Thursday, November 26, 2020

JEURI YA YANGA IPO HAPA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

PAMOJA na Simba kutamba na kaulimbiu yao, ‘pira biriani’, Yanga jeuri yao ipo katika ukuta wa chuma ambao hadi sasa umeruhusu mabao mawili tu. Yanga itakuwa mwenyeji ikiikaribisha Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Wanajangwani hao wamecheza mechi tisa, wameshinda saba na sare mbili na  kukaa  kileleni na pointi 23. Kitendo hicho cha Yanga kuonekana moto, ikiwa timu ambayo haijapoteza mchezo kati ya 18 zinazoshiriki ligi hiyo, kinawapa presha watani zao wakiamini itakuwa si rahisi kupenya. Ukuta wa Yanga uliofanya kazi kubwa uliundwa na Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto, lakini pia hata ulipobadilishwa katika mechi iliyopita dhidi ya Gwambina uliendelea kuwa mgumu kupitika. Ukiwaondoa Lamine na Mwamnyeto, kuna Abdallah Shaibu ‘Ninja’, na Juma Makapu ambao wote wana uzoefu wa kucheza mapambano ya watani na kuwapa presha mastraika wa Simba. Katika kuongeza mzuka, Kocha Mkuu Cedric Kaze, aliwapumzika Lamine na Mwamnyeto, wakati walipokutana na Gwambina ili kutengeneza nguvu ya kukabiliana na Mnyama, mtanange unaovuta hisia kubwa za mashabiki wa soka nchini. Ukiachana na ukuta huo kuna viungo wakabaji wenye uwezo mkubwa  kama vile Tonombe Mukoko, Feisal Salum ‘Fei Toto’, huku eneo la ushambuliaji likitarajia kubebwa na  Farid Mussa, Michael Sarpong. Wanayanga wana imani kubwa na nyota hao kutokana na kiwango walichoonesha katika mechi zilizopita, licha ya kufunga mabao machache.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -