Khan anawataka vijana kushiriki mchezo huo pasina kuwa na woga wowote huku pia akitoa wito kwa wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kuutangaza mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -