Friday, October 23, 2020

JEURI YA MBELGIJI SIMBA HII HAPA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amekiangalia kikosi chake namna kilivyo kisha akatamka wazi kuwa watakaowasogelea mbele yao, watapata kipigo cha ‘mbwa koko’.

Licha ya kwamba jukumu la usajili lilikuwa limebebwa na msaidizi wake, Masoud Djuma, Mbelgiji huyo alisema wachezaji waliosajiliwa wana viwango vya juu hivyo mashabiki watarajie makubwa.

Kocha huyo alikuja wakati Simba wakimalizia suala zima la usajili lililosimamiwa na Djuma, lakini amevutiwa kwa kiasi kikubwa na wachezaji waliopo na kutamka bayana kuwa ni ‘watu wa kazi’ hasa.

Akizungumza na BINGWA jana, Mbelgiji huyo alisema leo ndio makali yao yatakapoanza kuonekana mbele ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mbelgiji huyo alisema kwa namna alivyowanoa vijana wake, ana imani watatetea ubingwa wao mapema, lakini pia watafanya vizuri katika michuano ya kimataifa inayowakabili.

“Ninacho kikosi kizuri sana, yaani kila nafasi inao wachezaji watatu wanaoweza kupambana ndani ya uwanja, nadhani tutafanya vizuri tukianzia na mchezo wetu wa kesho (leo dhidi ya Mtibwa).

“Maandalizi yetu yananifanya niamini kuwa hata kwenye Ligi Kuu tutakuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri, lakini pia na michuano ya kimataifa inayotukabili,” alisema.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wataiwakilisha nchi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao na Mbelgiji huyo ametamka wazi kuwa lazima wapambane kuhakikisha wanafika mbali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -