Tuesday, November 24, 2020

JEURI YA ALEXIS SANCHEZ INAVYOIPASUA ARSENAL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

KITU pekee mashabiki wa Arsenal wanachohitaji kukisikia kutoka kwa Arsene Wenger, hivi sasa ni sababu za kwanini alimweka benchi, Alexis Sanchez, kwenye pambano dhidi ya Liverpool.

Imewezekana vipi mchezaji anayeongoza kwa ufungaji ndani ya klabu, nyota wa kikosi akawekwa benchi kwenye mchezo muhimu namna ile?

Swali hili limepata majibu.

Mtandao wa Telegraph, umeripoti kuwa siku moja kabla ya mechi ya Liverpool, Alexis Sanchez, alisusa kufanya mazoezi na kutoka uwanjani baada ya kugombana na mmoja wa wachezaji wenzake.

Tukio hili linatajwa kumkera sana Arsene Wenger ambaye alichukua uamuzi wa kumwondoa kwenye kikosi cha kwanza, Arsenal ilipolala bao 3-1 dhidi ya Liverpool, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Anfield.

Baada ya kichapo hicho, Wenger alilalamikiwa sana kwa kosa la kutomwanzisha Sanchez, lakini mwenyewe alisema alifanya maamuzi hayo kwa sababu za kiufundi.

Hivi sasa tayari taarifa zimeanza kuenea kuwa Sanchez ameandika barua ya kuomba kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huku sababu ikitajwa ni kukerwa na kitendo cha kuwekwa benchi.

Jarida la Telegraph limesema kuwa hali ya kikosi cha Arsenal haikuwa sawa baada ya ugomvi huo uliotokea wakiwa mazoezini, hivyo kuwavuruga kwenye maandalizi ya kuwakabili Liverpool.

Inaripotiwa kuwa wachezaji wa Arsenal, hawakufurahishwa na kitendo cha nyota huyo wa kimataifa kutoka Chile, aliyetupia mabao 17 mpaka sasa kujiona mtu muhimu zaidi ndani ya klabu.

Sanchez amekuwa na tabia ya kuwalaumu wachezaji wenzake wanapokuwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo pindi Arsenal wanapopoteza mchezo.

Tabia hii ya kujiona kiongozi kwa wengine na kutengeneza umuhimu ndani ya kikosi, ndiyo sababu ya Wenger kumweka benchi na si mambo ya kiufundi kama alivyosema mbele ya waandishi.

Na pamoja na wachambuzi wengi wa soka nchini England kumponda Wenger kwa maamuzi hayo, bado kocha huyo amekuwa akipewa sapoti kubwa na wachezaji kwa kumwondoa Sanchez kwenye kikosi cha kwanza.

Ikumbukwe kwenye pambano la Arsenal dhidi ya AFC Bournemouth, Sanchez alitoka uwanjani kwa hasira na kuvua glovu zake na kuzitupa chini, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Mtiririko wa matukio haya ni wazi yalitengeneza ishara kuwa Sanchez anataka kuitema Arsenal, hivyo alichokifanya Wenger kumweka benchi ulikuwa uamuzi wa kujenga umoja ndani ya klabu.

Lakini Wenger hivi sasa anakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuchagua kumpanga Sanchez kwenye kikosi cha kwanza au kumwondoa tena, pindi washika mitutu hao wa Jiji la London, watakapoikaribisha Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo wa kwanza nchini Ujerumani, Arsenal walipoteza kwa mabao 5-1, hivyo watalazimika kupambana kufa au kupona ili waweze kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, wakiwa katika dimba la Emirates.

Je, Wenger atajilipua na kuendelea na msimamo wake mbele ya Sanchez? Je, wachezaji wenzake wataridhika na kumpa ushirikiano pindi nyota huyo wa Chile atakaporejeshwa kwenye kikosi cha kwanza?

Nyota mwingine wa klabu hiyo, Mesut Ozil, alikosa pia mchezo wa Liverpool kwa sababu ya majeraha, lakini mtandao wa Telegraph kupitia vyanzo vyake, unaamini kuwa Mjerumani huyo pia aliondolewa kwenye mchezo kwa sababu ya kumuunga mkono Sanchez.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, Ozil na Sanchez, wamekuwa na msuguano na mabosi wa Arsenal wakidai kuongezwa kiwango cha mshahara ili waweze kusaini mkataba mpya.

Mpaka sasa bado hawajasaini mkataba na kwa jinsi mambo yanavyoendelea ni wazi kuwa wawili hawa wanaweza kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -