Tuesday, December 1, 2020

JINA LA MFALME WA TAARAB LINAVYOUTEKETEZA MUZIKI HUO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA KYALAA SEHEYE

MUZIKI wa taarabu ndiyo muziki ambao ulionekana kuendelea kulinda heshima yake tangu ulipoanzishwa na mababu zetu kutokana na warithi wake kufuata nyayo zile zile, huku wakiongeza vionjo vya kisasa.

Lakini kwa sasa muziki huo umeanza kuporomoka na kutoa mwanya kwa ule wa Bongo Fleva kushika kasi.

Kuna sababu kadha wa kadha zinazotajwa kuchangia hali hiyo, lakini wengi wakiamini ni kutokana na kupungua kwa ushindani baada ya aliyekuwa akiitwa Mfalme wa Taarab, Mzee Yusuph, kuachana na shughuli za muziki, huku pia akiagiza nyimbo alizowahi kuimba kutopigwa sehemu yoyote ile kutokana na uamuzi wake wa kumrudia Muumba wake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, BINGWA limefanya mahojiano na mmoja wa wataalamu wa muziki ambaye pia ni mwanamuziki wa muziki wa reggae, Innocent Nganyagwa ‘Ras Inno’, kujua nini chanzo cha kuanza kuporomoka kwa taarabu.

Ras Inno, anasema: “Mpaka sasa bado hakuna mfalme wa taarabu na itawachukua muda kumpata kwani kila mmoja anataka ajifanye yeye ndiye Mzee Yusuph, huku akiwa ameacha kabisa nyendo za Mzee na kufanya taarabu yake.

“Pamoja na Mzee Yusuph kuimba taarab ya kisasa (Morden Taarab), lakini katu hakutoka nje ya muziki asilia, sasa wao wanaimba mipasho na kudai kuwa wanaimba taarabu, hilo ndilo linalowapoteza.”

Ras Inno alifafanua kuwa kinachowashinda wasanii wa sasa kuendeleza muziki huo ni kutokana na kila mmoja kutaka kuvaa viatu vya Mzee Yusuph na kushindwa kuleta muziki wenye hadhi na viwango.

Anasema kuna wasanii wengi ambao wanashindwa kutumia uwezo wao walionao ili kufukia mapengo yaliyopo na kuifanya taarabu izidi kung’aa kama ilivyoachwa na Mzee Yusuph.

“Kwa mwelekeo unaoelekea, taarabu inaweza kufa kabisa kwa kupoteza mashabiki na kutoa nafasi kwa Bongo Fleva kutamba.

“Yule mama Mwanahawa Ally ana uwezo mkubwa sana kuliko hata watu wanavyodhani, ila hatumii uwezo wake na hata watunzi hawafahamu hilo, nina imani angeweza kuziba pengo lililoachwa na Mzee Yusuph kuliko hata hao wanaume wanaojivika ufalme wasiouweza.

“Mfano, Isha Mashauzi naona ameamua kuitelekeza kabisa taarabu na kuhamia kwenye rhumba, hii inazidi kuupoteza muziki wa taarabu kwa sababu ndiyo kipindi cha kujipanga, tunafahamu ana uwezo wa kuimba ila sasa achague moja, kubaki kwenye taarabu ili kuilinda au kwenda kwenye rhumba.”

Ras Inno aliongeza kuwa kama wasanii wanaoimba taarab wanahitaji kuwania kiti kilichoachwa na Mzee Yusuph, waunde ufalme wao unaoweza kuziba ufalme uliondoka na si kuvamia kwa juu.

“Hawana kitambulisho chochote ambacho kitamtambulisha mtu kwenye muziki, wamepoteza msingi wa taarabu, wakiwa na nia kweli warudi kwenye ujuzi na kufuata misingi ya taarabu kwani muziki huo una misingi yake na si wanavyoenda wao,” alisema.

Mkali huyo wa reggae alisema ikitokea siku Mzee Yusuph akarejesha mawazo na kurudi kwenye muziki, basi hao wanaojinadi kuwa wafalme wapya, watapotea na hata historia zao kufa kabisa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -