Saturday, October 31, 2020

Jay Dee kukata ngebe za Kiba tuzo za EATV?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

TUZO za muziki na filamu zilizoandaliwa na EATV zimeanza kupamba moto baada ya wasanii kuanza kujigamba kila mmoja kumzidi mwenzake.

Tayari wasanii wameanza kuomba kura kwa ajili ya kuweza kuibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro hicho kitakachofikia tamati Desemba 10 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Wasanii mbalimbali wameanza kukabana koo kwenye kuomba kura katika vipengele mbalimbali, ambapo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, amejikuta kwenye ushindani mkubwa na mwanadada Lady Jay Dee.

Jay Dee ambaye ni mkongwe wa muziki, amejikuta akikabana koo na Ali Kiba baada ya kuingia kwenye vipengele vinne kila mmoja.

Jay Dee ambaye ana rekodi ya kuzoa tuzo nyingi toka mwaka 2001 hadi 2004, kwenye tuzo hizo za EATV kila kipengele yupo na Ali Kiba.

Msanii huyo ambaye amewahi kushinda tuzo mbalimbali kama za M-Nets akiwa kama msanii bora mwa kike mwaka 2001, Kill Award (Video Bora ya Machozi 2002), Channel O (Video Bora ya Machozi 2003), Tanzania Youth Award 2003 (Wimbo Bora wa Usiuseme Moyo).

Tuzo nyingine ambazo Jay Dee ameshinda ni ile ya Albamu Bora kupitia tuzo za Kill Award 2005, Wimbo Bora wa kushirikiana Afrika katika tuzo za Chanel O (Wimbo wa Makini).

Wimbo wa Distance mwaka 2005 ulishinda tuzo za Chanel O na BBC Award, huku mwaka 2006 na mwaka 2007 akiibuka Msanii Bora wa Kike kwenye tuzo za Uganda Pearl of Afrika.

Jay Dee hakuishia hapo, mwaka 2008 alishinda tena kwenye tuzo za Uganda Pearl of Afrika, huku mwaka 2009 akifanya kweli katika tuzo za Kenya za Kisima Award kupitia wimbo wake wa Anitha kabla ya mwaka huo huo kuibuka kidedea tena kwenye tuzo za Kill Music Awards.

Lady Jay Dee ‘Komando’ ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Ndindindi, mwaka 2010, 2011, 2012, 2013, 2014 alitikisa tena kwenye tuzo za Kill Music Awards.

Mwaka 20014 Jay Dee alishinda kwenye tuzo za Watu, huku mwaka huo huo akiweka rekodi ya kutwaa tuzo za AFRIMMA.

Hivyo ni wazi msanii huyo atampa ushindani mkubwa Ali Kiba ambaye amewahi kujizolea tuzo mbalimbali tangu alipoanza muziki.

Tunajua Kiba alianza muziki kitambo ila atakumbukwa zaidi mwaka 2007 alipofanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela’ ambayo ilivuma sana na kusababisha albamu hiyo kuuzika zaidi sokoni albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2007 Afrika Mashariki.

Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Afrika Mashariki na kumtangaza zaidi kwa muda mfupi kupitia vibao vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu.

Albamu hiyo ilimpa mwanga ambapo alifanikiwa kuweka rekodi ya kufanya kazi na R Kelly mwaka 2010.

Alipata dili la One 8 na kufanikiwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa akiwemo R Kelly na wengine saba kutoka Afrika.

Alipokutana na R Kelly alimsifu kwamba ana sauti nzuri na ya kipekee hivyo kupendekeza aanze kuimba katika singo ya pamoja ya Hands Across the World.

Wimbo huo ulimfanya kumrudisha kwenye chati na kuweza kuzoa tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya BEFFTA Londan Award kama Best International Artists ‘ACT’ na kumshinda mwanamuziki 2 Face Idibia, pia alifanikiwa kurudi na tuzo ya Sexiest Male Artist.

Hivyo uwepo wake kwenye tuzo za EATV, ni wazi atakuwa na ushindani mkubwa na Jay Dee ambaye naye ana sifa ya kufanya vema.

Kwenye tuzo hizo, Kiba na Jay Dee wapo kwenye vipengele vya Video Bora ambapo zinashindana ni Ndindindi, Aje, Namjua, Don’t Bother na Njogereza.

Wimbo bora wa mwaka, Don’t Bother ya Joh Makini, Ndindindi, Kamatia chini, Aje na Moyo Mashine, huku Mwanamuziki Bora wa Kiume wakiwa ni G Nako, Shetta, Ben Pol, Mwana FA na Ali Kiba.

Mwanamuziki Bora wa Kike ni Lilian Mbabazi, Ruby, Linah, Vanessa Mdee na Jay Dee.

Vipengele vingine vinavyowaniwa kwenye tuzo hizo ni Mwigizaji Bora wa Kiume, Said Ally, Meya Shabani, Daudi Michael, Salim Ahmedy na Doto Hussein, huku Mwigizaji wa Kike wakiwa ni Chuchu Hans, Khadija Ali, Kajala Masanja na Rachel Bitulo.

Mwanamuziki Bora Chipukizi wanaoshindana wakiwa ni Manfongo, Feza Kessy, Rucky Baby, Mayunga na Bright, Filamu Bora ya Mwaka ni Hii ni Laana, Nimekosea Wapi, Safari ya Gwaru, Mfadhili Wangu na Facebook Profile.

Kundi Bora la Mwaka ni Wakali Wao, Navy Kenzo, Mashauzi Classic, Team Mistari na Sauti Sol.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -