Wednesday, September 30, 2020

Jeuri ya Simba kwa Morrison hii hapa

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

NA ASHA KIGUNDULA

WAKATI hatma ya Bernad Morrison kuichezea Simba au kubaki Yanga ikitarajiwa kujulikana leo, imeelezwa kuwa inaonekana wazi Wekundu wa Msimbazi hawajakurupuka kumtangaza nyota huyo.

Simba juzi ilimtangaza Morrison kama mchezaji wao akionekana katika picha akisaini mkataba, huku Yanga wakiendelea kusisitiza kuwa Mghana huyo ni mali yao.

Hata hivyo, leo Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kutoa hukumu juu ya sakata hilo leo.

Lakini wadadisi wa mambo ya soka wanadai kuwa Simba si wendawazimu kumtangaza Morrison, wakisisitiza inawezekana kuna kitu wanajiamini.

“Simba wanaonekana kujiamini sana kwa suala hili la Morrison, inawezekana wanajua wanachokifanya. Wasi wasi wangu inawezekana walishamsaini mapema kabla ya Yanga kumwongeza mkataba mpya.

“Kama walifanya hivyo, basi wana haki naye kwani walimsaini akiwa ndani ya miezi sita ya mkataba wake na Yanga, jambo linaloruhusiwa kwa mujibu wa kanuni za usajili za FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

“Kinachoonekana, inawezekana Yanga waliposhtuka baada ya tetesi kuwa Morrison anatakiwa na Simba na kumpa mkataba, walikuwa wamechelewa. Lakini kama kweli Morrison alikuwa amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Yanga, hiyo ni kesi nyingine,” alisema mmoja wa wachambuzi maarufu wa soka hapa nchini.

Inaelezwa kuwa Simba walianza kuvutiwa na Morrison baada ya kuwafunga bao pekee la Yanga katika ushindi wa bao 1-0 Machi 8, mwaka huu.

Mbali ya bao hilo, pia kiwango alichoonyesha Morrison katika mchezo huo na mingine, kiliwafanya Simba chini ya Mwenyekiti wao wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji ‘Mo’ kukubaki kutoa fedha kumng’oa Jangwani.

Morrison alianza kuichefua Yanga Julai 2, mwaka huu kwa winga huyo kuigomea klabu hiyo kusafiri kwenda Shinyanga, huku Julai 12, mwaka huu akiwaaga mashabiki wa Wanajangwani hao na siku moja baadaye, kutangaza rasmi kumalizana nao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -