Thursday, December 3, 2020

JAY JOY OKOCHA: KIPAJI CHA SOKA KUTOKA AFRIKA KILICHOITIKISA ULAYA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU


KWA mpenzi yeyote wa soka duniani, ikiwamo hapa Tanzania, ukimtaka akutajie jina la mchezaji kutoka Afrika aliyewatikisa Wazungu kutokana na kuwa na kipaji cha kipekee, hakuna ubishi jina litakalotajwa na wengi litakuwa ni la Augustine Azuka, maarufu jkama Jay-Jay Okocha.

Huyu ni gwiji mwingine ambaye historia yake inaanzia mwaka 1973 huko Enugu, nchini Nigeria.

Kama walivyo vijana wengi wa kiafrika, gwiji huyu naye alianza kucheza soka mitaani huko kwao kabla kipaji chake kugunduliwa.

Wazazi wake ni wenyeji kutoka katika jimbo la Ogwashi-Uku nchini Nigeria, mwanzoni jina la Jay Jay lilikuwa ni la kaka yake aliyefahamika kwa jina la James, lakini mara baada ya gwiji huyo kuanza kuonyesha kipaji kikubwa cha soka katika klabu yake ya awali ya nyumbani kwao ya Enugu Rangers jina hilo likahamia kwake.

Gwiji huyo enzi zake alikuwa ni moto wa kuotea mbali kuanzia katika bara hili la Afrika mpaka Ulaya, alifahamika kwa wengi kwa uwezo wake mkubwa kufunga pamoja na upigaji wa pasi za mwisho.

Mara baada ya kutamba kwa mda nchini kwao katika klabu ya Enugu Ranger, mwaka 1990 alianza kucheza soka la uhakika mara baada ya kujiunga na moja ya timu ya nchini Ugerumani mwaka 1991.
Katika moja ya mahojiano na Shirika la Hababari la BBC, aliwahi kukaririwa akisema kuwa mwaka huo wa 1990 alikwenda likizo Ujerumani Magaribi kumtembelea rafiki yake Binebi Numa aliyekuwa akicheza nchini humo katika timu ya Ligi Daraja la Pili.

Mara baada ya kufika nchini humo siku moja alimuomba rafiki yake kumuombea nafasi ya kufanya mazoezi kwa kocha aliyekuwa akicheza katika klabu ya Borussia Neunkirchen mara baada ya kuruhusiwa kufanya mazoezi alionyesha vitu adimu kiasi cha kila mmoja kumkubali.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya mazoezi kumalizika, kocha aliamua kumualika kwa ajili ya siku inayofuata baada ya kufurahishwa na kiwango chake na kwamba baada ya muda, aliingia mkataba na klabu hiyo.

Mwaka mmoja baada ya kuitumikia klabu hiyo, aliamua kuhamia katika klabu ya FC Saarbrucken ambako hakudumu kwani baadaye alijiunga na klabu ya Eintracht Franfurt iliyokuwa ikishiriki Ligi ya Bundesliga.
Na mara alipojiunga na klabu hiyo, alikutana na magwiji wengine kama Tony Yeboah na Thomas Doll ambaye kwa sasa ni marehemu.
Akiwa na klabu hiyo, gwiji huyo alikuwa ni moto wa kuotea mbali na mpaka leo wapenzi wengi wa soka bado wanamkumbuka kwa umahiri wake.

Moja ya kumbukumbu ambayo bado inakumbukwa hadi leo ni bao zuri alilofunga katika mchezo kati ya timu yake na Karlruhe ambapo aliwalamba chenga mabeki wote kabla ya kumfikia kipa Oliver Kahn na kufunga bao.

Bao hilo lilipigiwa kura na kuchaguliwa kuwa bao la mwaka na vyombo mbali mbali vya nchini humo, huo ukiwa ni mwaka 1993.

Mara baada ya kutamba na klabu hiyo, uhusiano wake na kocha Jupp Heynkes haukuwa mzuri kwa upande wake na wachezaji wenzake.

Mambo yaliendelea kwenda kombo na mwaka 1995, Okocha, Yeboah na mchezaji mwenzao Maurizio, waliingia katika uhusiano mbaya na meneja wao.

Mwisho wa siku, Yeboah na mwenzake Maurizio waliamua kuachana na klabu hiyo na kuhamia England, lakini Okocha alibakia ndani ya klabu hadi mwisho wa msimu.

Mara baada ya msimu kumalizika, kwa bahati mbaya klabu hiyo ilishuka hadi daraja la pili, ndipo Okocha akahamia nchini Uturuki katika klabu ya Fenerbahce.

Gwiji huyo alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni moja baada ya klabu yake ya nchini Ujerumani kushuka hadi daraja la pili.

Alikaa na klabu hiyo kwa misimu miwili na kufanikiwa kucheza mechi 60 na kufunga mabao 30, mengi yakitokana na mipira iliyokufa.

Mwaka 1998, gwiji huyo alijiunga na Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa paundi milioni 14, uhamisho uliomfanya kuwa mchezaji ghali kutoka Bara la Afrika kwa wakati huo.

Aliitumikia klabu hiyo kwa misimu minne na kucheza mechi 84 na kufunga mabao 12, hapo ndipo walipokutana na mchawi mwingine wa soka duniani kutoka nchini Brazil, Ronaldinho Gaucho.

Hata hivyo, gwiji huyo akiwa ndani ya klabu hiyo, alianza kuandamwa na majeraha yaliyoanza kumuweka katika wakati mgumu.

Mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwaka 2002, aliamua kuhamia England na kujiunga na Bolton Wanderers kwa uhamisho huru.

Alipojiunga na klabu hiyo aliikuta ikiwa katika harakati za kujinasua kushuka daraja na kufanikiwa kuinusuru kwa kufunga mabao saba, huku akiwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.

Msimu wa 2009, alikuwa kwenye kiwango kikubwa na uongozi kuamua kumpa majukumu ya kuwaongoza wenzake (Captain) baada ya kustafu kwa Guoni Bergsson.

Akiwa kama kiongozi ndani ya timu, aliiwezesha kufikia hatua ya fainali ya kombe la ligi, huku wakicheza soka la nguvu kiasi cha kuwa gumzo.

Hadi kufikia msimu wa 2006, alianza kuingia katika mikwaruzo na baadhi ya viongozi ndani ya klabu kitendo kilichosababisha kuvuliwa unahodha.

Kufikia mwisho wa mkataba wake, alikataa kuongezewa mwaka mmoja zaidi ili aweze kuhamia katika ligi ya Qatar.

Hali iliendelea kuwa mbaya katika klabu hiyo na kusababisha timu hiyo kushuka daraja mwaka 2012, hivyo mkali huyo kutimkia Qatar.

Mara baada ya kucheza kwa msimu mmoja katika ligi ya Qatar, gwiji huyu aliamua kurudi England na kujiunga na Hull City kwa uhamisho huru, huo ukiwa ni mwaka 2007.

Kwenye ngazi ya timu ya taifa, gwiji huyu alikuwamo katika kikosi kuanzia mwaka 1993-2006 na kufanikiwa kufunga mabao 14 ndani ya kikosi hicho.

Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha nchi yake kupata medhali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki Atlanta 1996 na aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Mataifa Huru ya Afrika 1994 na kombe la Asia, Afrika mwaka 1995.

Pamoja na kuwa miongoni mwa mastaa wakubwa katika bara hili, lakini gwiji huyo katika kipindi chote cha uchezaji wake, hakuwahi kushinda na kuwa mchezaji Bora wa Afrika.

Tuzo pekee alizowahi kupata wakati wa uchezaji wake ni kuwa mchezaji bora wa nchini kwao Nigeria kwa miaka saba na Mchezaji Bora wa BBC kutoka Bara la Afrika kuanzia mwaka 2003 na 2004.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -