Saturday, November 28, 2020

JENNIFER MGENDI KWA NDIZI NA SATO HAJAMBO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA BEATRICE KAIZA


KHERI ya mwaka mpya 2017 wapenzi wasomaji wa ukurasa huu wa Jiachie na staa wako, kwanza kabisa tunapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa pumzi hadi leo hii, pia tuwaombee wale wote walioshindwa kuuona mwaka 2017 kwa maana wametangulia mbele ya haki basi tuseme kwa pamoja amina.

Staa wetu aliyefanikiwa kutufunguliwa mwaka mpya wa 2017 ni Jenifer Mgendi, huyu ni mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za njili.

Kama tulivyokuahidi ndivyo tulivyofanya kwani Jiachie na Staa wako ilimsaka na ilipompata ilimfikishia maswali yenu ambayo aliyajibu kama ifuatavyo.

Swali: Eva Mpanju wa Boko, Dar es Salaam, hadi sasa ni faida gani umezipata kupitia tasnia ya muziki wa injili?

Jibu: Nimeweza kumujua Mungu na kuweza kutoa elimu na mafundisho kuhusu Yesu, kutumikia kazi za Mungu, pia nimejulikana kila kona ya nchi, watu wengi wanazipenda kazi zangu  kwa kupata ujumbe wa kumsifu Mungu kwa njia ya mashairi yangu.

Pongezi: Erick Samweli wa Mbezi Beach, Dar es Salaam, hongera dada Jennifer kwa kazi zuri.

Jibu: Asante sana Erick, Mungu akubariki.

Pongezi: Mwajuma wa Mikanjuni Mbeya, dada Jennifer napenda sana wimbo wa Nalia, kwani unanifariji.

Jibu: Asante Mwajuma kwa kupenda kazi zangu.

Swali: Koku John wa Kawe, Dar es Salaam. Naomba kujua uliaza kuimba mwaka gani?

Jibu: Mwaka 1995 ndio nilianza kuimba muziki wa injili.

Swali: Mzee Ally wa Kimara, Dar es Salaam. Kitu gani kilikusukuma hadi ukaamua kuimba nyimbo za injili na si Bongo Fleva.

Jibu: Kilichonisukuma kuimba muziki wa injili ni imani niliyonayo, nisingeweza kuimba muziki wa kidunia  zaidi ya kumsifu Mungu kwani ni sehemu ya maisha yangu. Yesu ndiye  aliyejaa moyoni mwangu  na si mwingine.

Swali: Estaline wa Tabora, chakula gani unapenda kula dada Jennifer.

Jibu: Napenda kula ndizi za Bukoba za kuponda na samaki sato.

Swali: Emanuel Kiama wa Dar es Salam, dada Jennifer nataka kujua kwanini kwenye muziki wa injili hakuna tuzo zinazoandaliwa kama kwenye Bongo Fleva?

Jibu: Kuhusu tuzo sijui chochote kama wanatoa au hawatoi, sina uhakika na suala hilo.

Swali: Elizabeth Thomas wa Morogoro, unawapa ushauri gani wasanii wanaovaa mavazi yanayoonyesha sehemu kubwa ya miili yao hasa wa muziki wa kidunia.

Jibu: Maombi ndio yanaweza kuwaokoa wasanii, kwa upande wetu sisi watumishi wajibu wetu ni kuwaombea, kifupi  usanii si lazima kuvaa nguo ambazo huwezi kuwa huru mbele ya macho ya watu.

Swali: Elizabeth wa Dar es Salaam, mashabiki wako tutegemee nini mwaka huu 2017.

Jibu: Kwanza kabisa nawapenda sana mashabiki wangu, kwani bila sapoti yao  katika kazi zangu za uimbaji wa nyimbo za injili nisingekuwa Jennifer huyu anayefahamika kila kona ya nchi.

Zaidi ya hapo, mashabiki wangu watarajie kazi nzuri zaidi mwaka 2017 kuna filamu nyingi zitatoka hivyo wakae mkao wa kula.

Swali: Ester Tesha umefanikiwa kupata watoto wangapi hadi sasa.

Jibu: Nimebarikiwa kupata watoto watatu.

Swali: Anold wa Dar es Salaam, unawapa ushauri gani wasanii wachanga ambao wanatamani kutimiza ndoto zao na kuwa kama wewe.

Jibu: Ushauri wangu kwa wasanii wachanga wafanye kazi kwa bidii kwani kwa Mungu hakuna linaloshindikana, pia wasikate tamaa.

Ushauri: Anjela wa Dodoma, naomba ufanye kazi na wasanii wa Bongo Fleva ili kuleta ladha tofauti katika tasnia ya injili.

Jibu: Asante kwa ushauri mzuri na Mungu akubariki, ni kitu kizuri nitakifanyia kazi kwa miaka ijayo.

Swali: Chenjeray wa Kimara-Temboni, Dar es Salaam. Unavutiwa zaidi na kazi za  wasanii gani wa hapa nyumbani kwa  upande wa Bongo Fleva.

Jibu: Nawapenda wote wanaoimba nyimbo zenye kubadilisha mitazamo ya watu waweze kuishi maisha yenye  kumpendeza Mungu.

Swali: Winfrida wa Mwanza, kuna ukweli wowote kuhusu tetesi za wasanii wa injili kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Jibu: Kwa upande wangu sijui chochote na kama wapo wanaotumia dawa za kulevya na kujifanya ni watu wa Mungu ipo siku Mungu atawatumbua.

Hawa ni baadhi ya mashabiki waliojitokeza kumuuliza maswali, kumpa ushauri na pongezi msanii wa injili, Jennifer Mgendi.

Katika toleo lijalo tunamleta kwenu mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Kassim Mganga maarufu kama Tajiri wa mapenzi.

Staa huyu amewahi kutamba na nyimbo nyingi  ikiwamo ‘Awena’, Nakuimbia, ‘Haiwezekani’, ‘I love you’, ‘Manuari’ na Nafsi Nyonge.

Tumia fursa hii kumuuliza maswali ili kukata kiu yako lakini pia waweza kumpa ushauri kwa kutuma sms kupitia namba ya simu iliyoko hapo juu na majibu yatapatikana hapa hapa katika toleo la Jumanne ya wiki ijayo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -